Zifahamu athari zitokanazo na matumizi ya dawa (adverse drug reactions )

Zifahamu athari zitokanazo na matumizi ya dawa (adverse drug reactions )

Apotheker

New Member
Joined
Jul 8, 2025
Posts
3
Reaction score
2
Kumekua na Changamoto mbalimbali zitokanazo na matumizi ya dawa kwa watu mbalimbali,wengine hujihisi kuwashwa mara baada ya kutumia dawa fulani ,wengine hujihisi kuchoka mara baada ya kutumia dawa fulani na wengine hali zao kubadilika kabisa na kuzidi hali walizokua nazo kabla ya kutumia dawa hizo.Uzi huu utakusaidia kuelewa athari mbalimbali zitokanazo na matumizi ya dawa, namna gani ya kukabiliana nazo athari hizo na mwisho kabisa jinsi ya kuripoti athari hizo.

ADR ni nini hasa ?

Athari zitokanazo na matumizi ya dawa (Adverse drug reactions ) ni majibu ya mwili ambayo hayatarajiwi,yanayotokea baada ya kutumia dawa dawa kwa njia sahihi na dozi sahihi kama ilivyoelekezwa na Mfamasia/Daktari.

NOTE: ADR haijumuishi dose inayoweza kuleta Overdose/Toxicity bali ni dozi iliyotumika kwa wakati sahihi na kwa njia sahihi.

Mfano wa ADR

- Mtoto anaetumia penicillin akapata upele na kuvimba usoni ndani ya saa chache

-Kuhisi usingizi mara baada ya kutumia cetrizen

1.AINA ZA ADR
Kuna aina kuu mbili za ADR
TYPE A (Augmented)
Hizi Mara nyingi zinatabirika na hutatuliwa kwa kupunguza dozi au kusitisha dawa
Mfano:Kuharisha mara baada ya kutumia erythromycin

TYPE B (Bizarre )
Hizi hazitabiriki na hutokea kwa watu wa chache kwa sababu za kurithi au kibaolojia
Mfano : Kupata allergy/Mzio mara baada ya matumizi ya Penicillin

2.DALILI ZA ADR
  • Zifuatazo ni dalili za ADR
  • Homa
  • Kuwashwa
  • Kizunguzungu
  • Maumivu ya viungo

3.WATU GANI WAKO HATARINI KUPATA ADR ?
  • Watoto na Wazee
  • Matumizi ya dawa nyingi kwa wakati mmoja
  • Wagonjwa wa ini au figo
  • Watu wenye vinasaba vyenye mzio wa dawa

4.HATUA GANI ZA KUCHUKUA UKIPATA ADR ?
  • Kusitisha matumizi ya dawa (Baada ya kuwasiliana na Mfamasia/Daktari)
  • Kuripoti kwa haraka kituo cha afya kilicho karibu nawe
  • Kuripoti kwa haraka kituo cha afya kilicho karibu nawe
NOTE: ADR inapaswa kuripotiwa mapema zaidi kwani hatua za haraka zisipochukuliwa inaweza ikasababisha kifo kwa mtumiaji wa dawa hio.

5.WAPI KWA KURIPOTI UKIPATA ADR ?
Kituo cha Afya kilicho karibu nawe ,Famasi yoyote iliyo karibu nawe au TMDA (Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania)

Jinsi ya kuripoti ADR ( TMDA )

Wasiliana nao kwa njia zifuatazo

Email:[email protected]

Phone :0658445222 au 2450751

6.MWISHO

Ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa afya mara kwa mara pale unapohisi mabadiliko yoyote kiafya baada ya kutumia dawa yako.

Je umewahi kukumbana na athari yoyote baada ya kutumia dawa ? karibu kwenye mjadala pamoja na maswali yote kuhusu athari baada ya matumizi ya dawa .
 
Back
Top Bottom