Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Baada ya kuyumbishwa na "hangover" ya madaraka itokanayo na POMBE kupitia mazungumzo muhimu ya pande hizi mbili, hapa sasa ndiyo kutakuwa na SULUHU pamoja na UHURU wa kufanya biashara kati ya nchi hizi mbili jirani.
Amiiin
 
Mkuu ukiangazia Masuala ya Maslahi ya ki-nchi hatutanufaika kwa kusifiwa kuwa na roho zuri, hakuna tuzo za hivyo.
Acheni Roho mbaya. Watanzania wamekuwa na hii gesi miaka mingapi.? Zaidi ya kujinufaisha nyie mafisadi watanzania wamepata nini? Kenya tutawauzia tuingize kipato hatuwapi bure
 
Mwanamke huongozwa na mwanaume! Eti leo hi mwanamke anaongoza wanaume zaidi ya milion, kadili muda unavyozidi kwenda tutegemee kufeli zaidi.
Ukiwa hivi hata nyumbani utaishia style moja ya kifo cha mende, kisa mwanamke hatakiwa kuwa juu. Change your attitude mkuu!!
 
Kinachonishangaza Zanzibar waliondoa maswala ya gesi na mafuta kuwa siyo vitu vya muungano lakini leo hii mzanzibar anaenda kusaini mkataba wa gesi ya Tanganyika hii siyo halali
Kwa hiyo Samia ni Rais wa Zanzibar sio?
 
Benki ipi hiyo CRDB?Twendeni Kenya tukawekeze tuache kulia lia,atakaye tajirika wacha atajarike atakayekuwa maskini shauri yake,kazi iendelee
 
Three learning domain,Cognitive,Phsychomoter na ....malizia kama kweli wewe ni mtu wa Education🤣🤣🤣🤣
 
Asante mkuu. Watu wasio na hoja hukimbilia ku-attack mtu hana jipya huyo.
 
Roho ya kichoyoo na kibinafsi ndio ililifanya taifa hili kua maskini tangu uhuru hadi sasa,hata watoto wa Nyerere wapo wanavyoishi kwa matokeo ya roho ya baba yao.....unajua maana ya free market economy?
 
Tukisema Magufuli alikuwa anajua sana kuangalia interests za nchi, na alikuwa hamuonei mtu haya kumwabia papo kwa hapo usoni kuwa hataki upuuzi. Kenya walipojifanya kuzuia ndege kutoka Tanzania kwa sababu ya eti ya korona, yeye akafuta leseni nzima ya KQ kuingia Tanzania, hadi wakanyooka. Hili la kushirikiana safari za anga baina KQ na mashirika ya ndege ya Tanzania ni diplomacy za kipuuzi sana; time will tell. ATCL tulishafanya majaribio ya kushrikiana na mashirka ya nje tukaishia zero. Sasa hivi ndiyo tunaanza tu, halafu tunaelekea kurudoi kule kule.

Wakati mwingine hayo ni matokeo ya kutokuwa na self confidence na kudhani kuwa wengine ndio wanaoweza kutusaidia. Magufuli alikuwa na ile selfu oc=confidence ya kusema hadharani kuwa "tunaweza tena kwa fedha zetu wenyewe!".

Issue ya kuuza gesi Kenya sina tatizo nalo, ila tu ni kwamba iuzwe kwa faida, siyo kuuzwa kama free sample halafu wao watengeneze opportunities zaidi. Gharama ya gesi na gharama ya bomba ipangwe kimkakati.
 
Kenya wahuni tu sana! Mama wa wetu wamemrubuni anafanya mambo kwa maslahi ya taifa letu!Ila bungeni ikijadiliwa hii Kuna sehemu tutawabana hawa wahuni!
 
Elimu haina mwisho! Ni vizuri ukajiendeleza kielimu sio kwa kurudi shule bali kujiendeleza kupitia majalida mbalimbali yahusiyo uchumi na biashara!
 
Sioni sababu ya kuzua gesi isiuzwe eti kwa ajili ya kulinda viwanda hii roho mbaya
Tena na viwanda vyenyewe hatuna,zaidi ya kuzinfua mashine za kusaga na kukoboa mpunga.
 
Unayo draft nzima ya hiyo strategic alliance ama unatumia speculations tu?

Kampuni iliingiza hasara kubwa kipindi cha JPM (Na usiseme kuna investment imefanyika coz ndege zinakodiwa) but still haikua profitable enough.

Anakuja Mama kujaribu kutafuta namna ya ku offset hasara mnaanza kumlinganisha na JPM. Hivi JPM kafanikiwa nini kwenye aviation industry zaidi ya kununua ndege ambazo hazikuleta faida?
 
Tujifunze kuishi vizuri na majirani. Dunia ni kijiji sasa. Ni vema kuimarisha diplomasia ya uchumi kuliko kutunishiana misuri. Tuunge mkono Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mhe. Uhuru Kenyatta kuongoza vema nchi zetu mbili.
 
Kwanini msisubiri muwe na taarifa rasmi kuliko kupotosha watu? Ni lini umeambiwa gesi itafika huko kabla ya Tanzania kupata? Kuna futi za ujazo zaidi ya trillion 50 unadhani hakuna surplus ya kuuzwa nje?

By the way hilo bomba tutawapa gesi bure au wananunua? Urusi pamoja ma kuwa na vita ya kiuchumi na EU bado wanawauzia gesi? Maana kuna faida inaingia kwao hafanyi bure pale.

Dunia inaelekea kwenye economic intergration na Common market kupitia regional integration na digital markets ila sisi tunawaza mambo ya kuisolate kiuchumi eti kuogopa ushindani!?

JPM alituharibu sana akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…