Ziara Maalum ya RC Makalla Kigamboni yabaini eneo la Avic Town na GSM walilopewa Yanga SC lina Mgogoro wa Ardhi

Ziara Maalum ya RC Makalla Kigamboni yabaini eneo la Avic Town na GSM walilopewa Yanga SC lina Mgogoro wa Ardhi

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Wakazi wa Kigamboni mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla wamesema kuwa Mmiliki wa eneo la Avic Town ambako ndiko Klabu ya Yanga kupitia Mdhamini wao GSM amewadhulumu eneo hilo na wanataka Haki itendeke Kwao.

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tunasikitika sana huyu Avic Town amejimilikisha eneo lote hili Kubwa na Kusababisha Watu 234 tukose Maeneo hapa wakati Kisheria ilikuwa ni Haki yetu kutokana na Vikao tulivyokaa huko nyuma na Waziri Lukuvi kwa Maagizo ya Hayati Rais Dkt. Magufuli" alisema Mmoja wa Wazee.

Hata hivyo wakati Mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla na Wakazi wa Kigamboni ukiendelea Mkuu huyo ametaka Maelezo zaidi kutoka Wizarani ya kwanini Mtu Mmoja Avic Town (GSM Wadhamini wakuu wa Yanga SC) wakiwemo wapewe eneo lote hilo peke yao na Wakazi Wengine wenye Haki nalo Kunyimwa.

Mkuu wa Mkoa Amos Makalla hongera sana kwa Kuliibua hili la Avic Town (GSM Wadhamini wakuu wa Yanga SC wakiwemo) na Mimi Mightier nakuomba ulipiganie vilivyo ili Avic Town (GSM na Yanga SC yao) wanyang'anywe, washtakiwe ikiwezekana na waambiwe wakajenge pale pale Mafurikoni Kwao Jangwani panawatosha sana tu.

Haya Avic Town (GSM Wadhamini wakuu wa Yanga SC) Kazi ndiyo Kwanza imeshaanza na taratibu Msukule wenu mliousajili unaanza Kuwaleteeni Nuksi huku Laana ya Kijana Mstaarabu mliomuacha Kiudhalilishaji Juzi kutokea Tanga ikianza Kuwatafuna.

Mkiambiwa nyie ni Matapeli hamtaki.
 
GSM wanahusishwa na mambo kibao ya kijanja janja, wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi wa kutosha na mamlaka ya nchi kujiridhisha kama kweli wanafuata sheria kwenye mambo yao ya biashara na umiliki wa mali.
 
Mimi sio Yanga lakiji ninachojua Alvic Town sio mali ya GSM bali wao wamekodi kuweka kambi. Ule ni mradi wa wachina kama nipo sahihi wamejenga nyumba na wanaziuza kwa wenye uwezo wao.
Alvic Town ndiyo nini? Tuanzie hapa Kwanza Ndugu.
 
Hilo eneo Yanga si walipewa na aliyekuwa mshauri mkuu wa simba ndugu BASHITE malyamungu?
Kama walipewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati huo Paul Makonda (mwana Simba SC) walishindwa Kuhoji au Kufuatilia uhalali wake hasa Kisheria na Kuuliza?

Na bahati nzuri aliyewapa Makonda alikuwa ni mwana Simba SC lia lia na huyu Mkuu wa Mkoa wa sasa wa Dar es Salaam Amos Makalla aliyeliibua hili leo pamoja na Wakazi wa Kigamboni nae ni mwana Simba SC tena Kindakindaki kabisa mwenye Kadi halali.

Si mnae Manara? Mwambieni awatetee.
 
Waambie GSM taratibu tu Amos Makalla (RC wa Dar) na mwana Simba SC Kindakindaki anawajaza tu kwenye Target ili awalime vizuri na wameshaingia hivi. Kudadadeki zenu!!
Tatizo umeha ushabiki mbele mpaka unarukwa na akili. Fanya utafiti kabla ya kuropoka. Avic Town si mali ya GSM. Pia usidhani kila anaecomment kukupinga ni mwanayanga
 
Ona hizi vinywaji

20210903_124751.jpg
 
Tatizo umeha ushabiki mbele mpaka unarukwa na akili. Fanya utafiti kabla ya kuropoka. Avic Town si mali ya GSM. Pia usidhani kila anaecomment kukupinga ni mwanayanga
Kutenganisha Avic Town na GSM ( Wadhamini wakuu wa Yanga SC ) ni sawa na Kumtenganisha Shetani ( Lucifa ) na Dhambi.

