Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

Ningekuwa mimi ndo wao, ningebadilisha kutoka "ZE Comedy" to "The Comedy." Mchezo kwisha.
 
Kwani ze Comedy ni jina la kikundi au la kipindi?
Kama ni jina la kipindi basi EATV watakuwa na haki nalo, ila iwapo ni jina la kikundi kilichosajiliwa basi wanaondoka na jina lao.
Majina ya waigizaji kama Joti, Masanja n.k hayamilikiwi na EATV.

...sijui Bongo, lakini ughaibuni Kipindi kinaondoka na mwanzilishi, i.e Larry King Live, Jerry Springer, hata Jackass wanaweza kuondoka na kipindi chao...

...
 
Mi nadhani hapa EATV na Mengi wanataka kujihami maana wameumbuka. Kama jina la kipindi Ze Comedy ni miliki ya EATV ni sawa tu, lakini character names ni lazima wathibitishe kuwa ni ya EATV ambacho tunajua si kweli maana hawa wasanii walitumia majina yao kabla ya Ze Comedy.
EATV wangecompromise, wabadilishe jina la kipindi na wao waendelee na jina hilo na wasanii wengine.
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe.
Wawaache vijana bwana ugomvi wa watu wengine wanataka tuaribia vijana wetu wakale wapi.
Joti akiingia mtaani si atakuwa mdokozi tuu.
 
COSOTA wamechemsha na kama kawaida itakuwa kitu kidogo kimepita hapo. Hawa Ze Comedy wamesajiliwa wakiwa huru. Kwani cheti chao kina jina la EATV? Sisi Watanzania tumezidi wivu. Ze Comedy endeleeni kama kawaida.
 
Nadhani ni fundisho kwetu sote. Ni vyema sote tukajifunza nini maana ya mkataba na athari zake. Mara nyingi tumekuwa tukisaini bila ya kusoma "fine prints"
 
vijana wanajituma .. vijisenti gani hivyo vya kupigania .. Mengi haoni hata aibu kuwakwamisha watoto wadogo kama hao? anataka wawe majambazi au ... yeye mbona anawaendeleza watoto wake ...

Lakini kweli Mungu alisema tajiri kuingia peponi ........ kumbe ni hayo
 
Nadhani ni fundisho kwetu sote. Ni vyema sote tukajifunza nini maana ya mkataba na athari zake. Mara nyingi tumekuwa tukisaini bila ya kusoma "fine prints"

Ni suala la haki miliki ambalo wao kama wasanii wanalilia kila siku. Huo ndio upande mwingine wa shilingi. Ze comedy sio yao, ni ya EATV kisheria. Wao wanaweza kubaki na majina yao lakini kama majina hayo yametokana na wao kuwa na mkataba na EATV au wamepewa majina hayo kutokana na kipindi hicho yatabaki kuwa ya EATV. Wakitaka kulitumia mahali pengine lazima walinunue na hiyo ndio full stop.

Wakitaka wanaweza kuja na kitu kipya lakini wajue Ze Comedy ndio trade mark. Kitu kingine kinaweza kisipate umaarufu kama Ze comedy katika nchi hii ya serikali ya Ki Ze comedy..

Na huko ndiko kupambana kishule achilia mabali kupelekwa Ulaya.
 
Ndo maana wazungu kila siku wanatupiga bao. Sisi tunapenda kusentimentalize mambo sana. Eti waonewe huruma..? you are kidding! Yes, kwa huruma eatv ni wanoko as some of us seem to suggest. But the other side of the coin, kulikuwa na Ze commedy kabla ya EATV? lets be analytical..huruma na sheria si kitu kimoja. EATV ndo waliwachukua kama kikundi chao cha burudani..sasa wao baada ya kupata umaarufu wakaona kwamba they can dispense with their employer...well, they can, lakini mpaka hapa EATV hawana kosa. Vijana wapewe ushauri wa kisheria. Kama wanataka wajipange upya waanzishe kundi lao walisajiri na kufanya wayatakayo.

EATV siyo wajinga....they know where the money is, na tatizo la TBC..wameamua kuwanunua hawa Ze Commedy baada ya kuona wamekuwa maarufu. But who gave them the platform to be maarufu? ni EATV..so EATV kama walisajiri kikundi chao....basi vijana..waanze upya.
 
vijana wanajituma .. vijisenti gani hivyo vya kupigania .. Mengi haoni hata aibu kuwakwamisha watoto wadogo kama hao? anataka wawe majambazi au ... yeye mbona anawaendeleza watoto wake ...

