Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

hizo ndio enzi tunazo zitaka sasa... ....mae mambo za kubanwabanwa kwishney mwananchi anufaike sio sirikale inufaike afu mwananchi abaki hoiii
 
Mama Samia anafungua Nchi kitu ambacho ni kizuri Watu wenye mawazo ya Ujamaa jinyongeni
Sukuma GANG hao , wameamua kumvuruga Mama mitaoni ili waonekane wananguvu. Tisha toto tu hiyo ya kisukuma ni yakishamba sana.
 
Mkuu ninakiunga mkono asilimia 200. Wakenya hawajawahi kutupenda watanzania na wanasema waziwazi. Tanzania ni dumping place ya Kenya
Tena mbaya zaidi bidhaa unayouzwa Tanzania hiyo hiyo ubora wake ni tofauti na inayopelekwa nchi nyinginezo. Huo mkataba wa gas ni mbovu kabisa. Yaani Tanzania bado watu wanapikia kuni halafu unapeleka gas kwa jirani? Viwanda vyetu umeme unaumiza. Gas majumbani hakuna wengi wanaomudu maana ni gharama kubwa. Huyo Economi Advisor aliyeteua ninaomba atizame upya.

Critical Economic analysis was very much needed ahead of the contract signing. Wakenya wanatembelea brains zao at 200% na sisi 50%. Tujipime.
 
Kwani kipindi cha "mwenda zake" kuna viwanda gani vilivyo jengwa ? Suala la viwanda Tz lishatushinda
 
Ama nchi hata Burundi utapokelewa.
 
Punguza chuki mkuu, usije ukapata presure au ugonjwa wa moyo bure!!!
haya maisha ni mapito tu.

Pia kumbuka kuwa binaadamu wote ni sawa tu mbele za Mungu hivyo hatuna sababu ya kuchukiana au kudharauliana.
Hao wasikupe presha jamaa yao kafa na ulaji umeisha sasa hasira zote wanamuangushia Rais wa sasa Samia
 
Mama endelea hivyo hivyo, ambao hamjawahi kufanya biashara,Hamuwezi kujua umuhimu wa nchi ya Kenya kwa Tanzania na Tanzania kwa Kenya.Mfano huko shinyanga Mnada wa Mhunze (upo Wilaya ya Kishapu).Wafanya biashara walikuwa wakinunua mbuzi na kupeleka Kenya.Bei ya mbuzi ilikuwa sawa na bei ya mbuzi katika mnada Pugu Dar.Sometime kule Mhunze mbuzi alikuwa ni bei gari kuliko Pugu.Lkn toka tuvunje uhusiano wa kibiashara na Kenya.Na kuwazuia wakenya kuja nchini.Bei ya mbuzi imepolomoka katika huo mnada,kiasi kwamba hakuna hata wanunuaji mpaka mbuzi anauzwa Tsh 20,000/=
 
Hivi gas ya Mtwara inaenda wapi vile?
Umeme wa Stiglers ni mwingi sanaaa!
TUSIOGOPE! Tukiona Kenya wanatuzingua tutawazingua. Tuanze tuone hayo msemayo kwani sio Biblia au Quran!
 

Kwani kunufaika Wakenya ni dhambi. Wakenya wamekuwa ni waarabu Kama wazanzibari ? Mbona miroho yenu ni ya korosho hivi. Ule uafrika wenu umeyayuka
 
Kama tutawauzia wakenya gas kwa bei nafuu inamaana sisi tutauziana kwa bei nafuu zaidi,, ushindani wetu utabaki kwenye kuchapa kazi.

Kuhusu biashara ya ndege hatuwezi kuwa competent kwa kuwazuia Kenya airways bali tuboreshe huduma zetu kwa weledi na ubunifu tutafanya biashara nzuri.

Lakini mwisho wako nimegundua unaembrace kujifungia na kujifanya kisiwa. Unapenda kiongozi aliye sumu- identiy yako inajidhihilisha.

Hii hutokana na mlezi , kuna mliokulia mijeledi hamuoni kama kuna maisha bila kuchalazwa bakora.
 
Huo sio udhaifu hiyo ni complementarity hakuna faida ya kufanya kazi kwa kujifungia
 
Mama hatoki zero zero wewe,mpaka sasa ameiletea nchi manufaa makubwa sana kwa kukutana na rais wa kenya
 
Hakuna mantiki yeyote zaidi ya kuendeleza zile siasa za mwalimu kwamba madini hayaozi tuyaache mpaka watanzania watakapopata akili. Tutachelewa ndugu zangu.
Umesoma.lakini au ndo umeamia kushupaa tuuuu relax tumeshazoea kupigwa kila.mara
 
Baada ya kuyumbishwa na "hangover" ya madaraka itokanayo na POMBE kupitia mazungumzo muhimu ya pande hizi mbili, hapa sasa ndiyo kutakuwa na SULUHU pamoja na UHURU wa kufanya biashara kati ya nchi hizi mbili jirani.
 
Pumba tupu. Hiyo gesi mmekaa nayo miaka yote mmefanyia nini zaidi ya ufisadi tu. Kenya tutawauzia gesi hatuwapi bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…