Ziarani Tabora uzinduzi miradi ya Maendeleo

Ziarani Tabora uzinduzi miradi ya Maendeleo

Waziri mzima unakuja hapa kujinasibu kwa kuzindua mradi wa vyumba vitatu, VYUMBA😂
ma ma mae walai nchi hii ni kama tumelaaika, hivi kwa haraka haraka tu msafara wako kuanzia mafuta, posho na mengineyo inagharimu kiasi gani.

Hivyo vitu vya kipuuzi, vinafaa kuzinduliwa hata na katibu kata huko, mngekuwa serious hata mwenyekiti wa kijiji anaweza zindua hii kitu.

Nyie viongozi ndio mnatifelisha pakubwa, taifa linakwama kwa ajili yenu, uwajibikaji zero, badala mfanye ya maana muonekano, mnashindwa mnakimbilia kuonekana katika vitu vidogo,
Ndio maana mpaka leo taifa linajengewa vyoo kwa misaada.
Miaka 60+ ya uhuru ila ukichora graph ya maendeleo yetu vs muda ni inasikitisha.

Haya kila la kheri kwenye uzinduzi, na kwa kiwa mnatuongozamaiti zinazotembea, msipate shaka endeleeni kula cake ya taifa.
 
Unajua humo kwenye shule za msingi kiasi gani mmomonyoko wa maadili unaendelea kwa kuwa tu, huko majumbani wanakotokea watoto hakuna anayewapa elimu hiyo? Unajua kuwa ubakaji na ulawiti wa watoto unaanzia majumbani kwa 60% kisha unahamia mashuleni na kusambaza? Unajua kuwa kwa mshangao huo sambamba na mkutano wa wananchi Leo hii wote mtajua mengi msiyoyajua? Na mikakati itokanayo na ziara hii itaokoa taifa lote? Waza wa upana na kutoka nje ya box.

Pia unajua kuwa tayari nimeshaupiga mwingi kwa kukufanya na wewe uje usome Uzi huu na kuushangaa na kuuliza maswali huku nami napata fursa ya kupenyeza mengine mengi ya faida ambayo hayajulikani ikiwemo kuwa, Tabora wamepokea TRILION 1.1 tangu Serikali ya Awamu ya 6 ingine madarakani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo bàadhi tu ndiyo nazindua kati ya tele tele ambayo imeshazinduliwa na mingine inaendelea.

Hivi pia unajua kuwa ukiacha magorofa makubwa ya nje, mengine yako kwenye fikra zetu na hayajulikani hivyo yanahitaji kujengwa kwa viongozi kutembelea jamii na kuwapa elimu ya kubadilisha fikra Ili mfano kuepuka mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia na kwa watoto na kuzijua fursa za kiuchumi? Unajua kama kuna billion 18.5 zinaenda kutolewa mkopo wa mtu mmoja mmoja kwa Wafanyabiashara ndogo ndogo wenye kitambulisho cha kidigitali? Watajuaje kama sijaja

Tafakari..

Picha; nikipokelewa na Mhe Paul Chacha, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, mwenye sauti ya bluu na timu yake ya wataalamu wa mkoa.
 
Attachments

  • IMG-20241022-WA0015.jpg
    IMG-20241022-WA0015.jpg
    71.1 KB · Views: 2
  • IMG-20241022-WA0013.jpg
    IMG-20241022-WA0013.jpg
    52.7 KB · Views: 1
  • IMG-20241022-WA0011.jpg
    IMG-20241022-WA0011.jpg
    54.2 KB · Views: 1
  • IMG-20241022-WA0016.jpg
    IMG-20241022-WA0016.jpg
    71.1 KB · Views: 2
waziri chapa kazi watanzania wengi wananufaika na uongozi wako,dua njema zikutangulie katika majukumu yako ya kila siku

binafsi huwa na utaratibu wa kuwaombea viongozi wa nchi chama na serikali kila asubui
 
Hivi waziri we huogopi ,yaani shule zinaongeza umaskini tu hapa nchini kweli mtu anafundishwa kitu na mtu ambaye hajawahi hata kufanya hicho kitu .unakuta mtu anaingia darasani kufundishwa biashara na mkufunzi ambaye hajawahi hata kufungua kiosk BS.,kweli unatoa pesa yako kugharamia elimu ambayo ndio inazalisha Upuuzi mwingi nchini
 
Swali zuri Sana, nitakuja kulijibu nikianzia na uzinduzi wa mkakati wa tarehe 15 Mei 2024 Dodoma, pale viwanja vya Chinangali Park, ambapo mawaziri wa kisekta na wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa walikuwa wanatoa ahadi zao. Sema HUKUFUATILIA. Ila Leo ngoja kwanza tumalize kuzindua mafuriko ya miradi huku Tabora kisha tutakuja na kwenye ajenda hii. Huwa napenda Sana maswali kama haya maana yanaongezea sauti kwenye uwepo wa mikakati kwani, pengine huwa kuna baadhi yetu hatufuatilii hata kurasa za wizara na taarifa za habari hivyo, maswali kama haya huturejesha kwenye kusema tena na tena, ahsante Sana 🇹🇿😍

Thanks, endelea na majukumu yako Mama.
Usituchoke wananchi tuna mengi kwenye vichwa vyetu mengine yakukera na kufurahisha pia, mengine ni msaada pia kwenye nchi hii.

Hope utakuja na data, wengine ni waumini wa matokeo na data sio makaratasi na mipango.
Utuambie mkakati wako utaleta matokeo kwa kiasi gani na kwa muda gani tutegemee kuona matokeo lini.
 
Hongera @Dr Gwajima D kwa kuwa mfano bora wa Mawaziri wasioogopa challenges na wanaojibu watu wa kawaida kabisa hapa JF.
Ziara njema mama
 
Back
Top Bottom