Zembwela katika Super mix

Zembwela katika Super mix

Habari wakuu,

Nimekuwa msikilizaji mzuri wa kipindi cha supa mix cha East africa Radio kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana. Kipindi hiki kinatangazwa na Zembwela (mchekeshaji wa zamani) na mwanadada mwingine.

kinachonikera katika kipindi hiki ni upotoshaji mkubwa wa Zembwela, ambaye siamni kama ana elimu nzuri (kulingana na hoja zake) zaidi ya kuongea mambo asiyoyajua hovyo hovyo. Kazi yake kubwa ni kukebehi wabunge, serikali za mitaa n.k. bila kutoa uchambuzi yakinifu. Utangazaji huu haufai kwa maendeleo ya taifa kwani mtangazaji anatakiwa kuchambua jambo ambalo ana ufahamu nalo, na iwapo hana ufahamu wa kutosha basi aalike wataalamu wa fani husika ili watoe habari kwa kina.

Zembwela anaropoka ovyo kiasi cha kukera wasikilizaji makini,

Rai - Zembwela ulikuwa mchekeshaji mahiri, usikurupukie fani ambazo una uelewa finyu. Nakushauri uwe na busara ukufahamu kuwa unasikiliza na watanzania wenye uelewa tofauti, punguza uropokaji usio na tija.

Nashindwa kukuelewa humpendi kwa uropokaji wake au kwa kugusa uchafu mnaofanya katika jamii.

Mkuu ni mara Milioni umsikilize Zembwela ambaye anafichuo uovu katika jamii na serikali bila kuogopa na kutoa ufisadi wa aina mbalimbali kuliko kuwasikiliza Jahazi wale wenye matatizo ya mtindio ubongo kama jina lake Kibonde.
Wamekaa pale kuongea Propaganda tu na kusifia upuuzi wa Serikali nao sijui wanataka Ukuu wa Wilaya au ndo kujipendekeza?

Keep it up Zembwela unajua unachofanya ulikua na uwezo wa kujipendekeza na kuifagilia Serikali yako lakini ukaona hapana. Chukulia hizo ni Challenge tu katika kazi yako.
 
Mkuu hiyo username yako ni Dr.kweli au ile ya kupewa kama Mkuu wa Kaya? Maana napata tabu kuelewa uwezo wako,,hao wadhamini ndio wanaoendesha hicho kipindi kwahiyo bila wao huwezi kumsikia Zembwela wa Irene.
Sasa hapo wewe hujaelewa nini....zamani RTD walikuwa na mda wa nusu saa ....wa kipindi cha mziki na matangazo....sasa kama talk show mziki na matangazo ni mengi kuliko talk yaenyewe...si bora uite kipindi cha mziki na matangazo....sijui kama utaelewa logic yangu maana huku jf napo...!!
 
Zembwela aunganishwe kwenye kundi la Comedy pamoja na kina Bambo kule ndiyo kwenye Talent yake, tusipende kulazimisha fani.

Mtu anaropoka tu mwanzo mpaka mwisho wa kipindi halafu panatokea watu hapa eti mnamsifia!! labda ninyi ni Waswazi wenzake ndio maana anawakonga nyoyo, kwangu mimi Zembwela ni useless.

Sintoshangaa wengine nikisikia mnapendekeza awe Mbunge maana anasema ukweli, kama ukweli huwa unaongelewa bila logic na mpangilio basi Baadhi ya Watanzania wenzetu mna zaidi ya tatizo.
 
Habari wakuu,

Nimekuwa msikilizaji mzuri wa kipindi cha supa mix cha East africa Radio kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana. Kipindi hiki kinatangazwa na Zembwela (mchekeshaji wa zamani) na mwanadada mwingine.

kinachonikera katika kipindi hiki ni upotoshaji mkubwa wa Zembwela, ambaye siamni kama ana elimu nzuri (kulingana na hoja zake) zaidi ya kuongea mambo asiyoyajua hovyo hovyo. Kazi yake kubwa ni kukebehi wabunge, serikali za mitaa n.k. bila kutoa uchambuzi yakinifu. Utangazaji huu haufai kwa maendeleo ya taifa kwani mtangazaji anatakiwa kuchambua jambo ambalo ana ufahamu nalo, na iwapo hana ufahamu wa kutosha basi aalike wataalamu wa fani husika ili watoe habari kwa kina.

