Zele mhuni sana badala ya kunyanyua bendera nyeupe juu anaomba mazungumzo

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,840
Reaction score
8,202
Rais Putin baada ya kutoa amri ya kutaka vita imalizwe kabla ya mwaka kuisha,mashambulizi ya Oreshnik yaendelea kwa kasi kubwa Kiev.

Z

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya ana kwa ana kati yake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika juhudi mpya za kutafuta suluhisho la kumaliza vita vinavyoendelea kati ya nchi hizo mbili.

Kupitia barua ya wazi aliyomwandikia Putin, Zelensky alisema kuwa ni muhimu viongozi hao wawili kukutana moja kwa moja ili kujadili njia za kurejesha amani.

Katika barua hiyo yenye zaidi ya maneno 1,800, Zelensky alisisitiza kwamba amani ya kudumu inaweza kupatikana tu kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Ukraine na Urusi.

Aliongeza kuwa haitakuwa sahihi kusubiri hadi Marekani irejee kuipa kipaumbele vita vya Ulaya baada ya kuelekeza nguvu zake kwenye migogoro mingine ya kimataifa, ikiwemo suala la Iran.

Zelensky pia alipendekeza kusitishwa kwa mapigano kwa kipindi chote cha mazungumzo hayo ili kutoa mazingira mazuri ya kufikia makubaliano.

Hata hivyo, Putin awali alikataa wazo la kusitisha mapigano kwa muda, akisisitiza kuwa bado kuna masuala muhimu yanayohitaji kujadiliwa kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote.

Serikali ya Urusi imethibitisha kupokea barua hiyo na kusema kwamba rais wa Urusi atapewa taarifa kamili kuhusu yaliyomo kabla ya kutoa msimamo rasmi.

Rais wa Marekani, Donald Trump, pia alitoa maoni yake kuhusu pendekezo hilo, akisema kuwa itakuwa jambo jema ikiwa viongozi hao wawili watakutana uso kwa uso. Wakati huo huo, Zelensky alipendekeza kwamba mazungumzo hayo yaweze kufanyika katika nchi isiyoegemea upande wowote kama Switzerland au Turkey.

Vita kati ya Urusi na Ukraine vilianza kwa uvamizi mkubwa wa Urusi mwezi Februari mwaka 2022 na vimesababisha maelfu ya vifo pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu. Licha ya majaribio kadhaa ya mazungumzo yaliyofanyika katika maeneo mbalimbali, juhudi za kufikia usitishaji wa mapigano zimekuwa zikikwama.

Pendekezo hili jipya la Zelensky linaonekana kuwa hatua nyingine muhimu katika kutafuta njia ya kumaliza mzozo huo wa muda mrefu.
 
... ushenzi unaofanywa na Marekani Duniani, ikiwa ni pamoja na Venezuela, Cuba na Mashariki ya kati, vimempa Putin mtazamo chanya miongoni mwa raia na viongozi wenzie ndani ya Russia na Dunia kwa ujumla wake! ... kwamba kupunguza kasi ya kupanuka kwa NATO, na sera zake za uvamizi, ni kitendo cha ukombozi Duniani!
GOD BLESS PUTIN AND THE RUSSIAN STRUGGLE!
 
Urusi hawezi sitisha vita kabla hajatimiza malengo yake.
Njia ya kutumia mazungumzo ili Ukraine ajizatiti na kujipanga walishaishtukia.

Hizi vita mbili zitaenda na chumi za nchi nyingi sana duniani. Hasa ulaya
Kutokana na sera za ubabe zilizoonyeshwa na Marekani, malengo sahihi kwasasa ni kiukamata Ukraine yote na kuitawala! Hiyo ndiyo njia pekee ya kuweka mzani sawa Duniani!
DUNIA HAIFAIDIKI CHOCHOTE NA UBABE WA TAIFA LA WABINAFSI LA MAREKANI!
 
