Tarehe 01 Agosti, 2024 rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani amesafiri kwa Treni ya kisasa ya SGR kutoka Darisama kuelekea Dodoma kwenye uzinduzi wa safari kutoka Dar Es Salaam kwenda Dodoma
Dhiara hiyo ya rais samia ilianza asubuhi ya tarehe 1 Agosti akitokea Ikulu ya magogoni na ujumbe mkubwa wa mawaziri, rais wa Zanzibar, marais wastaafu na wadau wengine wa septa ya usafiri na machawa akina baba Levo kuelekea Dodoma
Kutokana na mfululizo mrefu wa vingozi hao barabara ya Sokoine drive ilifungwa na askari wa barabarani (Traffic) kutoka saa moja asubuhi mpaka saa tano kuruhusu viongozi mbali mbali kufika stesheni ya Dar kwa ajili ya kusafiri na treni ya mwendokasi kuelekea Dodoma
Kitendo hicho kimesababisha biashara za kiuchumu kusimama jijini Dar kwa muda wote huo kutokana na foleni na barabara nyingi zinaongia mjini kufungwa
Mwananchi mmoja allyetokea Mbagala kuja maeneo ya Mnazi Mmoja Kitumbini kufuata mabero ya mitumba ili ende kuuza kwenye meza yake Mbagla alilalamika kuzuiwa kwa daladala kuingia katikati ya mji kwa ajili ya kupisha msafara wa rais na wapambe wake kupita njia ya sokoine drive kuja stesheni kupanda SGR
Mfanyabiashara huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa amelazimika kutembea kwa miguu kutoka Polisi Ufundi mpaka Mnazi Mmoja ili kununua mabero kwenda kuuza Mbagala
Alisema ameishiwa na mzigo leo alitoka asubuhi kuja mnazi mmoja kununua mabero ya nguo za mtumba lakini ameathiriwa na foleni kubwa mno na kuchelewa kufannya biashara yake kwa wakati
Pia wafanyakazi wengi wa Bandari wamelalamika kuchelewa kufika kazini kutokana na foleni kubwa nyakati za asubuhi na kulazika kutembea kwa miguu umbali mrefu mpaka kufika Kazini kwao Bandarini
Ikumbukwe kuwa uchumi wa nchi unategemea Bidhii zinazoshuka kutoka Bandari na TRA makusanyo yao makubwa ya kodi yanatoka Bandarini
Inasemekana na wataalam wa uchumi kuwa makusanyo ya kodi ya TRA asimia 70% yanatoka Bandari ya Darisalama
Mfanyabiashara mmoja wa Posta alisema kuwa kulikuwa na sababu gani rais kutokea Dar kwenda kuzindua SGR Dodoma na kwamba kwanini asingepanda ndege akaenda Dodoma kufanya uzinduzi huo?
Mfanyabiasha mwingine alisema kuwa anashangaa kuona uongozi umetokea Dar mji wa kibiashara wakati viongozi wote makazi yao ni Dodoma na kuhoji kuwa kwa nini wasingemaliza uzinduzi huo huko huko Dodoma mpaka waje Dar mji wa kibiashara kuathiri utendajikazi wa watu?
Comasava