Zembwela anaropoka ovyo kiasi cha kukera wasikilizaji makini,

Rai - Zembwela ulikuwa mchekeshaji mahiri, usikurupukie fani ambazo una uelewa finyu. Nakushauri uwe na busara ukufahamu kuwa unasikiliza na watanzania wenye uelewa tofauti, punguza uropokaji usio na tija.

kaka mbona na wewe pia ni kama umeropoka kwa usilolijua maana umeshindwa hata kutuambia alipotosha jambo gani?jipangeee
 
Tatizo vyombo vya habari vinashindwa kuajiri wasomi kwa sababu ya kupenda mtelemko,wanaishia kuchukua makanjanja wa mtaani,pale alipo Zembwela sina uhakika kama ana mkataba wa ajira.

wasomi wenyewe nyie makanjanja,kijana kazi anaiweza mwache apige kazi,nyie mnaojiita wasomi endeleeni kutoka povu na kubwabwaja tu.
 
Zimbwela ni mropokaji,na hana elimu ya kutosha na hakijui anchoongea,kila anachoongea huwa anaropika,ni moja ya watu wanaokariri na kufanyia kaz maneno ya vijiweni.cha ajabu anadhani ndo sifa kukashfu na kuongea habar za siasa nakati hata sheria hajui.kuna mwenzake anaitwa kibonde,sasa bora zembwela kibonde nahisi hata akili yake ni kama jina lake anajipendekeza kwa serikali ambayo hata haimjali.na kila kitu ye anapinga

mbona wewe ulikariri yale ulikuwa ukifundishwa darasani,je utajiita msomi kwa kukarir? Bora jamaa ana elimu ya kawaida lakini ana uelewa wa hali ya juu.
 
Tatizo vijana wengi siku Tanzania kujidai wao ndio wamesoma sana na wanajua vitu vingi sana kumbe hamna lolote,elimu wanayojidaia wengine wameinunua kwa peas,wengine wamehonga miili yao ili wafaulu na wengi wao walikariri kile walichofundishwa bila kuchanganua,mwisho wa siku mnakuja kutusumbua mitaani eti nimesoma na mnatukashifu tusiosoma.

Katika dunia hii wasiosoma ndio wenye maendeleo makubwa,wewe endelea kujidai umesoma sana kushinda wengine utakufa na ujivuni wako.
 
Habari wakuu,

Nimekuwa msikilizaji mzuri wa kipindi cha supa mix cha East africa Radio kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana. Kipindi hiki kinatangazwa na Zembwela (mchekeshaji wa zamani) na mwanadada mwingine.

kinachonikera katika kipindi hiki ni upotoshaji mkubwa wa Zembwela, ambaye siamni kama ana elimu nzuri (kulingana na hoja zake) zaidi ya kuongea mambo asiyoyajua hovyo hovyo. Kazi yake kubwa ni kukebehi wabunge, serikali za mitaa n.k. bila kutoa uchambuzi yakinifu. Utangazaji huu haufai kwa maendeleo ya taifa kwani mtangazaji anatakiwa kuchambua jambo ambalo ana ufahamu nalo, na iwapo hana ufahamu wa kutosha basi aalike wataalamu wa fani husika ili watoe habari kwa kina.

