Ziara ya Rais Traole wa Burkina Faso italeta kichocheo kwa Watanzania cha kuchukia utawala wa kifisadi unaogawa rasilimali za Taifa kwa wageni?

Ziara ya Rais Traole wa Burkina Faso italeta kichocheo kwa Watanzania cha kuchukia utawala wa kifisadi unaogawa rasilimali za Taifa kwa wageni?

View attachment 3212449

Kuna watu maarufu ambao wamewahi kutembelea Tanzania, na kwa namna moja au nyingine kuwa chachu ya mwamko wa kisiasa nchini. Tumetembelewa na watu kama Fidel Castro, Che Guevara, Nelson Mandela, nk. Hata kama hawakuongea mengi wakiwa nchini, kuwapo kwao nchini kulileta hamasa na mwamko fulani ndani ya mioyo ya Watanzania juu ya kuwa na utawala wa haki na kuchukia utawala wa kifisadi usiojali kupoteza rasilimali za taifa na kuiweka nchi katika ukoloni mamboleo, mambo waliyoyapinga vikali.

Tanzania kwa sasa inazidi kuwa kinara wa utawala wa kifisadi unaokumbatia wageni na kuwajali zaidi ya wananchi katika nchi yao wenyewe. Sasa je, ziara ya Captain Ibrahimu Traole hapa Tanzania, italeta mwamko na msisimko wa kukataa utawala wa namna hiyo kwa Watanzania, kutia ndani na ndugu zetu wa JWTZ?
Hii michadema Kila wakati inawaza michuki tu😬😬😬
Ndo maana Mungu anawaadhibu hawafanikiwa kwa lolote........Sasa wamepoteza 42% basi inatafuta kwa kutolewa stress.
 
Mbona mkutano wa Brics south Africa alienda na hata juzi kati kuapishwa rais wa Ghana alikua huko
Huko Ghana alienda dk za mwisho na hata kukawa na taarifa kwamba asingehudhuria,na bado anapanda na mabastola jukwaani
 
Hii michadema Kila wakati inawaza michuki tu😬😬😬
Ndo maana Mungu anawaadhibu hawafanikiwa kwa lolote........Sasa wamepoteza 42% basi inatafuta kwa kutolewa stress.
Huelewi maana ya impact leaders huwezi kuelewa, wewe nenda kashangilie watu wako ndilo unaloweza
 
Nyuzi zako nyingi pamoja na comments umekuwa ukisisitiza kwamba hakuna UCHAWI. Au mimi ndio huwa sielewi?
Hakuna uchawi, uchawi ni imani kuhusu kitu ambacho hakipo.

Kama vile inavyowezekana ikawa hakuna Mungu, lakini kuna waamini wa Mungu wenye imani ya kuwapo Mungu, vivyo hivyo, hakuna uchawi, ila kuna wachawi wanaoamini uchawi, uchawi ambao haupo.

Umeshanielewa?
 
Back
Top Bottom