Zifahamu nchi zisizokuwa na rushwa Afrika Mashariki. Tanzania yashika nafasi ya 2

Zifahamu nchi zisizokuwa na rushwa Afrika Mashariki. Tanzania yashika nafasi ya 2

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Taasisi ya Transparency International imeorodhesha nchi zinazoongoza kwa rushwa duniani na kwa Afrika Mashariki Tanzania inashika namba 2 kama nchi ambayo ina rushwa kidogo zaidi katika ukanda huu.



corruption .png

Source: Buzzroom Kenya, Transparency International
 
Wakuu,

Tanzania tunaendelea kung'aa kimataifa. Royal tour na safari za nje zinaendelea kupendezesha sifa za nchi yetu

Mama anatekeleza. CCM mitano tena!

================================================

Taasisi ya Transparency International imeorodhesha nchi zinazoongoza kwa rushwa duniani na kwa Afrika Mashariki Tanzania inashika namba 2

Source: Buzzroom Kenya, Transparency International
...from least to most corrupt

Hujaelewa hiyo lugha hapo wanamaanisha zenye kiwango kidogo cha rushwa kwenda viwango vikubwa, Kwa list hiyo Rwanda ni namba 1 kwa rushwa kidogo na Tanzania ni ya pili
 
Rwanda wanaendelea kung'ara katika kupambana na rushwa.
 
Yaani hadi DRC na Manyang'au Kenya tumewazidi! Hii ni hatari sana. Na usikute trafiki ndiyo watakuwa wametubeba kwenye hiyo orodha.
Traffic police kunanuka rushwa. Na sijui takukuru wamekwama wapi kufuatilia hiki kitengo. Ingekuwa mimi ningewadaka 2000 Kila siku na wangeogopa kupokea rushwa. Pesa za moto wanazo wanai maofisini tu.
 
Tatzo lugha huelewi bobgo sisi hatujawahi kupenda vyetu kila kitu tunapinga hata sehemu tufanye vizuri
 
Traffic police kunanuka rushwa. Na sijui takukuru wamekwama wapi kufuatilia hiki kitengo. Ingekuwa mimi ningewadaka 2000 Kila siku na wangeogopa kupokea rushwa. Pesa za moto wanazo wanai maofisini tu.
Takukuru tokeni maofisini mkarunguke na mkaanzenma magari ya abiria. Askari akisimamisha bus mpe driver au Kondakta pesa ya moto akishampa muibukie mkamate. Mbona mtafanikiwa kwa 70% kupunguza rushwa kwa hawa traffic police!?
 
Kichwa cha habari kimekaaje?
Hivi ukiwa kinara wa rushwa, maana yake si ndiyo umetopea kweye rushwa balaa, au!?
 
Hapa kuna mfano wa sentensi inayotumia "least to most" kuonyesha kiwango cha rushwa:

"The Corruption Perception Index ranks the East African Community (EAC) member states from least to most corrupt as follows: Rwanda, Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, and South Sudan."

Sentensi hii inaeleza kwamba Rwanda inaonekana kuwa na kiwango kidogo cha rushwa, ikifuatiwa na Tanzania, na kadhalika, hadi South Sudan, ambayo inaonekana kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha rushwa. Hii inamaanisha kwamba nchi zimepangwa kulingana na jinsi rushwa inavyoonekana kuwa mbaya, kutoka nchi ambayo rushwa inaonekana kuwa ndogo zaidi hadi nchi ambayo rushwa inaonekana kuwa kubwa zaidi.

Hawa waliotoa hizo takwimu nao wamehongwa.
 
Uzi ukiwekwa huwa hamtaki kusoma mnakimbilia kucomment?
Hiyo list ni from least to most corrupt. Wameanzia yenye viwango vya chini kwenda juu
Bado haiwezi kuondoa ukweli wa kukithiri kwa vitendo vya rushwa, na hasa kwa askari wetu wa usalama barabarani.
 
Back
Top Bottom