Zelensky: Askari wa Urusi wanatega mabomu ya ardhini wanapoondoka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewaonya watu wake mapema leo Aprili 2, 2022 kuwa wanajeshi wa Urusi wanaoondoka katika maeneo yao wanatengeneza kile amesema ni "mazingira ya maafa" nje ya mji mkuu kwa kutega mabomu ya ardhini katika eneo zima hata karibu na nyumba za watu na maiti.

Ametoa onyo hilo wakati mzozo wa kiutu katika mji uliozingirwa wa Mariupol ukitokota. Wanajeshi wa Urusi walizuia operesheni za kuwahamisha watu kwa siku ya pili mfululizo hapo jana.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema litajaribu tena asubuhi hii kuingia katika mji huo. Wakati huo huo, Moscow imewatuhumu Waukraine kwa kufanya shambulizi la kutumia helikopta kwenye ghala la mafuta katika ardhi ya Urusi.

Ukraine imekanusha kuhusika na mripuko huo, uliotokea katika mji wa Belgorod. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema shambulizi hilo haliweki mazingira mazuri ya kuendelea kwa mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi.

Source: DW
 
kinachoenda kutokea hapa ni kama kile kilichotokea kule Syria na Venezuela wakati Mmarekani na watu wake wa nato walipojaribu kuingiza nguvu za kijeshi ili kuchomeka Viabaraka wao waendelee kuchota radilimali kama kule libya

Ila kilichowakwamisha ni baada ya Mrusi kuingilia kati na kupeleka majeshi yake pamoja na kumwaga zana zake za ulinzi wa anga ikawa ngumu kwa marekani kuiangusha Syria na Venezuela

Vile vile uvamizi wa Putin Ukraine umekumbana na yale yale ya Ukraine kusaidiwa na kupewa silaha za kutosha ndio maana hii Iperation imekuwa ngumu na huenda Putin asiweze kabisa kuikwapua Ukraine maana tayari Nato kashajiingiza kimya kimya na Urusi anapigana na Nchi nyingi ndio maana anapata shida
 
Putini ni mnafiki na muoga sana, Ivi yule putini niliyekuwa naskia ni yuko wapi? amekuwa coward kiasi hiki, vita ameshindwa mchana kweupe lakini ana na unafiki wa ajabu sana sasa kwanini anaondoka na atege mabomu ni ishara ya woga
 
Watu wanabadili mbinu..........walishasema awamu ya kwanza imekamilika..........hii kitu kuisha bado sana
 
Putini ni mnafiki na muoga sana, Ivi yule putini niliyekuwa naskia ni yuko wapi? amekuwa coward kiasi hiki, vita ameshindwa mchana kweupe lakini ana na unafiki wa ajabu sana sasa kwanini anaondoka na atege mabomu ni ishara ya woga
Ha ha ha hakuna taifa nililokuwa naliheshimu ktk medani ya vita kama Russia, ila toka vita hii ianze, taratibu naanza kuondoa imani yangu kwa Russia.
 
kinachoenda kutokea hapa ni kama kile kilichotokea kule Syria na Venezuela wakati Mmarekani na watu wake wa nato walipojaribu kuingiza nguvu za kijeshi ili kuchomeka Viabaraka wao waendelee kuchota radilimali kama kule libya

Ila kilichowakwamisha ni baada ya Mrusi kuingilia kati na kupeleka majeshi yake pamoja na kumwaga zana zake za ulinzi wa anga ikawa ngumu kwa marekani kuiangusha Syria na Venezuela

Vile vile uvamizi wa Putin Ukraine umekumbana na yale yale ya Ukraine kusaidiwa na kupewa silaha za kutosha ndio maana hii Iperation imekuwa ngumu na huenda Putin asiweze kabisa kuikwapua Ukraine maana tayari Nato kashajiingiza kimya kimya na Urusi anapigana na Nchi nyingi ndio maana anapata shida
Umejibu sahihi, kwanza jua UKRAINE Kwa nguvu kijeshi Duniani ni ya 22 , msidhani ni kanchi Kama TANZANIA Au Kenya, Duniani mwaka 1990 UKRAINE upande wake ndo ulikuwa unaongoza kwa Nuclear, na wana spy system nzuri kuzidi nchi nyingi, pia wana Jeshi kubwa japo halifiki viwango vya Urusi, hivo Russia walifanya miscalculation kudhani adhma yao itatimia kirahisi
 
huoni unachoongea ni kinyume chake , urusi ilimlinda Assad ila West inamlinda Zelewisky
 
Putini ni mnafiki na muoga sana, Ivi yule putini niliyekuwa naskia ni yuko wapi? amekuwa coward kiasi hiki, vita ameshindwa mchana kweupe lakini ana na unafiki wa ajabu sana sasa kwanini anaondoka na atege mabomu ni ishara ya woga
Nato aingie kumsaidia, anasubiri nini?
 
Kama kweli hii nihabari njema sana
Watege mabomu yakutosha ili watu wengi wafe vyakutosha
VIVA PUT IN
 
Mabomu ya ardhini yalishapigwa marufuku vitani sababu ya athari zake za muda mrefu

Msumbiji na Sudan kusini wana Ardhi zenye rutuba sana lakini maeneo mengi yana mabomu ya ardhini.Ukienda kulima unalipukiwa na bomu

Putin lazima apelekwe mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita the Hague he is a butcher wa current generation ns future generation
 
kinachoenda kutokea hapa ni kama kile kilichotokea kule Syria na Venezuela wakati Mmarekani na watu wake wa nato walipojaribu kuingiza nguvu za kijeshi ili kuchomeka Viabaraka wao waendelee kuchota radilimali kama kule libya

Ila kilichowakwamisha ni baada ya Mrusi kuingilia kati na kupeleka majeshi yake pamoja na kumwaga zana zake za ulinzi wa anga ikawa ngumu kwa marekani kuiangusha Syria na Venezuela

Vile vile uvamizi wa Putin Ukraine umekumbana na yale yale ya Ukraine kusaidiwa na kupewa silaha za kutosha ndio maana hii Iperation imekuwa ngumu na huenda Putin asiweze kabisa kuikwapua Ukraine maana tayari Nato kashajiingiza kimya kimya na Urusi anapigana na Nchi nyingi ndio maana anapata shida
Hapana ni tofauti, mfano uliotoa wa Syria ni kwamba majeshi ya Russia yalikuwepo physically ndani ya nchi wakiwa equipped na vifaa kama vyote. Ukraine hakuna officially hata mguu mmoja wa jeshi la marekani ama NATO kuwepo
 
Umejibu sahihi, kwanza jua UKRAINE Kwa nguvu kijeshi Duniani ni ya 22 , msidhani ni kanchi Kama TANZANIA Au Kenya, Duniani mwaka 1990 UKRAINE upande wake ndo ulikuwa unaongoza kwa Nuclear, na wana spy system nzuri kuzidi nchi nyingi, pia wana Jeshi kubwa japo halifiki viwango vya Urusi, hivo Russia walifanya miscalculation kudhani adhma yao itatimia kirahisi
Sasa mbona Krimea ilichukuliwa kiajabu ajabu bila resistance?
 
Back
Top Bottom