Nimengalia kwa makini na kutafakari sana kisha nikaona kuwa kuna watu wanadhani kuwa watanzania wote ni wajinga kwa kiwango wanachotufikiria wao. Sasa hivi mama Salma Kikwete ana ziara Tanzania nzima. Magari anayotumia ni mazuri sana na yapo zaidi ya manne. yale magari hayaingii akilini kuwa ni ya chama cha mapinduzi. Ni magari ya SERIKALI yaliyonunuliwa na kodi za wananchi wavuja jasho ila wanatudanganya kwa kubandika namba za kiraia. Badala ya magari hayo kufanya kazi za serikali leo yanazunguka kufanya kampeni wilaya kwa wilaya. Kwa nini yasihudumie wananchi?
Kwa nini wanatufanya wajinga? anatembelea wilaya na kuongea na kina mama. Je CCM ndio wamemuwezesha au ni pamoja na serikali maana ubavu wake ndio mkuu wa kaya.
Kwa nini wanatufanya wajinga? anatembelea wilaya na kuongea na kina mama. Je CCM ndio wamemuwezesha au ni pamoja na serikali maana ubavu wake ndio mkuu wa kaya.