Uchaguzi 2020 Ziara ya Dkt. Magufuli Kilimanjaro imebeba ajenda za msingi

We jamaa bana.. Moshi wanajielewa.. Yani mpaka umpigie mtu kura ndio akuletee maendeleo? maendeleo yanaletwa na kodi yako sio kura yako!
 
Yaani na akili zako zotee ndio umeandika huu UHARO hapa,kwanza nikuulize unaamini katika mfumo wa siasa za vyama vingi?kama kweli haya uyasemayo leo hii Marekani na nchi za Ulaya leo hii zingekuwa nyuma kimaendeleo umeeandika sana lakini ni ZERO nijuavyo mie na uelewa wangu mdogo ni kwamba bila vyama vingi kwa nchi haiwezi endelea hapa unaweza sema mbona China crazy.

Kama serikali na mgombea mwenye akili timamu baada ya uchaguzi anakuwa Rais wa wote huwezi lazimisha kila mtu kumpenda Pombe hata YESU KRISTO wapo watu leo hii hawakubaliana nae sembuse Pombe!Nijuavyo serikali ndio inakusanya kodi na kuwahudumia wananchi unaposemaa Moshi Kilimanjaro walikosea wamemkosea nani haswa, kwani wamemkosea nini huyo mtu?Hivi kodi za watu wa Moshi zaenda wapi au nani anazikusanya?This happening only in Tanzania watu wenye akili kutoka Mataifa mengine wakisoma huu ujumbe watadharau Watanzania wote kumbe sio wote wale wachumia Tumbo ndio wene kujitoa ufahamu.

Nikuulize swali moja Majimbo ya Mkoa wa Tanga yanaongozwa na Upinzani au yalishawahi kuongozwa na Upinzani ukiacha jimbo la Tanga mjini na je yana hali gaani waweza yafananisha na majimbo ya Vunjo na Rombo ambayo yako chini ya Upinzani hebu tuache kujitoa ufahamu.

Rais yoyote atakayechaguliwa anakuwa Rais wa Tanzania na anahudumia kila sehemu hata kama sehemu husika hawajampa kura hata moja lakini kwa kuwa ni Watanzania na walipa kodi lazima wapate huduma kupitia kodi zao.Pombe hajawahi na hatawahi kutoa pesa zake mfukoni ati ajenge kitu flani never pesa yote ni ya wavuja jasho full stop acheni ushamba wa ubaguzi wa kisiasa.

Kuhusu Dr Shaoo kuhudhuria amehudhuria kama kiongozi ambae sio mbaguzi kama Pombe alivyo kila anapoenda anatisha watu mara siwaletei maendeleo hivi yeye ndio anaatoa pesa yake mfukoni?Mlivyo wabaguzi Dr Shoo angeenda kwa mikutano ya Lissu usingeyasema haya kuwa ndio kukubalika kwa Lissu never sana sana ungeandika Dr Shoo kajihusisha na siasa mara ungesema Mkuu wa KKKT ajihusisha na siasa za upinzani.
 
Umeongea vizuri sana katika kuwaaminisha wakazi wa Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla kuwa kasi yao ya maendeleo imedumazwa na wao kuegemea zaidi upande wa wapinzani kuliko Chama Tawala. Umewahakikishia kuwa wakijirekebisha na kuchagua kukabidhili uongozi wa mkoa wao na nchi yao kwa Chama Tawala basi maendeleo makubwa kama mji wao mpendwa wa Moshi kupewa hadhi ya Jiji na jimbo la Vunjo kuwa kupewa Halmashauri yake yatapatikana. Ungekuwa umewafanyia jambo jema sana wananchi wa Kilimanjaro kama ungewaonyesha jinsi mikoa ya Ruvuma, Tabora na Dodoma ilivyopaa kimaendeleo baada ya kutokitosa Chama Tawala hata mara moja. Kwa kuendelea kuwalaumu wabunge waliopita kwa kujijengea makasri wakati walio wachagua wanaendelea kupiga miyao. Ingekuwa vyema kama ungeweka wazi majina ya wabunge hao na vyama vyao ambao walijenga hayo makasri baada ya kupata nafasi ya uongozi. Aidha, ungewahakikishia pia hao wananchi jinsi hali yao itakavyoboresha baada ya kuwa wanapata lifti kwenye hard top na V80 ya viongozi wao yakiwa full viyoyozi.

Amandla...
 
Hakika sisi tutamchagua Ndugu Magufuli awe tena Rais wa Jamhu ya Muungano wa Tanzania
 
Walifanya makosa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…