Ziara ya Rais Samia Qatar inavyozidi kuleta neema kwenye sekta ya mifugo.

Ziara ya Rais Samia Qatar inavyozidi kuleta neema kwenye sekta ya mifugo.

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
413
Reaction score
471
Ziara ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya Oktoba, mwaka jana nchini Qatar, imeendelea kuvuta wawekezaii kutaka kuwekeza kwenye sekta; ya mifugo nchini.

Katika kikao kati ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Widam Food, Al Noubay Al Marri, wa Qatar kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe jijini Dodoma Mkurugenzi huyo alisema uamuzi wa kutaka kuwekeza hapa nchini ulipata msukumo kufuatia ziara ya Rais Samia aliyoifanya nchini Oatar:

Alisema lengo la ziara yake ni kukamilisha hatua za kuanzisha kampuni ya Widam Food nchini ambayo inashughulika na biashara ya nyama.

"Tunamshukuru Rais Samia kwa kutufungulia milango ya uwekezaii hapa Tanzania na sisi tunaona nyama ya Tanzania ina mustakabali mzuri kibiashara nchini Qatar," alisema Al Noubay.

Waziri Ulega alisema serikali imedhamiria kuboresha uzalishaji wa sekta ya mifugo, hivyo ujio wa mkurugenzi huyo unaunga mkono jitihada za serikali.

"Sisi tunawakaribisha hapa Tanzania, Rais Samia ameshafungua njia. Kilichobaki ni sisi kuwawezesha ninyi ili uwekezaji wenu ufanikiwe,"alisema Ulega.
 
Back
Top Bottom