Lakini kweli Mungu alisema tajiri kuingia peponi ........ kumbe ni hayo

Acha kumuonea mengi..hapa ni akili tuu ya shule, hawa vijana waliingia kichwa kichwa..wakatumiwa na wakalipwa just like any other employer...ndo tatizo la kufanya biashara bila plans..wao hili sakata lote limetokea baada ya kuona kumbe aise...hii kitu inalipa..so we should go solo! Ndo hivyo mikataba mingi inavyotuumiza watu wa dunia ya tatu..we dont think ahead......

Jamani unataka mengi afanye nini sasa? au unataka kila kitu kiwe ujamaa?
 
Naungana na Masanja. Watu tusiwe wepesi wa kutukana watu tu. Mengi ni mfanyabishara! Na kama management ya eatv inadhani hao vijana wanataka kukiuka sheria , lazima wa act! Jamani tusimamie sheria. Hao vijana si nao wameshakuwa wafanyabiashara (professional comedians)! Basi, wafuate sheria. Hii habari kwamba wataenda kumwona sijui waziri mkuu hadi rais haitawasaidia. Hao wanasiasa ndio watawachanganya kabisa! Wataishia kuihubiri CCM, na hatimaye watachuja! Watumie wanasheria, waende mahakamani. Tangu lini wanasiasa wakawa mahakama! Cha msingi aliyewanunua kichwakichwa awalipie hiyo copyright (kama hiyo ndio issue). Kuwapeleka Ulaya ni sponsor wao kutafuta publicity.

Hapa ndio shule inapokuwa muhimu kwa watanzania. Waangalie wenzao kenya (redikyulas) - wale vijana wanaelimu ya kutosha and they are doing a good business. Sasa hawa wangewatumia wataalamu (wanasheria). Wakikurupuka wataishia kuharibu kila kitu. Pia lazima waacknowledge eatv imeplay role kubwa sana 'kutoa'. Lakini hiyo siyo sababu ya kuwaendelea kuwa nao hasa kama kuna a greener pasture somewhere else.

Lakini wafuate sheria, wasitafute huruma (ya wamashabiki wao, wala wanasiasa).
 
Sheria Ifwate Mkondo Wake
Waziri Hana Jipya La Kufanya Hapo
Vijana Rudini Kaeni Chini Na Eatv..msidanganyike Na Waziri Yoyote
Mtaishia Porini Na Kusahaulika....
 
kwani wakitaka kununua hati miliki kwa EATV watakataliwa?hile kesi iliyoshindikana iliyoamuliwa mahakamani yarudi kwenye sanaa manji vs mengi. nadhani manji naye anataka safari hii ashinde, basi atatumia fedha nyingi katika kushindana, wakati hizo pesa angewapatia tu wakanunua hiyo haki miliki toka kwa EATV.
jamani ehee dunia sijui ikoje ukiwa na fedha balaa, na kama huna ndiyo usiseme.
 
Leo hii wanadamu ndo wanaona kuwa ze comedy wanaonewa. Hiyo si kweli kwani wao walikuwa pale kama ajira. Walikuwa hawalipii vipindi na kila mwisho wa kipindi utaona tangazo la copyright ya eatv.

Sioni kosa kwa eatv bali naona kosa kwa hao waliokuwa wakijiita akina masanja kwa kumtosa mzalendo na kukimbilia kwa fisadi manji ili wapate makombo na hapo ndo watavuna mavuno halisi ya walichokipanda.

EATv kaza buti, msiwaachie hao jamaa kwa kuwa wamekula ya mbuzi wakaota mapembe.

Kwanza kabisa si kweli kwamba hawa jamaa walikuwa wabunifu kwani staili waliyokuwa wakitumia kurusha vipindi vyao ilitokana na staili ya kundi moja la Kenya na kuna kipindi nilisikia malalamiko kutoka kenya kwa wakenya kwa kusema kuwa jamaa wamewaigizia.

Na zaidi, kwani ni lazima uitwe masanja ili watu wacheke? Ama vichekesho ni hayo majina na staili za kutembea?

Kama mmeishiwa tafuteni tu-hela mpige shule mpate ajira nyingine.

wakora waitu!!
 
hawa jamaa wa eatv inaonyesha kuwa walikuwa wanashibisha matumbo yao kwa kupitia ZE comedy kwa nn wamewang'ang'ania wasitumie vipaji vyao??
Nao hao COSOTA inabidi wamulikwe labda kuna mkono wa mtu.
Lakini tuangalie upende wa shilingi labda kitendo cha hawa jamaa kuomba ulezi kwa Manji utakuwa umewaletea matatizo....si mnajua fika eatv ni ya Mengi sasa Mengi na Manji paka na panya...wanakomoana wakubwa huku wadogo wakiumia sasa.
 
Sasa akina mkandamizaji watajua kuwa 'kuna sheria' Tanzania.
Manji amewadanganya sasa wataula wa chuya.
 
Back
Top Bottom