Uchaguzi 2020 Ziara ya Dkt. Magufuli Kilimanjaro imebeba ajenda za msingi

Kwani hayo masale si yamebebwa na wanaccm? Nyie vipi?
 
Sina la kusema hapa. Ila kili people are smart.

Kama kweli wamemuamini tutarajie maajabu.

Ila pia hao watu wa Kilimanjaro Ni wagumu kukuamini mpaka uthibitisho wewe Ni Wa kuaminika. Sasa Kama Magu kafanya mambo ambayo wananchi( wa Kilimanjaro) wamuamini ) Basi atapata Kura zao.

Vinginevyo atarajie maumivu.
 
Ndio mnasema tuchague tuwapeni hadhi ya jiji? Its too late ingekuwa maendeleo hayana chama lingeshakuwa jiji long time.
 
Mabus yalibeba watu toka Arusha, Upareni na kwingineko. Moshi mjini biashara zilikuwa ninaendelea kama kawaida kama vile hakuna jambo. Lissu maduka yalifungwa na uwanja ilikuwa nyomi. Leo mabus lakini uwanja haukujaa na wengine walienda kuona wasanii. Kuna shemeji zangu walifuata watu Vijijini na Hiace.
 
moshi na arusha ni kona za chadema, skuamini mapokezi aliyopata, nadhan ataelekea na arusha pia
 

Tuna sifia kiasi na chumvi tunaweka. Cha ukweli ni kimoja tuu coffee tree labda kidogo shule ila zinaendeshwa na serikali, vingine sio kweli.
 

Moshi wanapewa gari moshi mwanza wanapewa reli ya umeme. Chato wamejengewa uwanja wa taifa wakati KIA ambayo inaleta watalii 99% na zaidi ya $2B kwa nchi uwanja haujafanyiwa matengenezo
 
Sale linatumika kuomba msamaha pale mkosaji akiwa na wasuluhishi anapoenda kwa mkosewaji na kupeana jani la sale kama ombi la msamaha, kwa hali ya jana wananchi hawakumaanisha msamaha kama huyo jamaa alivyodhani.bali kama ulivyosema sale pia humpokea mtu maarufu, ila zaidi hata ktk shughuli ya sherehe hutumika, na hata misiba.

Jee hivi sale likiwekwa kwenye gari ya maiti nayo ni kuomb msamaha au hyo maiti ni maarufu?
Hapana.
Naomba tafsiri alotoa jamaa ipingwe vikali na ni mara ya pili amerudia, mara ya kwanza alienda hai akasema hivyohivyo.
Kama anadhani wachaga walimkosea basi ndo maana aliwavunjia nyumba zao kimara kwenda mbezi.Huyu hafai kwani kwa kukosewa alilipiza kisasi.
 
Kila upande una lawama lakini CCM ilikua unafanya business as usual, ila upinzani ukazidi kuwa radical 2010 - 2015, kupinga kila kitu na ujuaji, kitu ambacho hawakutegemea ni CCM kuja na mtu kama Magufuli mkali asiyependa siasa zao na anawajua niwepesi mana amaekaa nao bungeni...

Uchaguzi ata uwe wa haki vp kama kuna toxic relationship ngumu kufanya maendeleo ya pamoja baina ya vyama (refer situation ya marekani ya Trump na siasa zao), solution wapinzani warudi kwenye basics wasupport pale wanapoona hakuna nia mbaya au wa compromise pale wanapoona kuna priority zao zimefikiwa kwa asilimia hata 50, hii pia itawajengea uaminifu kwa wapiga kura kwamba sio watu wakupinga tu ila wanapima na issue yenyewe, ila ili waweze kufanya hivyo nafikiri uongozi ndani ya vyama vyao lazima ubadilike mana mengi ya sasa wanatumwa tu wabunge hata kama hawaafiki, so wanahitaji kiongozi mwenye maono tofauti

Sent from my SM-J510L using JamiiForums mobile app
 

..uchaguzi wa 2015 ulikuwa toxic.

..na bahati mbaya, Jpm hana busara za ku-handle kilichotokea, na kurudisha maelewano na masikilizano ktk siasa zetu.

..tatizo lingine ni kwamba Jpm hapendi demokrasia ya vyama vingi, na ukikosolewa anajisikia kama ametukanwa.

..Jpm amefanya siasa ziwe kama vita kwa kuelekeza vyombo vya dola vipambane na wanasiasa wa vyama mbadala.
 
Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wanaona kabisa kuna vitu jiwe alivyofanya kachemka na vimewaumiza hata wao ila wakiangalia namna ya kumfikishia wanakumbuka ni aina ya watu wasioshaurika wala kupangiwa ! Hao nao wana jambo lao japo ni wanaccm wenzenu[emoji3]
 
Unaweza kuthibitisha huu uongo wako? Maana Ana Ngwhira alipewa ukoo wa mkoa wakati ni mpinzani. Vita iko wapi? NCCR Mageuzi na TLP wanafanya siasa safi.
Chadema mmezoea harakati badala ya siasa.
 
Unaweza kuthibitisha huu uongo wako? Maana Ana Ngwhira alipewa ukoo wa mkoa wakati ni mpinzani. Vita iko wapi? NCCR Mageuzi na TLP wanafanya siasa safi.
Chadema mmezoea harakati badala ya siasa.

..kufanya harakati ni uhaini nchi hii?

..Jpm hana busara, na anachukia demokrasia ya vyama vingi.

..kiongozi gani anapokea walawiti[babu seya,papii] watoto ikulu, badala ya kualika wanasiasa wenzake na kuzungumza nao?
 
..kufanya harakati ni uhaini nchi hii?

..Jpm hana busara, na anachukia demokrasia ya vyama vingi.

..kiongozi gani anapokea walawiti watoto ikulu, badala ya kuzungumza na wanasiasa wenzake.
Katiba ya JMT inampa malaka ya kusamehe wafungwa. Sasa kama walifungwa alafu wakajirekebisha kuna ubaya kuwapokea?
Uongee na Chadema ambao hata Covid 19 waliitumia kwa harakati za kisiasa badala ya kuungana na watanzania kupambana na hili janga.

Mbona Act,Cuf na Nccr Mageuzi waliitwa ikulu? Chadema haifai kabisa.
 

..wewe unaweza kualika walawiti watoto nyumbani kwako, au ofisini kwako?

..aliyetumia covid19 kisiasa ni Jpm mpaka kufikia kutoa maneno ya kufuru.

..cdm walichukua tahadhari zote ambazo wataalamu walielekeza zichukuliwe.

..nieleze cdm walifanya jambo gani ambalo lilikuwa limekatazwa na wataalamu wa afya kipindi kile cha tishio la covid19.

..mtu asiyefaa ni Jiwe, hapendi demokrasia ya vyama vingi, anataka kuturudisha kwenye mfumo wa chama kimoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…