Zembwela anaropoka ovyo kiasi cha kukera wasikilizaji makini,

Rai - Zembwela ulikuwa mchekeshaji mahiri, usikurupukie fani ambazo una uelewa finyu. Nakushauri uwe na busara ukufahamu kuwa unasikiliza na watanzania wenye uelewa tofauti, punguza uropokaji usio na tija.
mkuu tatizo za redio zetu ndo hizi wanaajiri kisaa umaarufu,nilienda east africa na degree yangu ya mass communication kilicho nisibu acha tu.kachukuliwa ndugu doh salalaa ila wanaharibu hii fan kabisa kwa kubebana
 
WEWE kuwa na degree sio kigezo tosha cha kukufanya wewe upate kazi. Labd east afrika katika Kuwafanyia Mahojiano Walikuona hauna mvuto wa utangazaj ingawa ulikuwa na degree, Labda Muda Huo ulioenda kuomba kaz walikua hawaitaj mtu mwenye elimu ya degree, Pia unaweza ukawa na degree usiwe na uzoefu, angali yule DULLA wa planet BONGO alikua na umaarufu gani ? na elimu yake mbona ilikua ndogo sana ukilinganisha na yule alan laki wa skonga, Ndo athari za elimu za kiafrika kukalili mambo ya darasani mpaka mambo ya mtaan , yaan wewe unafikiri ukiwa tu na degree ya mass comminication hata kama first class bas umepata kazi, Afu kwa taarifa yako nyie Wasomi Weng ndo mmekua mkiharibu hii nchi kwasababu ya kukalili, JE, WEWE UNAUJASIR WA KUTANGAZA KAMA ZEMBWELA NA HIYO DEGREE ?
 
Zembwela aunganishwe kwenye kundi la Comedy pamoja na kina Bambo kule ndiyo kwenye Talent yake, tusipende kulazimisha fani.

Mtu anaropoka tu mwanzo mpaka mwisho wa kipindi halafu panatokea watu hapa eti mnamsifia!! labda ninyi ni Waswazi wenzake ndio maana anawakonga nyoyo, kwangu mimi Zembwela ni useless.

Sintoshangaa wengine nikisikia mnapendekeza awe Mbunge maana anasema ukweli, kama ukweli huwa unaongelewa bila logic na mpangilio basi Baadhi ya Watanzania wenzetu mna zaidi ya tatizo.

Kumbe kwako wewe ni useless, basi kwetu sisi ZEMBWELA ni useful, kwan kuna kitu gani cha upekee katika ubunge mpaka wewe ushangae watu kumpendekeza zembwela kuwa mbunge? Logic katika maana ya a way of thinking or explaining bas huyu jamaa anaongea ukwel wenye logic, na kuwa comedian haikuzuii mtu kufanya kaz nyingine, hivyo jamaa huyu ni mtangazaji jasiri ambaye kisha wahi kutishiwa mpaka maisha yake, kwa misimamo yake katika utangazaji, lakini bado anasonga mbele.
 
Hah hah hah Redio Tumaini wale wanaomaliza kusali Sala ya Salam Maria kisha wanapiga Mugongo Mugongo ya Twanga?

We jamaa kweli unatumia kichwa kubebea mashkio hayo

hahahahaha Gang Chomba umenichekesha sana, yani nilitune hii radio siku moja nilishangaa sana daa hawa jamaa wanachekesha sana
 
Last edited by a moderator:
ukimuona anavyojikunja akiwa anatangaza utacheka
 
mbona zembwela ni mkali tu wana au unakitaka kibarua nini?
 
Zembwela ni hulka yake kusema kitu ambacho yeye anakiamin kuwa ni sahihi,wapo wanaoona si sahihi kwa sababu si wao walosema.

Hivyo kama zembwela kwa nafasi yake ni sahihi kunena yale ambayo anaamini,pia anaweza kuwa alikosea au alitafsiriwa vbaya na mleta uzi na hyo haisemi kwamba hafai kwani walomuweka wanaamini anakidhi matwaka yao.hujawahi kujiuliza hayo anayosema ni ya kwake au ya redio??
 
Hao tunawaita waimbaji akija kwenye onyesho anakwambia,weka cd niimbe!..
Ni kama ilivyo kwa tasnia ya muziki yaani kila mtu anataka kuwa mwanamuziki, wao wanajiita eti wasanii, usisahau na wacheza filam huko ndo utacheka.
 
Back
Top Bottom