Ziara Rais Samia zinavyotumika kuhalalisha upigaji

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Asubuhi ya Leo majira ya saa 5 hivi nimepishana na msafara wa Rais ukitokea mkoa wa Rukwa kuelekea Songwe. Binafsi kama Mwandishi wa habari za mazingira naelekea mwambao wa ziwa Tanganyika kikazi. Nilipofika Namanyere wilaya ya Nkasi nimeachana na basi niliyokuja nayo toka Mbeya maana inaendelea na Safari Hadi Mpanda Katavi nami kikazi naelekea tarafa ya KIRANDO hivyo nalazimika kuchukua usafiri mwingine kuelekea huko.

Wakati nasubiri usafiri hapa stendi Kuu Namanyere nimekutana na Stori ya ajabu ambayo sijawahi kuisikia maeneo mengine. Vijana wa Bodaboda na wapiga Debe wanahadithiana Jambo ambalo limefanyika hapa jirani na Stendi usiku wa July 14 kuamkia July 15 siku ambayo Rais Samia alianza ziara Mkoani Rukwa akitokea Katavi.

Kwamba tarehe 14 Julai kwenye kiwanja cha Wazi karibu na Stendi kilifanyika Sherehe iliyobatizwa jina la Mkesha wa Mama ulioandaliwa na viongozi wa Wilaya hii wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya. Katika Mkesha huo wa nje watu walisafirishwa toka Kata zote, kulikuwa na vinywaji vikali na baridi vya kutosha, Muziki wa kukodi, nyama choma ya Mbuzi na Nyamapori na pia waalikwa toka mbali pamoja na Viongozi walilipwa posho na Wageni kulipwa malazi.
Labda wenzangu mnieleze faida ya Aina hii ya mikesha. Yaani Mh. Rais kalala Mpanda, halafu Wananchi wa mkoa mwingine wanakesha wakinywa na kucheza Kwa gharama za serikali? Mh Rais amefika Namanyere akazindua mradi mmoja tu wa Hospitali ya wilaya na akasalimia Wananchi Kwa Muda mfupi Sana. Wengi tuliona maana TBC ilikuwa live. Kwa shughuli hiyo ya nusu saa ya Mh Rais ndo watu wakeshe usiku kucha wakila na kunywa kumsubiri?

Mbona Jambo hili halijafanywa Sumbawanga ambako Rais amelala siku 3 July 15-18?
Hapa hela ya Watanzania imepigwa Kwa Kisingizio cha Mkesha wa kumsubiri Mama.

Hivi ni utamaduni wa kabila gani nchi hii ukisikia kesho mgeni anakuja kwako wewe unalala nje ukila na kulewa na mgeni Huyo kwako anapita tu hata maji hanywi, Maana Mh Rais hakula wala kunywa hapa Namanyere.

TAKUKURU tafadhali, haya ni matumizi mabaya ya fedha za Umma, tunataka kusikia kiasi kilichotumika na kilitoka fungu gani.

Mji hauna maji ya uhakika halafu viongozi wanachukua fedha za Umma kugharamia matukio ya kujineemesha? HAPANA.
 
Pesa ya Mwenge na ziara za maza watu hupiga pesa ndefu sababu hakuna cha CAG au TAKUKURU watasogea, mbaya zaidi na wao huwa wapo kwenye kain

Pesa ya Mwenge na ziara za maza watu hupiga pesa ndefu sababu hakuna cha CAG au TAKUKURU watasogea, mbaya zaidi na wao huwa wapo kwenye kamati
Nakubaliana na wewe maana Mambo ya ovyo kama haya TAKUKURU wilaya walitakiwa wayachujulie hatua mara moja. Lakini kama TAKUKURU wamekaa kimya je TISS wako wapi?
 
Asubuhi ya Leo majira ya saa 5 hivi nimepishana na msafara wa Rais ukitokea mkoa wa Rukwa kuelekea Songwe. Binafsi kama Mwandishi wa habari za mazingira naelekea mwambao wa ziwa Tanganyika kikazi. Nilipofika Namanyere wilaya ya Nkasi nimeachana na basi niliyokuja nayo toka Mbeya maana inaendelea na Safari Hadi Mpanda Katavi nami kikazi naelekea tarafa ya KIRANDO hivyo nalazimika kuchukua usafiri mwingine kuelekea huko.

Wakati nasubiri usafiri hapa stendi Kuu Namanyere nimekutana na Stori ya ajabu ambayo sijawahi kuisikia maeneo mengine. Vijana wa Bodaboda na wapiga Debe wanahadithiana Jambo ambalo limefanyika hapa jirani na Stendi usiku wa July 14 kuamkia July 15 siku ambayo Rais Samia alianza ziara Mkoani Rukwa akitokea Katavi.

Kwamba tarehe 14 Julai kwenye kiwanja cha Wazi karibu na Stendi kilifanyika Sherehe iliyobatizwa jina la Mkesha wa Mama ulioandaliwa na viongozi wa Wilaya hii wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya. Katika Mkesha huo wa nje watu walisafirishwa toka Kata zote, kulikuwa na vinywaji vikali na baridi vya kutosha, Muziki wa kukodi, nyama choma ya Mbuzi na Nyamapori na pia waalikwa toka mbali pamoja na Viongozi walilipwa posho na Wageni kulipwa malazi.
Labda wenzangu mnieleze faida ya Aina hii ya mikesha. Yaani Mh. Rais kalala Mpanda, halafu Wananchi wa mkoa mwingine wanakesha wakinywa na kucheza Kwa gharama za serikali? Mh Rais amefika Namanyere akazindua mradi mmoja tu wa Hospitali ya wilaya na akasalimia Wananchi Kwa Muda mfupi Sana. Wengi tuliona maana TBC ilikuwa live. Kwa shughuli hiyo ya nusu saa ya Mh Rais ndo watu wakeshe usiku kucha wakila na kunywa kumsubiri?

Mbona Jambo hili halijafanywa Sumbawanga ambako Rais amelala siku 3 July 15-18?
Hapa hela ya Watanzania imepigwa Kwa Kisingizio cha Mkesha wa kumsubiri Mama.

Hivi ni utamaduni wa kabila gani nchi hii ukisikia kesho mgeni anakuja kwako wewe unalala nje ukila na kulewa na mgeni Huyo kwako anapita tu hata maji hanywi, Maana Mh Rais hakula wala kunywa hapa Namanyere.

TAKUKURU tafadhali, haya ni matumizi mabaya ya fedha za Umma, tunataka kusikia kiasi kilichotumika na kilitoka fungu gani.

Mji hauna maji ya uhakika halafu viongozi wanachukua fedha za Umma kugharamia matukio ya kujineemesha? HAPANA.
Unauhakika kuwa ww ni mwandishi wa habar?
Acha kutungua story mm npo hapa hayo unayasema ni uongo mtupu

sema tu umeumizwa na nyomi la watu kwenye ziara ya Mh. Rais wetu mpendwa Dr Samia Suluhu Hassan
 
Wakuu ndo tumeshaamua kwenda na Samia mpaka 2030 nyie endeleeni kukesha humu mkiandika ma essay ya uongo mtakufa kwa pressure si mmeona lile nyomi, SAMIA tulimmis Sana wanakatavi tunampenda mno
 
wacha wajisevia na mwengine anakunya mezani
GSsKSbrWQAAO2Z1.jpg
 
Back
Top Bottom