Ziara ya Rais Samia Nchini DRC ni Utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo

Ziara ya Rais Samia Nchini DRC ni Utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Tumeona Mtanzania Brigedia Jenerali Juma Nkangaa akiidhinishwa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kama Mkurugenzi. Hatua hii inatokana na juhudi za serikali ya Rais Samia kuendelea kushirikiana na mataifa mengine kikamilifu katika nyanja zote muhimu.

Licha ya mikutano ya SADC, ziara ya Rais Samia nchini DRC ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania na wawekezaji mbalimbali wenye nia ya kuchangamkia fursa zilizopo katika nchi mwanachama mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwenye idadi ya watu zaidi ya Milioni 90.

Sanjari na fursa za kibiashara nchini DRC, Nchi hii pia inategemea miundombinu kama Bandari ya Dar na wanunuzi wakubwa wa bidhaa za kilimo kutoka. Kwa juhudi zinazoendelea kuimarisha sekta ya Kilimo ni wakati sahihi kwa kuendelea kuimarisha masoko yake ya nje.

Rais Samia Suluhu anatekeleza sera ya mambo ya nje ya nchi inayochagiza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo, shime watanzania wote tuendelee kumuunga mkono katika kazi zake hizi zenye tija kwa kila mmoja wetu.
 
Safi sana na kongole kwake mh. Rais wetu. Congo ni FURSA mpya na muhimu kwenye ukanda huu.
 
Hii ni fursa watanzania hatutakiwi kuiacha iende
 
Kuna mambo ya sgr na Atcl 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220817-212320.png
    Screenshot_20220817-212320.png
    121.5 KB · Views: 4
Safi sana na kongole kwake mh. Rais wetu. Congo ni FURSA mpya na muhimu kwenye ukanda huu.
Rais Samia kila akitoka nje ya nchi jua ameenda kutafuta fursa hakuna sehemu anayoenda kusiwe na fursa we are so proup of her
 
Hizo zinazoitwa fursa si kwa wananchi wa kada ya chini.
 
Hizo zinazoitwa fursa si kwa wananchi wa kada ya chini.
Hakuna kitu maisha haya kipo kwa ajili ya mwananchi wa kada ya chini, wanafikiwa kwa kuwa sehemu ya uzalishaji wa biashara za matajiri.

Ni mentality za kijamaa kuamini kuwa serikali inao uwezo wa kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kada ya watu wa chini siku zote, kitu hicho hakipo.
 
Back
Top Bottom