Ziara ya Paul Makonda yaingia shubiri Bagamoyo na kuibua mapungufu ya Serikali ya CCM

19 January 2024

WAFANYAKAZI WA UVCCM WAPEWA MWEZI MMOJA KULIPA MADENI WALIYOKOPA BENKI YA DCB Commercial Bank Plc


Wafanyakazi hao 132 walikopa jumla ya shs. 600,000,000 .... mikopo hiyo ilichukuliwa miaka 10 iliyopita na mbali ya kufuatiliwa wameshindwa kujitokeza hivyo ndani ya mwezi mmoja majina yao yataanikwa hadharani baada ya njia za chini chini kutunza siri zao kushindikana mkurugenzi mtendaji wa DCB Commercial Bank Plc amewatahadhatisha makada wa UVCCM ...
 
Mbona wenye hati miliki wengi wameporwa Ardhi zao?
Hati miliki nchi hii hazina thamani
Siasa za CCM ndiyo hatamu

Makonda akiamua nyumba ya GSM iwe yake sawa
Wana CCM walivamia shamba la Mo sawa
Wakivamia Ardhi ya Twigs cement sawa
Wakivamia shamba la mstaafu wa CCM mwenzao kule Ndachi dodoma sawa
Yaani Nyani akimula Nyani mwenzake sawa
Kama Taifa tuna kazi kweli kweli kubadili mfumo tulio uachia ukaota mizizu
 
Makonda akiamua nyumba ya GSM iwe yake sawa
Wana CCM walivamia shamba la Mo sawa

Kwa kifupi CCM wameteka nyara mifumo yote yaani mfumo wa jinai haki ( criminal justice system), mfumo wa uchaguzi, mfumo wa demokrasia n.k n.k

Pia chini ya utawala wa chama hiki kongwe, wahalifu wanapewa vyeo ndani ya chama na katika vyombo vizito vya serikalini ...


CCM imeshindwa kubana matumizi makubwa ya anasa ya kuwagharamia viongozi ..... pesa hizo zingeweza kutumika kutoa huduma bora za kijamii kama afya, elimu, maji kwa wote ....

 
Na bado! CCM itakufa kifo kibaya
 
Mwembeni, Tanga

MAKONDA AWA MKALI WANANCHI KULAZIMISHWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

View: https://m.youtube.com/watch?v=IzRI8hWUql8
Mkurugenzi wilaya ya Pangani abanwa hakuna kituo cha afya miaka miwili .. zahanati ilijengwa chini ya viwango ikaanguka hivyo sasa juhudi zinafanyika ....

Paul Makonda ambana mkurugenzi ni sheria ipi inayotaka wananchi wachangie ujenzi wakati fedha za serikali tayari zimetolewa ...

Paul Makonda asema kodi inayokusanya ni hela ya wananchi hivyo kuwabana michango tena na halmashauri siyo sahihi kisheria na serikali tayari imetoa fedha nyingi ....
 
Makonda akutana na maswali magumu yaliyomtoa jasho kuhusu mfumo wa bima ya afya

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…