... ushenzi unaofanywa na Marekani Duniani, ikiwa ni pamoja na Venezuela, Cuba na Mashariki ya kati, vimempa Putin mtazamo chanya miongoni mwa raia na viongozi wenzie ndani ya Russia na Dunia kwa ujumla wake! ... kwamba kupunguza kasi ya kupanuka kwa NATO, na sera zake za uvamizi, ni kitendo cha ukombozi Duniani!
GOD BLESS PUTIN AND THE RUSSIAN STRUGGLE!
DOES PUTIN BELIEVE IN THE LIVING GOD ?
 
Raisi Putin baada ya kutoa amri ya kutaka vita imalizwe kabla ya mwaka kuisha,mashambulizi ya Oreshnik yaendelea kwa kasi kubwa Kiev.​

Z

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya ana kwa ana kati yake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika juhudi mpya za kutafuta suluhisho la kumaliza vita vinavyoendelea kati ya nchi hizo mbili.
Kupitia barua ya wazi aliyomwandikia Putin, Zelensky alisema kuwa ni muhimu viongozi hao wawili kukutana moja kwa moja ili kujadili njia za kurejesha amani.
Katika barua hiyo yenye zaidi ya maneno 1,800, Zelensky alisisitiza kwamba amani ya kudumu inaweza kupatikana tu kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Ukraine na Urusi. Aliongeza kuwa haitakuwa sahihi kusubiri hadi Marekani irejee kuipa kipaumbele vita vya Ulaya baada ya kuelekeza nguvu zake kwenye migogoro mingine ya kimataifa, ikiwemo suala la Iran.
Zelensky pia alipendekeza kusitishwa kwa mapigano kwa kipindi chote cha mazungumzo hayo ili kutoa mazingira mazuri ya kufikia makubaliano. Hata hivyo, Putin awali alikataa wazo la kusitisha mapigano kwa muda, akisisitiza kuwa bado kuna masuala muhimu yanayohitaji kujadiliwa kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote.
Serikali ya Urusi imethibitisha kupokea barua hiyo na kusema kwamba rais wa Urusi atapewa taarifa kamili kuhusu yaliyomo kabla ya kutoa msimamo rasmi.
Rais wa Marekani, Donald Trump, pia alitoa maoni yake kuhusu pendekezo hilo, akisema kuwa itakuwa jambo jema ikiwa viongozi hao wawili watakutana uso kwa uso. Wakati huo huo, Zelensky alipendekeza kwamba mazungumzo hayo yaweze kufanyika katika nchi isiyoegemea upande wowote kama Switzerland au Turkey.
Vita kati ya Urusi na Ukraine vilianza kwa uvamizi mkubwa wa Urusi mwezi Februari mwaka 2022 na vimesababisha maelfu ya vifo pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu. Licha ya majaribio kadhaa ya mazungumzo yaliyofanyika katika maeneo mbalimbali, juhudi za kufikia usitishaji wa mapigano zimekuwa zikikwama. Pendekezo hili jipya la Zelensky linaonekana kuwa hatua nyingine muhimu katika kutafuta njia ya kumaliza mzozo huo wa muda mrefu.
Mbona kichwa cha habari na mada iliyopo haviendani? Wapi amenyanyua bendera nyeupe?
 
Trump mwenyewe kaona hebu ngoja nikae pembeni kidogo, niipigie kelele Israel halafu Ukraine si itakuwa balaa. Kwanza wale Cossacks wanajuana watajua jinsi ya kumaliza vita zao.
 
