Ziara za Chalamila akiongozana na watumishi wa umma, tena usiku wa manane, zina muongozo upi wa sheria? Hasa kwa wenye watoto na ndoa?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nimeona Mkuu wa Mkoa amezindua ziara za usiku mzima, tena akiwa na watumishi wa umma wa kike na kiume.

Ninachofahamu, muda wa mtumishi wa umma kuwa ofisini mwisho saa tisa na nusu. Sasa sijafahamu kuhusu huu utumishi wa mpaka usiku wa manane.

Kwanza, hao watumishi wanatakiwa kuwa kazini saa moja na nusu asubuhi, kulikoni uwalaze saa kumi na moja alfajiri? Kwa kanuni ipi ya utumishi wa umma?

Je walioolewa, na waume zao wanawasubiri, ndoa zitakuwa salama? Je si kuhatarisha na kuyumbisha taasisi muhimu ya ndoa na hata maisha ya wanandoa hao, hasa wa jinsia ya kike, kwamba kuna namna tu imetafutwa, lakini lengo sio ziara ila ni kupakua asali?

Asubuhi watu hao wataweza kufika maofisini? Usingizi?

Ziara hizo zilipata clearance za ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma? May be the RC is over ambitious!

Kwamba anataka maafisa ardhi, TRA na wengine wakae maofisini usiku kucha, at this digital age. Nadhani angefanya consultation, kabla hajaingia kwenye mivutano, na kuwapa hoja wapinzani.

Let him reform the system first, tena kwa kutungiwa sheria, ili jambo hili lisiende kwa personal whims, and, he should sweep all the panya road wanaozurura usiku ili watumishi wawe salama.

Otherwise, uchumi wa masaa 24 unawavuta watu, sio watu wauvute. Yaani, mazingira yatawavuta watu wakae mpaka pakuche
 
Nimeona Mkuu wa Mkoa amezindua ziara za usiku mzima, tena akiwa na watumishi wa I'mma wa kike na kiume.

Ninachofahamu, muda wa mtumishi wa umma kuwa ofisini mwisho saa tisa na nusu. Sasa sijafahamu kuhusu huu utumishi wa mpaka usiku wa manane...

Utumishi wa umma ni 24/7 na hakuna kulala…. Kuna kupumzika kwa zamu tu

Tuache ulalamishi hata kwenye basic stuff
 
Ninachofahamu, muda wa mtumishi wa umma kuwa ofisini mwisho saa tisa na nusu. Sasa sijafahamu kuhusu huu utumishi wa mpaka usiku wa manane.
Kwa hiyo jambo likitokea zaidi ya saa tisa na nusu, serikali haihusiki???. Ndo point yako kuu!!!! 🤒🤒🤒
 
Exceptional cases. Nenda kasome Kanuni na sheria za Utumishi wa umma
Sheria zimewekwa ili zifuatwe, ila kuna mda mwingine sheria hupindishwa kwa Maslahi ya wananchi.. ✍️ ✍️.

Kwa hiyo hizo kanuni na sheria hazina Athari katika utendaji kazi... Ni jamii ya wavivu tu ndo huwa wanahisi wanaonewa..
 
Tunatakiwa kupumzika sio kulala Kama wote tukilala nchi itauzwa asubuhi na mamepa kabla hatujaamka,!!
 
Nimeona Mkuu wa Mkoa amezindua ziara za usiku mzima, tena akiwa na watumishi wa umma wa kike na kiume.

Ninachofahamu, muda wa mtumishi wa umma kuwa ofisini mwisho saa tisa na nusu. Sasa sijafahamu kuhusu huu utumishi wa mpaka usiku wa manane.

Kwanza, hao watumishi wanatakiwa kuwa kazini saa moja na nusu asubuhi, kulikoni uwalaze saa kumi na moja alfajiri? Kwa kanuni ipi ya utumishi wa umma?

Je walioolewa, na waume zao wanawasubiri, ndoa zitakuwa salama? Je si kuhatarisha na kuyumbisha taasisi muhimu ya ndoa na hata maisha ya wanandoa hao, hasa wa jinsia ya kike, kwamba kuna namna tu imetafutwa, lakini lengo sio ziara ila ni kupakua asali?

Asubuhi watu hao wataweza kufika maofisini? Usingizi?

