Ziara ya Samia nchini Urusi inakwenda kutukosesha fursa nyingi za maendeleo kutoka nchi za Magharibi

Watoto wetu wengi wanasoma US na nchi za EU wachache sana wako Urusi, scholarships nyingi, research nyingi tunafanya na vyuo vya US na EU, biashara nyingi na investment kubwa, pesa nyingi tumewekeza Ulaya.
ukifika Urusi unadanganywa unaingizwa kwenye vita
 
Ondoa mawazo ya kusaidiwa , dunia imebadilika sana. Kwa sasa hata USAID haipo lakini wewe bado unawaza misaada tu.
Nazungumzia biashara tunazofanya na nchi tajwa misaada nakuja baada ya mahusiano mazuri ya kibiashara, jikite hapo.
 
Ile siyo friend visit ni business visit.

Ndio maana nimeuliza tangu miaka ile ya 70 na 80 ni kipi kwa miaka ya hivi karibuni alichotusaidia.

Ujue Rais wetu amealikwa, ndio sababu nikaita friendly visit!
Lakini pia; Urusi na China ndio Nchi pekee zenye nguvu unaweza kusema ni rafiki wa kweli wa Tanzania; hawa wengine wote waliosalia ni rafiki wa kimaslahi.

Sasa huwezi kusubiri wakoloni wakupangie lini uweze kuwasiliana au kutembelea rafiki yako.
Narudia tena; Tulifaidika sana na ma engineer na madactari bingwa waliosoma Urusi. Natamani mama aombe tena hizo fursa za scholarship kwani uwekezaji kwenye Elimu hasa ya Sayansi ni muhimu kuliko kitu chochote na ndio umefikisha China hapo ilipo!
 
Mnahangaika mpk mnasahau jana mlisema nini.
Kila siku mnahubiri US na EU wawepanga kukata mahusiano nasi kwa sababu ya Oct 29. Leo mnasema ziara ya Urusi ndio itakayosababisha tukatiwe. Tushike lepi sasa! Au la Oct 29 halina nguvu tena na sasa issue ni ziara ya Russia?
 
Nazungumzia biashara tunazofanya na nchi tajwa misaada nakuja baada ya mahusiano mazuri ya kibiashara, jikite hapo.
Mbona hueleweki, simamia hoja moja.
Kama ni biashara jikite humo. Kama unataka misaada pia jikite humo.
 
Kwahiyo Samia kapangiwa na Urusi aende, mbona unaji contradict.
 
Hawa watz wenzetu hawapo objective ndio maana wanaruka ruka kama popcorn
 
Nani anahangaika anayeenda kuombaomba au mimi ninayeandika nikiwa nimelala kwenye kochi.
 
Ahsante sana mkuu kwa maelezo mafupi yenye kueleweka kwa waelewa.

Ukweli ni kwamba mada nyingi zinazoanzishwa humu ni za wapinzani wa Samia kama Samia (nawaita haters). Na bahati mbaya ni kuwa wengi wao wanakurupuka tu kutoa 'matamanio' yao na si uelewa Wala kuelezea uhalisia uliopo.....wachache wanaoujua ukweli, wanalazimika kudanganya kwa lengo tu la kutimiza takwa lao kuu la kuleta hofu na kudororesha Imani kwake. Kwao wao, Samia kaamka tu asubuhi na kujipangia safari ya Russia. Kwao wao, Samia kavunja mawasiliaho yoooote na nchi za ulaya na marekani (kichekesho). Kwao wao, Samia na serikali yake yooote hawajui kitu kuwazidi wao haters na chadema yao🤣🤣🤣🤣

Jibu la mjinga ni kumkalia kimya. Naunga sana mkono hii style ya hii mama anayeendelea nayo Sasa hivi ya kuwakalia kimya. The saying goes, "don't argue with fools, they will drag you down to their level and beat you with experience".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…