Zifahamu njia rahisi za kupunguza kitambi

Raphael focus

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2018
Posts
779
Reaction score
4,564
Habari ya muda huu wanajanvi!

Kama mada inavyo jieleza hapo juu.

Hizi ni njia tatu bora na rahisi za kupunguza kitambi ambazo huitaji kwenda jimu au kukimbia kwenye ukingo wa bahari.

NJIA YA KWANZA: kopa mkopo mkubwa benki
Kwa wewe unaehitaji kupunguza kitambi kopa mkopo benki, zile presha za kupigiwa simu kila mara na benki ku kumbushia deni lao kwa mwezi mzima. Kumbuka utakapokuwa umekopa mkopo haijalishi ni kiasi gani, kama utakuwa umepewa mkataba wa miaka mitano kulejesha mkopo maana yake utakuwa umepigiwa simu kwa miaka mitano mfurulizo.

NJIA YA PILI: tembea na mwenza wa mwanajeshi
Maana yake kama wewe ni kidume tembea na mke wa mwanajeshi, kama wewe ni dada unasifika mjini kwa kubeba waume za watu tembea na mume wa mwanajeshi.

Hapa kutokana na zile pilika pilika za kutafutwa na mikwaju na kuruka fensi. Mara umekaa mjeshi anakutokea barazani, hapa ndo pale unapoamuwa kupitia uwani kwa sababu ya presha.

NJIA YA TATU: nunua gari bovu
Ulishasikia gari ya M1.8? au laki saba? Yaani gari ambayo hutaki kuagiza kutoka Japan, gari ambayo hutaki kununua kwenye yadi, ila gari utakayo nunua ni kutoka mikononi mwa mtu.Gari ambayo ukiwa ndani unaona lami kupitia matundu huku kwenye madimbwi ya maji ukipita kwa tahadhari kubwa.

Hapa mpela mpela wake pale inapozima na unaamuwa kushuka ili uisukume .Ghafla unamuona trafiki anakuja kuikagua ile gari ambayo haina hata vibali ile presha yake sasa hapo kitambi ndo kinakata ghafla.








ONGEZA NA ZAKO.
 
Hebu toa ufafanuzi mkuu!

kama hujaelewa soma comments.
Huo ndo ukweli...Tress iwe physical(too much exercise without time to recover) au Emotional stress huongeza kwa kasi hormone ya Cortisol...Cortisone ni Fat Storage Hormone akishirikiana na ndugu yake Insulin
 
Endesha pikipiki ya kichina route ndefu ya kuanzia kilometa 500. Baada ya safari ya kwenda na kurudi kitambi kwisha.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sikutegemea kukutana na hizo njia. Haki mimecheka.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sikutegemea kukutana na hizo njia. Haki mimecheka.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] mkuu na wewe unakitambi[emoji851] chukuwa mkopo benki mkuu, au nunuwa gari bovu [emoji851] [emoji851] [emoji851].

kama hujaelewa soma comments.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…