Naungana na Masanja. Watu tusiwe wepesi wa kutukana watu tu. Mengi ni mfanyabishara! Na kama management ya eatv inadhani hao vijana wanataka kukiuka sheria , lazima wa act! Jamani tusimamie sheria. Hao vijana si nao wameshakuwa wafanyabiashara (professional comedians)! Basi, wafuate sheria. Hii habari kwamba wataenda kumwona sijui waziri mkuu hadi rais haitawasaidia. Hao wanasiasa ndio watawachanganya kabisa! Wataishia kuihubiri CCM, na hatimaye watachuja! Watumie wanasheria, waende mahakamani. Tangu lini wanasiasa wakawa mahakama! Cha msingi aliyewanunua kichwakichwa awalipie hiyo copyright (kama hiyo ndio issue). Kuwapeleka Ulaya ni sponsor wao kutafuta publicity.
Hapa ndio shule inapokuwa muhimu kwa watanzania. Waangalie wenzao kenya (redikyulas) - wale vijana wanaelimu ya kutosha and they are doing a good business. Sasa hawa wangewatumia wataalamu (wanasheria). Wakikurupuka wataishia kuharibu kila kitu. Pia lazima waacknowledge eatv imeplay role kubwa sana 'kutoa'. Lakini hiyo siyo sababu ya kuwaendelea kuwa nao hasa kama kuna a greener pasture somewhere else.
Lakini wafuate sheria, wasitafute huruma (ya wamashabiki wao, wala wanasiasa).