Ze komedi...

Ze komedi...

Mi naona ww una bifu na original comedy hivi kuna watu gani wanachekesha kwa sasa au ze comedy ya EAC wale ungeolea ungeeleweka
 
kwisha kazi, vingi vizuri havidumu bila jitihada za kuboresha na ubunifu, zaidi watu ulewa sifa za kijinga, they fans are now below 10yrs of age
 
bado wana uwezo ila kwa sasa inabidi watoke kivingine kama wako kwenye wigo unaowabana kiasi hicho. Anyway ila nawakubali sana hawa EATV simajina makubwa kihivyo ila ubunifu wao. Kusema kweli kama channel ten wakitukumbusha michezo ya enzi hizo za king Majuto,na jamaa mmoja alifariki walikuwa wa ukweli!
 
Mimi naona tatizo ni sanaa ya Tanzania kwa ujumla, haijengwi kwenye misingi endelevu ndio maana hata mziki ukitoka una hit sana lakini in no time unakuwa umechuja vibaya mno.
Kwa maana hiyo nachelea kusema hata komedi ni wasanii wanaokumbwa na hali halisi ya kukosa ubunifu matokeo yake ni kuanzisha mitafaruku na watazamaji wao kwa katika jitiada za kuendeleza fanii.
 
Nowdays anaboa masanja sijui watu wake wa karibu hawamwambii.
Tutamchoka soon na repetitive style zake
 
Kauzu kama dagaa,ndoa ndoano unataka ubunifu gani give them suport,na ushauri ni mzuri kuliko kulaumu,tujaribu kupenda vyetu jamani
 
Ivi jana walidhamiria kuifurahisha audience gani? Labda watoto wa chekechea ndo walicheka aisee. Kwisha habari yao.
 
yote tisa,lakini sipendi kabisa tabia iliyoanzishwa ya wanaume kuigiza kama majike!naona imeenea mpaka kwenye tv nyingine.huu ni udhalilishaji kwa vijana wetu wa kiume na taifa kwa ujumla.inawezekana wanalazimishwa kufanya hivyo kwa sababu ya umaskini wao........tukemee kabisa tabia hii inayofanywa na matajiri wachache kutudhalilisha.wenzetu wakenya ni waigizaji wazuri sana lakini hata sikumoja hatujamuona mzee ojwang au mwala akiwa amevalishwa gauni.jamani watanzania tunaelekea wapi?mbaya zaidi upuuzi huo unaonyeshwa na televisheni ya taifa ambayo ilipaswa kulinda maadili ya mtanzania.hivi kweli umasikini umetufikisha hapa?.naomba kuungwa mkono katika kulikemea hili.ikiwezekana lifike bungeni!
 
Kuna laana hata kama mtu sio mzazi wako, malipo ni hapa hapa.

Wale watoto (Joti na Mpoki) Walikuwa pale na walikuwa wanalazimishwa enzi hizo mpaka director wao Seki, wanacheza cheza tu, hovyo kabisa wakaingia EATV wakapata umaarufu, wakapata umaarufu, wakajifanya wajanja, Hakuna mwanzo usiokuwa na Mwisho!.

Kauli za masanja ni mbovu sana bora watu wengine wowote lakini sio masanja!



Hawa wameshakwishilia mbali, bado kuwazika tu~
 
Back
Top Bottom