Zembwela wa Wasafi FM aitaka Serikali iruhusu Uvutaji wa Bangi kwa Wanaohitaji huku akiisifia mno

Maoni anayatolea Redioni Wasafi FM? Are you Okay Mentally?
haha ulitaka akayatolee wapi yeye kama mwananchi wa kawaida?

sio kila maoni yakatolewe bungeni
wengine kwao ni haramu hata kuangalia hilo bunge la ccm likiwa live

ppm tukuka
hahha
 
Siku hizi Wadai haki za Kizandiki wanaongezeka kila uchwao , Mtu kujitokeza na kuhamasisha watu watumie dawa za Kulevya huwezi kumtofautisha na hawa wadai haki za Kishoga
Sahihi mkuu. Huwa mambo yanaanza hivi hivi taratibu kimasiara baadae yanakua kwa kasi na kupata wafuasi wa kuyapambania yahalalishwe.
 
Mkuu GENTAMYCINE si unajua huyo jamaa ni comedian? Huenda alikuwa anachekesha tu watanzania turuhusiwe kuvuta bangi. Kwa kuwa tunajua madhara ya bangi wengine hatutavuta bangi hata kama ikiruhusiwa kama ilivyo tumbaku
 
Mkuuu genta akimaliza betina kuongea naomba uanzishe Uzi uje na hoja zake zote kwa ujumla wake
 
Yani mru kutoa maoni yake tu ndiyo iwe nongwa mpaka unataka TCRA wamchukulie hatua? Sasa Uhuru wa maoni upo wapi?

Kwa zembwela ninayemjua mimi endapo mwandika uzi angekuwa anakufahamu kwa jinsi ulivyoandika ukuda na kumkanyagia hivi,leo ungeumuka mwili Kama mkate maana angekupiga kata funua nyingi sana.
 
Sahihi mkuu. Huwa mambo yanaanza hivi hivi taratibu kimasiara baadae yanakua kwa kasi na kupata wafuasi wa kuyapambania yahalalishwe.

Wasafi inabidi wapigwe ban haraka sana kwa kukiuka taratibu na kutoa Maudhui yasiyofaa kwa public, huku ni kudhorotesha juhudi zinazofanywa na Serikali
 
Nakumbuka mwaka 2002 pale diamond jubilee kulikuwa na tamasha pale la wasanii kipindi hicho akina jumla nature wapo jukwaaani wanatumbuiza huyu zembwela na wahuni wenzake walikuwa wanavuta bangi chooni na wengine wanasaga unga, zamani uvutaji bangi mbele za watu ilikuwa fashion
 
Turuhusu wawekezaji waje kusindika bangi na kuuza. Tutoe elimu namna ya kulima bangi ambayo tunaweza uza ata kimataifa.

Bangi oye, zembwela oye, Tulia oye
 
Tena usinitibue kabisa nikayaanika yake mengineyo hapa na mkamdharau mazima.
 
Kuhamasisha uvutaji wa bangi hakuna tofauti kubwa na kuhamasisha ushoga, wasiotumia bangi watakasirika lakini wanaoivuta kama hayati Bob Marley hutawaambia kitu. Wanaoiona bangi nzuri ni wale wanaoivuta na haijawahi kuwaletea madhara yeyote kiafya. Hivi umewahi kushuhudia vijana waliopatwa na maradhi ya akili kisa kuvuta bangi?, unaweza kukisia takwimu za wale waliochanganyikia akii shauri ya kuvuta bangi? Sasa elewa tu kwamba wale waliokaa na kuharamisha bangi siyo vichaa na walielewa fika madhara ya mmea huu.

Ubongo wa kila mwanadamu ni tofauti na hatulingani katika viwango vya kuhimili madhara yatokanayo na kemikali au dawa mbalimbali. Kuna watu huvuta sigara mpaka miaka hata 100 na hawapatwi na kansa kabisa lakini wapo watu wengi tu hata kuwa karibu na mvuta sigara kwa muda mrefu unasikia tayari kapatwa na kansa. Sasa akili ya kuambiwa changanya na yakwako usiwe juha kufuata kila anachosema au kufanya mtu maarufu hata ikiwa ni Bob marley au Zembwela, huwezi jua ubongo wako ni dhaifu kiasi gani wewe kabugie mimoshi ya bange, utakapokuwa ukihangaika Muhimbili au Mwananyamala ni shauri lako. Nina ushahidi Bangi ni moja kati ya vitu vinavyochangia kutibuka kwa magonjwa ya akili. Hakuna binadamu asiyekuwa kichaa ila kichaa halisi huja baada mtu kupalilia vichokoo vyake.
 
Shida ya hawa watu wasio na taaluma ya utangazaji ni kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…