Na hivi RC Makalla ni Simba SC mtanyooshwa tu na katika hili anzeni kujiandaa nalo Kisaikolojia kwani limewakalia vibaya sana.
 
..Hebu wakumbushe hao mikia fc. Kutwa kucha wanawaza Yanga tuuu.. Kumbe mikono yao haiendi kinywani bila kuandika habari za TIMU YA WANANCHI eeh? Mtu mmoja majina kumi, ya nn yote hayo kama sio kutumika? Shubaaaaaamit
Waambieni GSM na Yanga SC waache Utapeli kwani huenda ndiyo maana Yanga SC hamfanikiwi Kimpira Uwanjani kwakuwa mna Laana za hao Wakazi 234 wa Kigamboni mliowadhulumu Ardhi yao.
 
hilo eneo ni kweli wananchi walidhulumiwa kwani liliuzwa na wananchi kuondolewa bila kupewa hakizao cha ajabu wizara na manispaa wamekuwa wakitupiana mzigo na Lukuvi amekuwa kimya muda mrefu si ajabu na yeye alipozwa kama eneo walilopewa yanga lina mgogoro ni wazi aliyewapa anahusika na utapeli na aliwapa ili kujificha chini ya mgongo wao ingawa nachojua yanga wanakodisha kwa ajili ya mazoezi na kambi
 
Kama walipewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati huo Paul Makonda ( mwana Simba SC ) walishindwa Kuhoji au Kufuatilia uhalali wake hasa Kisheria na Kuuliza?

Na bahati nzuri aliyewapa Makonda alikuwa ni mwana Simba SC lia lia na huyu Mkuu wa Mkoa wa sasa wa Dar es Salaam Amos Makalla aliyeliibua hili leo pamoja na Wakazi wa Kigamboni nae ni mwana Simba SC tena Kindakindaki kabisa mwenye Kadi halali.

Si mnae Manara? Mwambieni awatetee.
Mightier, Mo na Barbara mlikuwa mnamtesa Manara hadi akakonda, sasa hivi kila siku anaongezeka kilo 5. ha ha ha
 
Yaani hilo Makonda hakuliona aje alione Makalla na porojo zake kwa watu waliopangwa kuongea.

Asilete u Simba wake kwenye masuala ya kisheria. Anaweza kuwa RC atakaye kaa muda mfupi sana awamu ya Samia.
 
GSM wanahusishwa na mambo kibao ya kijanja janja, wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi wa kutosha na mamlaka ya nchi kujiridhisha kama kweli wanafuata sheria kwenye mambo yao ya biashara na umiliki wa mali.
Hawa jamaa; watu wengi walidhani kipindi cha Magufuli ndiyo ingekuwa arobaini yao lakini sijui waliponaje. Kwa kifupi ni watu wabaya sana sana na hata huko kwenye mpira wamekwenda kimkatiti tu. Siyo watu wazuri kabisa. Ila kama waliweza ku-survive wakati wa Magufuli kwa huyu mama ndiyo watatanuka na ku-terrorize wanavyopenda. Mtu asikudanganye hata huyu Mo aliyeko Simba ni mtu mzuri kama anavyojifanya. Mimi ndiyo maana ushabiki wa mpira wa hizi club nilishaupiga teke siku nyingi na sijishughulishi huko kabisa.
 
Yaani hilo Makonda hakuliona aje alione Makalla na porojo zake kwa watu waliopangwa kuongea.
Asilete u Simba wake kwenye masuala ya kisheria. Anaweza kuwa RC atakaye kaa muda mfupi sana awamu ya Samia.
Makonda naye utamhesabu kwenye viongozi? Yule alikuwa mpiga dili na mtu wa show off tu.
 
Back
Top Bottom