Ziarani Tabora uzinduzi miradi ya Maendeleo

Ziarani Tabora uzinduzi miradi ya Maendeleo

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
966
Reaction score
6,019
Hodi hodi Tabora. Mulé mpola?! Wabéja.

Haya, tuendelee sasa kuzindua miradi ya maendeleo na kuyatangaza maendeleo ya Tabora.

Ikumbukwe, mkoa wa Tabora tayari umeshapokea takribani Trilioni 1.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya sekta mbalimbali tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya 6 chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿

Taarifa zaidi kukujia hapa✍🏻🇹🇿

IMG-20241021-WA0106.jpg
 
Nina maswali nje ya mada:-
Mama mjamzito kupewa kadi ya clinic anatakiwa kulipia shikingi 10,000?
Mama mjamzito anae hudhuria clinic kupata kipimo cha ultrasound anatakiwa kulipia shilingi 20,000?
 
Kuna watu watakuja hapa kukushangaa Mhe. Waziri kuandaa ziara ya kufungua vyumba vitatu vya madarasa. Uwe na ziara njema.
Kwa Sababu hawaelewi maana ya waziri wa Maendeleo ya Jamii kuwa ni kushuka chini iliko jamii kuendelea kuamsha Ari ya jamii ikiwemo kubadilisha fikra za jamii kazi ambayo ni mtihani mkubwa Sana. Aidha, muunganiko wa program ya malezi na makuzi ambayo ni msingi wa kuepuka mabaya mengi huku kwenye jamii ikiwemo kuna umuhimu wa elimu ya msingi ambako, watoto wengi wanaacha shule na kutorokea mitaani na huku sehemu kubwa ya jamii ikiwa haisemi.

Hivyo waje tu wanishangae na mimi nitawashangaa🥹hivi.... Mshangao kwa mshangao🥹
 
Una mkakati gani na hawa ombaomba na homeless waliozagaa mitaani na mikoa mikubwa nchi nzima?
Wengine ni watoto hawasomi, wanalala nje nk.

Una mkakati gani na wadangaji waliojaa Tanzania nzima, wengine ni mabinti wadogo ambao wameathiliwa na hizi social media na kuamini udangaji ni sehemu ya maisha na ni jambo la kawaida sana huku tukiwapromote wasanii ambao nao wanadhidi kuchochea hali hii.

Maendeleo ya technolojia yamekuja na athari kubwa kwenye jamii yetu na tunaonekana kama hatuna control na kuachia nyimbo, maudhui ya hovyo nk matokeo yake kumetokea mmomonyoko mkubwa WA kimaadili, vijana hawafanyi kazi, mabinti wamekuwa wadangaji/malaya nk.
Kama wizara kuna programs zozote za kupambana na haya?
 
Ni kweli kabisa. Na maendeleo ni hatua kwa hatua.
 
Mimi mmojawapo, huko mkoani wapo mabosi wa mikoa, wilaya nk wa hiyo wizara anayoiongoza.
Uongozi ni kushuka na kukagua utekelezaji wa sera na kuwapa moyo, pia sauti inaenda mbali zaidi akija mgeni, na pia, miradi ni mingi Sana ambapo ingine walizindua wao, ingine akaja Mhe Rais, mingine akaja Mhe Makamu wa Rais, mingine akaja Mhe Waziri Mkuu na mingine akaja Mhe Mhe Naibu Waziri Mkuu na haijaisha tumekuja sisi mawaziri. Uone sasa ukubwa wa utekelezaji wa serikali ya Awamu ya 6 kwenye mafuriko ya miradi. Na Mimi nitaacha mingine wataendelea tena wenye mkoa hadi mtendaji wa kata na bado haitaisha. Ni hivyo tu🇹🇿😍
 
Una mkakati gani na hawa ombaomba na homeless waliozagaa mitaani na mikoa mikubwa nchi nzima?
Wengine ni watoto hawasomi, wanalala nje nk.

Una mkakati gani na wadangaji waliojaa Tanzania nzima, wengine ni mabinti wadogo ambao wameathiliwa na hizi social media na kuamini udangaji ni sehemu ya maisha na ni jambo la kawaida sana huku tukiwapromote wasanii ambao nao wanadhidi kuchochea hali hii.

Maendeleo ya technolojia yamekuja na athari kubwa kwenye jamii yetu na tunaonekana kama hatuna control na kuachia nyimbo, maudhui ya hovyo nk matokeo yake kumetokea mmomonyoko mkubwa WA kimaadili, vijana hawafanyi kazi, mabinti wamekuwa wadangaji/malaya nk.
Kama wizara kuna programs zozote za kupambana na haya?

Swali zuri Sana, nitakuja kulijibu nikianzia na uzinduzi wa mkakati wa tarehe 15 Mei 2024 Dodoma, pale viwanja vya Chinangali Park, ambapo mawaziri wa kisekta na wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa walikuwa wanatoa ahadi zao. Sema HUKUFUATILIA. Ila Leo ngoja kwanza tumalize kuzindua mafuriko ya miradi huku Tabora kisha tutakuja na kwenye ajenda hii. Huwa napenda Sana maswali kama haya maana yanaongezea sauti kwenye uwepo wa mikakati kwani, pengine huwa kuna baadhi yetu hatufuatilii hata kurasa za wizara na taarifa za habari hivyo, maswali kama haya huturejesha kwenye kusema tena na tena, ahsante Sana 🇹🇿😍
 
Back
Top Bottom