Ziara hizo zilipata clearance za ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma? May be the RC is over ambitious!

Kwamba anataka maafisa ardhi, TRA na wengine wakae maofisini usiku kucha, at this digital age. Nadhani angefanya consultation, kabla hajaingia kwenye mivutano, na kuwapa hoja wapinzani.

Let him reform the system first, tena kwa kutungiwa sheria, ili jambo hili lisiende kwa personal whims, and, he should sweep all the panya road wanaozurura usiku ili watumishi wawe salama.

Otherwise, uchumi wa masaa 24 unawavuta watu, sio watu wauvute. Yaani, mazingira yatawavuta watu wakae mpaka pakuche
Unaelewa nini ukiambiwa Kuna masaa ya ziada kazini?? Je serikali huwa inalala??
 
Haya ni maoni ya Mtanzania aliyekulia uvivu, amezoea uvivu, na analipwa kwa kuendekeza uvivu.

Mtu hana habari kuwa siku moja ina masaa 24, na yote ukitaka na kuamua yanaweza kuwa ya kazi.
Ni watu kama mtoa mada anafikiri TOYOTA inatengeneezwa wakati wa mchana tu. Ndege za Boeing tunazoziona zinatengenezwa jua likiwaka tuu!!

Ewe Mtanzania AMKA.................!
Na nmpageza sana Mkuu wa Mkoa Chalamila kwa kulionyesha kwa vitendo.
 
Samahani, madaktari, manesi, polisi, wanajeshi siyo watumishi wa umma?? Vipi muda wao, unaufahamu??

Mwisho punguza:

papara

bila ya makini; kwa harakaharaka

Kila mtumishi wa umma anatakiwa kufanya kazi kwa masaa manane tu kwa siku. Ikizidi hapo atafanya kwa malipo ya ziada. Kuna kada zinafanya kazi masaa 24 ila wanafanya kwa shift. Kukiwa na jambo la dharura mtumishi atafanya hayo masaa ya ziada kwa malipo
 
Nimeona Mkuu wa Mkoa amezindua ziara za usiku mzima, tena akiwa na watumishi wa umma wa kike na kiume.

Ninachofahamu, muda wa mtumishi wa umma kuwa ofisini mwisho saa tisa na nusu. Sasa sijafahamu kuhusu huu utumishi wa mpaka usiku wa manane.

Kwanza, hao watumishi wanatakiwa kuwa kazini saa moja na nusu asubuhi, kulikoni uwalaze saa kumi na moja alfajiri? Kwa kanuni ipi ya utumishi wa umma?

Je walioolewa, na waume zao wanawasubiri, ndoa zitakuwa salama? Je si kuhatarisha na kuyumbisha taasisi muhimu ya ndoa na hata maisha ya wanandoa hao, hasa wa jinsia ya kike, kwamba kuna namna tu imetafutwa, lakini lengo sio ziara ila ni kupakua asali?

Asubuhi watu hao wataweza kufika maofisini? Usingizi?

Ziara hizo zilipata clearance za ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma? May be the RC is over ambitious!

Kwamba anataka maafisa ardhi, TRA na wengine wakae maofisini usiku kucha, at this digital age. Nadhani angefanya consultation, kabla hajaingia kwenye mivutano, na kuwapa hoja wapinzani.

Let him reform the system first, tena kwa kutungiwa sheria, ili jambo hili lisiende kwa personal whims, and, he should sweep all the panya road wanaozurura usiku ili watumishi wawe salama.

Otherwise, uchumi wa masaa 24 unawavuta watu, sio watu wauvute. Yaani, mazingira yatawavuta watu wakae mpaka pakuche
Unachofahamu ni mazowea lakini siyo kanuni au sheria.

Sheria inataka mfanyakazi awe kafanya masaa yasiyozidi na kupunguwa kadhaa kwa wiki au kabla hajapumzika.

Wale madaktari, mapolisi, wauguzi, na sehemu zingine kadhaa wa kadhaa za hudumu zinafanya kazi usiku na mchana.

Chalamila yupo sahihi, alishatangaza anataka Dar liwe jiji la biashara kwa saa 24 (jiji lisilo lala), ni lazima atembee usiku ajionee anajipanga vipi.
 
Back
Top Bottom