Ndugu, upo sahihi kuhusu PSU lakini tambua hivi;
PSU inaundwa na idara zifuatazo
1. TISS- Hawa ndiyo waratibu wakuu wa ulinzi wa rais. Ndani ya TISS Kuna kitengo Cha ulinzi wa viongozi wakuu wa kitaifa ( mashuhuri)
2. Jeshi la polisi - kwa kushirikiana kwa ukaribu na TISS, polisi kupitia kitengo Cha VIP protection unit Wana askari maalumu kwa ajili ya ulinzi wa executive leaders.
JWTZ haihusiki moja kwa moja na ulinzi wa rais, labda itokee uhitaji wa kutoa nguvu ya kiulinzi kwa vyombo tajwa hapo juu ( yaani TISS na polisi).