Zifahamu Engine oil

KndNo1

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2021
Posts
627
Reaction score
2,049
Tabia yake
Oil inakuwa nyepesi jinsi inayopata joto na kuwa nzito jinsi inavyopoa. Kwahiyo kufahamu viscosity sahihi kwenye cold start na operating temperature ni muhimu!

Viscosity ni resistance ya oil kuflow.. Kwahiyo oil yenye viscosity kubwa ni ngumu kuflow hence nzito zaidi..!

Kazi yake
Kulainisha msuguano wa vyuma ndani ya engine!

Oil pump inaizungusha oil kwenye sehemu za engine kama damu inavyozungushwa kwenye mishipa..
Wakati inarudi kwenye sump inakutana na oil filter ambayo inachuja uchafu na kuhakikisha oil inavyozungushwa ipo vizuri.

Sump huwa inakuwa chini kabisa ya gari, as gari inatembea cold air inapooza oil kwenye sump na kusaidia kutoa joto kwenye engine.

Aina zake
Mineral oil - hii inatokana na kuchujwa kwa crude oil..haina mambo mengi kwenye uzalishaji wake..molecules zake hazipo uniform.. Kwahiyo flow sio nzuri..bei ipo chini.. Interval ya service nayo ni karibu karibu..!

Semi Synthetic na Synthetic oil - hizi zipo very refined.. Hasa hasa synthetic.. Ni oil zinazotengenezwa LAB kwa formula.. Kwahiyo molecules zake zipo uniform.. Flow inakuwa nzuri. Interval yake unaenda kilometers nyingi..
Hapa panahitaji umakini.. Oil inaweza kuwa nzuri kwa kilometers nyingi ila oil filter isiwe na uwezo wa kwenda kilometers nyingi.

Grading ya Oil
Oil imekuwa graded na hawa SAE kwenye makundi 2. Monograde na Multigrade.
Mono kama jina lake.. Ina viscosity moja throughout. Wakati Multi ni zaidi ya moja.

MFANO wa Monograde SAE40.. Hii inakuwa na viscosity ya 40 kuanzia cold start mpaka operating temperature.. Kwahiyo ukiwasha gari inabidi uipe muda kidogo ili oil ipande vizuri kwenye engine.. Unaweza ukawasha gari then ukaenda kuoga.. Mpaka ukitoka mambo yamekaa sawa.

Hizi zinafaa kwa mazingira ambayo hakuna temperature change kubwa kwenye seasons kama hapa TZ..!

Mfano wa Multigrade 5W40.. Hii inabehave kama oil ya 5 viscosity kwenye cold start na 40 viscosity kwenye operating temperature.

Kwahiyo ukiwasha tuu gari. Oil itapanda chap kwenye engine haihitaji kusubiri muda. Hizi zinafaa kwenye mazingira yenye mabadiliko makubwa ya temperature ndani ya mwaka.

Hii inapunguza usumbufu wa kubadilisha oil wakati wa winter na summer.

0W40 ni nyepesi zaidi ya 5W30 kwenye winter(cold start) ila ni nzito zaidi kwenye summer(operating temperature).!
 
Uzi mzuri.

Ungeongezea nyama mfano unaposema 5W30 unamaanisha nini?

5 ina maana gani?
W ina maana gani?
30 ina maana gani?

Winter ni 5 au 30? Viscosity ni 5 au 30? Na je is viscosity direct proportional to temperature?

Kwa mazingira ya TZ ni oil gani inatumika zaidi? Na range ya temperature ni ipi? Na pia hiyo inayoangaliwa ni temperature ya engine au external temperature?

Magari yenye engine ndogo yanatumia oil range ipi? 0w30 au nini?

And other nyama nyama...
 
3000km au 5000km ni kutokana na ubora wa oil.. Mineral vs Synthetic..!
Watengenezaji ndio wanajua ubora.. Bei zitapishana pia..!

Magnetic.. Hizo ni additive(magnetic particles) wanaongeza manufactures.. Wamegundua kukiwa na particles zinasaidia kupunguza wear ya engine..!
Hii ni sababu zitanasa kwenye walls za engine.. Then kutakuwa na protective layer..!

5&30 zote ni viscosity.. Ndio maana inaitwa Multigrade..
5 ni viscosity ya winter..
30 viscosity kwenye operating temp..
 
uzi mzuri kwa watumiaji wa magari, tusio nayo tutulie tuli
 
hongera kwa elimu nzuri...
 
Kwa gari ndogo ya engine ya 2Nz unashauri oil namba ngapi itumike?
 
Naomba kuongezea kitu hapa, hakuna oil ambayo imetengenezwa specific kwenda km 3000 au 5000 Bali hiyo ni assumption ya mafundi tu baada ya kuona madumu ya total yana lebel oil zao kwa no na wakawaaminisha kwamba hizo ndio km zinazotembea Hadi ufikie kubadilisha oil kwa kufanya hivyo mnaua magari kwa sababu ile sio km ya oil Bali ni business name ya kampuni ikisomeka hivyo kwenye products zao

Badala yake ukweli ni kwamba monograde oil nyingi zinashauriwa kubadilishwa kwenye gari angalau si zaidi ya km 2000 tokea uiweke na hii ni kwa sababu ubora wake ni mdogo na mfano wake ndio hizo sae40 etc na multgrade oil ambayo sio synthetic ibadilishwe si zaidi ya 3500 na zile ambazo ni multgrade oil na synthetic ibadilishwe sii zaidi ya km 10,000 kulingana na material yaliyotumika kutengenezwa.
 
Shukrani kwa mchango.. Sema hapo kwa mafundi haipo sawa.. Madumu ya Total yenye maandishi umeanza kuyaona lini..!!? Kabla ya hapo mafundi walikuwa wanasoma wapi..!!?

Achana na labels za kwenye madumu.. Oils zinatengenezwa kwa kilometers kadhaa..
Ndio maana haijalishi ni mineral au synthetic oil miaka mitano baada ya kuwa packed kwenye dumu then haijatumika.. oil inakuwa haifai..zote zinaexpire sawa..
Ila zikiwa running kwenye engine mineral oil itachoka mapema zaidi ya synthetic.. Kwahiyo kilometers ndio muamuzi..!
 
Nikiri hapa umeongeza neno.... So ni range tu inayo matter
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…