Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kujenga chama, kueneza chama ,kuongeza wanachama na wafuasi,kupata kura za ndio kutoka kwa watu inahitaji akili, umakini,sera,ajenda zenye kugusa maisha ya watu. Inahitaji kuwa na sera mbadala zidi ya yule aliyepo madarakani,inahitaji ushawishi wa hoja nzito na sera bora zenye kuleta matumaini kwa watu. Inahitaji mpangilio mzuri wa mawazo na akili iliyotulia. Siyo suala la kufanya mikutano mingi wala kutembelea vijiji vingi wala kusafiri umbali mrefu wala kuongea muda mrefu jukwaani.
Ili ufanikiwe kuteka hisia na mawazo ya watu na kupata uungwaji mkono , inategemeana unazungumzia nini? Sera zako ni zipi kwa kila kundi? Ni lazima watu waone Tumaini kabla ya kukupa imani yao.
Ukiangalia na kufuatilia kwa umakini ziara za Lissu kwa hakika utagundua kuwa ni za kupoteza nguvu na kujichosha tu mwili na akili na zisizo na matokeo yoyote Chanya kwa CHADEMA. Kwa sababu hakuna kitu chochote kile chenye kugusa hisia na maisha ya watu unachoona akizungumza na kutoa katika mdomo wake .hana mpangilio wa mawazo wa kuelewa lengo lake ni lipi.ni mtu anaongea tu kulingana na litakalomjia kichwani mwake.
Mfano utasikia yupo jukwaani anaongea kuwa sijuwi chama kilimpokeaje Nyarandu? Swali linakuja jambo hili linawagusa na kuwahusu vipi Wananchi? Lina tija gani kwao? Wao ndio waliompokea? Halafu hapohapo kwa usahaulifu wake anasahau kuwa mtu huyo huyo anayemshambulia aliacha ubunge wake na akaungana nao na akaenda hadi hospitalini kumjulia hali. hapa unaweza kuona Lissu ana matatizo fulani kichwani mwake yaliyo makubwa sana.
Kiufupi ni kuwa mikutano yake haina ajenda wala sera, na ndio maana amekuwa mtu wa kutunga uongo,uzushi, uchonganishi na habari za kupikwa zisizo na ushahidi wala ukweli wa aina yoyote ile zaidi ya maneno matupu ya kizushi na chuki binafsi. Ndio maana unaona na kushuhudia hata habari zake zikiwa hazina msisimko wala kuteka mijada ya kisiasa wala kuwagusa wenye akili Timamu na wanaojitambua.kwa kuwa ni mtu anayejizungumzia tu lolote linalotangulia kutoka mdomoni mwake.
Kinachomsumbua Lissu ni mihemuko iliyopita kiasi,kukosa umakini,kuongea ongea hovyo hovyo kwa kila neno linalomjia Mdomoni,kukosa mpangilio na maandalizi ya nini akaongee jukwaani,kujiona anajuwa kila kitu na yupo sahihi kwa kila kitu na yeye ndiye ana akili kuliko mwingine yeyote yule, na kwamba watanzania wote walio mbele yake ni wajinga na ndio maana anataka awaambie ujinga wowote ule akifikiria wanameza na kunyonya tu kama madodoki.
Ndio maana unaona kuna mambo Ambayo unaona yalipaswa kuzungumzwa kwenye vikao vyao vya ndani lakini utaona yeye akiongea kwa kuripuka jukwaani. Kwa sababu ni mtu aliyekosa utulivu,Busara, hekima,staha na nidhamu ya kuchunga ulimi anaopaswa kuwa nao kiongozi.Ndio maana habari zake hazichukuliwi kwa uzito wowote ule.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.