beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Utiaji Saini wa Mikataba na Makubaliano hiyo unalenga kuendeleza Uhusiano kati ya Mataifa hayo mawili. Miongoni mwa Makubaliano hayo ni Mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wa Euro Milioni 178 kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi wa barabara wa mabasi yaendayo haraka
Vilevile, Tanzania na Ufaransa zimesaini Mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wa Euro Milioni 80 kuimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Nchi hizo pia zimesaini tamko la dhamira ya kushirikiana katika Uchumi wa Buluu na Usalama wa Bahari
========
Serikali za Tanzania na Ufaransa leo zimetia saini jumla ya mikataba sita ya makubaliano kwa nia ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba na Mhe. Franck Reister, Waziri wa Biashara wa Ufaransa wametia saini baadhi ya mikataba na makubaliano wakishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa makubaliano hayo ni mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 178 kwa ajili ya kugharamia mradi wa ujenzi wa barabara wa mabasi yaendayo haraka.
Serikali hizo pia zimesaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 80 ili kuimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kufikia malengo ya kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa sekta ya kilimo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametia saini mikataba mengine ya ushirikiano kwa niaba ya serikali.
Pia serikali za Tanzania na Ufaransa zimesaini tamko la dhamira ya kushirikiana katika eneo la uchumi wa buluu na usalama wa bahari.
Wakati huo huo, Rais Samia ameyasihi mataifa yote kuheshimu makubaliano na maazimio waliyotia saini, kama wajibu wa kuchukua hatua madhubuti katika kulinda bahari.
Rais Samia aliyasema hayo wakati wa kuhutubia mkutano wa siku tatu ujulikanao kama 'One Ocean Summit' mjini Brest, Ufaransa, ulioandaliwa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Pia, Soma=> Orodha ya mikopo iliyokopwa awamu ya sita tangu Rais Samia Suluhu aingie madarakani March 19, 2021