Raisi Putin baada ya kutoa amri ya kutaka vita imalizwe kabla ya mwaka kuisha,mashambulizi ya Oreshnik yaendelea kwa kasi kubwa Kiev.​

Z

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya ana kwa ana kati yake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika juhudi mpya za kutafuta suluhisho la kumaliza vita vinavyoendelea kati ya nchi hizo mbili.
Kupitia barua ya wazi aliyomwandikia Putin, Zelensky alisema kuwa ni muhimu viongozi hao wawili kukutana moja kwa moja ili kujadili njia za kurejesha amani.
Katika barua hiyo yenye zaidi ya maneno 1,800, Zelensky alisisitiza kwamba amani ya kudumu inaweza kupatikana tu kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Ukraine na Urusi. Aliongeza kuwa haitakuwa sahihi kusubiri hadi Marekani irejee kuipa kipaumbele vita vya Ulaya baada ya kuelekeza nguvu zake kwenye migogoro mingine ya kimataifa, ikiwemo suala la Iran.
Zelensky pia alipendekeza kusitishwa kwa mapigano kwa kipindi chote cha mazungumzo hayo ili kutoa mazingira mazuri ya kufikia makubaliano. Hata hivyo, Putin awali alikataa wazo la kusitisha mapigano kwa muda, akisisitiza kuwa bado kuna masuala muhimu yanayohitaji kujadiliwa kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote.
Serikali ya Urusi imethibitisha kupokea barua hiyo na kusema kwamba rais wa Urusi atapewa taarifa kamili kuhusu yaliyomo kabla ya kutoa msimamo rasmi.
Rais wa Marekani, Donald Trump, pia alitoa maoni yake kuhusu pendekezo hilo, akisema kuwa itakuwa jambo jema ikiwa viongozi hao wawili watakutana uso kwa uso. Wakati huo huo, Zelensky alipendekeza kwamba mazungumzo hayo yaweze kufanyika katika nchi isiyoegemea upande wowote kama Switzerland au Turkey.
Vita kati ya Urusi na Ukraine vilianza kwa uvamizi mkubwa wa Urusi mwezi Februari mwaka 2022 na vimesababisha maelfu ya vifo pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu. Licha ya majaribio kadhaa ya mazungumzo yaliyofanyika katika maeneo mbalimbali, juhudi za kufikia usitishaji wa mapigano zimekuwa zikikwama. Pendekezo hili jipya la Zelensky linaonekana kuwa hatua nyingine muhimu katika kutafuta njia ya kumaliza mzozo huo wa muda mrefu.
Vita huwa inamalizwa tu bila kupanga ratiba. Bita si mchezo wa soka uzwma tutamaliza mchezo kwa dakika fulani.

Ukisikia kiongozi anapanga ratiba vita imalizike kwa tarehe fulani, wakati vita inaendelea bado, huyo anayetaka kumaliza vita kwa ratiba ya kutangazia dunia ndiye anayenyanyua bendera nyeupe.

Putin alifikiri hii vita anaweza kuimaliza kirahisi, uhalisia umekuwa tofauti sana.
 
PUTIN NA TRUMP WALIKURUPUKA KUANZISHA VITA KWA UKRAIN AND IRAN RESPECTIVELY. SASA WANAOANA HADI AIBU KUCHUTAMA.
 
Kutokana na sera za ubabe zilizoonyeshwa na Marekani, malengo sahihi kwasasa ni kiukamata Ukraine yote na kuitawala! Hiyo ndiyo njia pekee ya kuweka mzani sawa Duniani!
DUNIA HAIFAIDIKI CHOCHOTE NA UBABE WA TAIFA LA WABINAFSI LA MAREKANI!
Mtasubiri sana!!! Putin hawezi kushinda hii vita kipigo anachopata hamuambiwi tu mkia bila ndipo mtajua kwa nini Russia kushindwa kuimaliza hii vita. Ilikuwa masaa 72 sasa hivi miaka 5 na wajinga Kama nyie Mnajidanganya kuwa atashinda!!
 
We ndugu yangu utaendelea kuimba Yesu mpaka mabomu ya Marekani yatakapositisha uhai wako!
Umepofushwa na dini ambayo adui wa Dunia anaitumia tu kwa manufaa yake ilhali yeye mwenyewe ni Luziferi tu aliyejivika vazi la malaika!
 
Back
Top Bottom