Ziara ya Katibu Mkuu Wa CCM na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa Mikoa Ya Geita, Kagera, Kigoma, Katavi na Tabora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA MIKOA YA GEITA, KAGERA, KIGOMA, KATAVI NA TABORA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo atakuwa na Ziara ya Kikazi Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Katavi na Tabora akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Ziara hiyo itaanza tarehe 13 - 24 Novemba, 2021 Mkoani Kagera katika Wilaya zote za Mkoa huo, na kuendelea katika Mikoa ya Geita, Kigoma, Katavi, na kuhitimisha mkoa wa Tabora.

Malengo ya ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama katika ngazi za Mashina pamoja na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025, ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa cha tarehe 29 Juni, 2021.

Wajumbe wa Sekretarieti watakaojumuika katika Ziara na Katibu Mkuu ni
  • Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara Ndg. Christina Mndeme,
  • Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka,
  • Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga,
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg. Kennan Kihongosi,
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Dkt. Philis Nyimbi na
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Ndg. Gilbert Kalima.


 
Safi sana, ni vizuri kupita na kujionea utekelezaji wa ilani CCM ili ahidi na inatenda.
 
Anapita kukagua uhai wa chama, lakini ikifika wakati wa uchaguzi vyombo vya dola na tume ya uchaguzi ndio vinageuka kuwa nguzo ya kutangazwa washindi!
Tatizo liko wapi nanyi hamshiriki tena maishani!
 
Jumuiya ya Wazazi ijitafakari kama inastahili kuendelea kuwepo au ifutwe.
 
Wakati wa Magufuli Nani aliekuwa na uwezo wa kusimama barabaran na kuizomea CCM hata wapinzani wenyew hawakua na hiyo confidence si kwasabab CCM ilikubarika kiasi icho ila pia mkono wa chuma pia ulitumika sana
 
Yaani huyu ndo hana mvuto kabisa! Kweli anaweza kuwa mtendaji mzuri ila naona katibu mkuu hapana! Ila ndo hivo mwisho wa chama umefika!
Mwisho wa kwenda wapi ?!!

CCM ipo kabla ya Samia na JPM na itakuwepo miaka mingi sana kutoka hapa......


Siempre CCM
 
Sababu hamna ajenda ya uchaguzi mtaeleza nini wananchi wawaelewe!
Muda wa siasa za kishenzi umepita dogo. Kama sisi hatuna hoja za kuwaambia hao wananchi, mbona wananchi wenyewe hawajitokezi tena kupiga kura?
 
Mkimaliza ziara hii, anzeni mikoa ya Singida, manyara, arusha, Kilimanjaro, na Tanga. Kuna miradi imepigwa
 
Kila lenye heri viongozi wetu,

Mungu atembee nanyi wakati wote I bless you
 
Yaani huyu ndo hana mvuto kabisa! Kweli anaweza kuwa mtendaji mzuri ila naona katibu mkuu hapana! Ila ndo hivo mwisho wa chama umefika!
Sure,Chongolo amepwaya sana.Bashiru alifiti sana ila aliharibu kuwadharau wazee na vyama pinzani.

Chongolo hana dharau ila hana mbinu zakujenga hoja watu wavutike nakushawishika.

Shaka humchukulia Chongolo kama mshikaji wake tu.Kabla ya Kinana kulikuwa na katibu mmoja anafanana na Chongolo kiutendaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…