Ziara ya Rais Samia nchini Marekani, wapinzani wakichezesha vizuri karata zao za diplomasia itasaidia sana kurejesha Demokrasia

Kwa tqarifa yako wewe huwezi kumuamulia mpinzani wako atumie utaratibu gani kudai haki yake. Tangu lini wakwa ndugu zenu?
Always nasema siasa ikichukuliwa kishabiki Kama Simba au yanga NI vigumu Sana kufikiri katika logic. Logic hapa ama NI kutafuta suluhu au kuionesha dunia pamoja na yote mnayopitia bado mnania ya kutafuta suluhu kwa njia ya diplomasia.
 
Mkuu unahangaika na Mushumbushi !
 
Democrasia gani mnayoitaka zaidi ya ile ya Mdude kusema atamnyoa mama yetu kama alivyo mnyoa JPM na hadi Leo yupo uraiani anadunda
 
Democrasia gani mnayoitaka zaidi ya ile ya Mdude kusema atamnyoa mama yetu kama alivyo mnyoa JPM na hadi Leo yupo uraiani anadunda
Kwani kunyoa NI tusi. Au ulitaka atekwe au apewe kesi nyingine ya uhujumu uchumi?
 
Mimi na swali ziara za mama zote huwa tunaona mpaka anapanda ndege ila hii ya USA hakuna hata picha moja kumuona Mama anaaga kama mazoea au kachukuwa airbus hataki watu wapige kelele. Mimi sina shida na safari Rais ni jukumu lake kwenda kuhudhuria mikutano ya kimataifa wala sio issue kuna watu wanataka kufananisha na JPM mbona alikuwa hasafiri hapo sio sawa hata JPM alisemwa kwanini asafiri. Kusafiri ni hobby kuna watu wanapenda safari na kuna watu hawapendi kawaida sana shida kwanini leo hii mama anaenda ziara kubwa kama hii USA hakuna hata picha moja akipanda ndege wanaficha nini? Nahisi kabeba Airbus litaenda ku pack kule na kulipa ground charges, na sijui kaondoka na ujumbe gani ziara utasema mtu kafumaniwa kimya kimyaa bila mbwembwe za picha za Mama yetu.
 
Ana mengi ya kuhutubia na hasa kuhusu Ugaidi wa Tanzania.
 
Naona umeandika jambo usilolijua, haujui Rais amekwenda wapi! Kabla ya kuandika ni bora ungewauliza jirani zako mama kaenda wapi.
 
Ana mengi ya kuhutubia na hasa kuhusu Ugaidi wa Tanzania.
Unajuwa wa Tanzania tulivyo, ukisema urudi Bongo kutembea ukifika tu utasikia wanakuja unajuwa mwanangu anaidaiwa ada ya shule, unajuwa mtaji tu, unajuwa kodi inaisha unajuwa nataka kuowa, unajuwa na bawasir muhimu wakamue unajiuliza ina maana nisingekuja ada angelipa nani? Na sisi kama nchi kwa level nyingine unajuwa Covid imeharibu sana, unajuwa ugaidi unaanza please misaada tupambane lakini nafsi zote tunajuwa hayo wala sio muhimu kichaka cha kupiga pesa za misaada.
 
Nyie jamaa zetu, mnataka nini? Mangi wenu yuko mqhakamani na analetwa na kesi inaendelea na mnaingia na makamera hadi kizimbani, jamaa yenu hata pingu hafungwi mnataka demokrasia gani? Ndio maana napendaga utawala wa talebani unakula shaba watu wanaendelea na mambo mengine
 
Huyo jamaa yenu aliyeko huko Belgium kwa watalebani wengine si angeenda kutoa salamu US. Yupo tu anatafuna mbawa za kuku tu ,kiongozi makini kabisa mkimbizi wa chama cha upinzani.
Nazani muda walikuwa nao na wamefanya lililowezekana Ila Kama walilala basi
 
Kwa machadema demokrasia ni uhuru wa kufisidi nchi. Uhuru wa mtu kuuza na kununua haki ndio demokrasia yao.
 
Kwa machadema demokrasia ni uhuru wa kufisidi nchi. Uhuru wa mtu kuuza na kununua haki ndio demokrasia yao.
Changia hoja kwa msingi wa hoja zenye tija na mifano hai sio kishabiki. Maoni mazuri NI muhimu kwenye kujenga taifa Bora na chuki hazijengi
 
Pingu IPO kumzuia mtuhumiwa asitoroke sio kumuadhibu mtuhumiwa. Sasa Kama mazingira NI salama Pingu za Nini Sasa.
 
Kabla hata hawajakutana, na nchi ikiwa kwenye taharuki kubwa kutokana na kifo cha Rais akiwa madarakani kwa mara ya kwanza ndani ya nchi hii, wapinzani hao wakaanza movement ya katiba nchi nzima!!!! Yaani hata 40 ilikuwa haijapita, at that time hata Samia mwenyewe alikuwa yupo kwenye taharuki! Mlishindwa nini kusubiri ule upepo wa msiba uishe ndipo muanze moves zenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…