Zifahamu siri za maisha

Zifahamu siri za maisha

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
(Toka mtandaoni)

[emoji840]Soma kwa umakini sana Soma Siri zote[emoji840]

[emoji3502]Maisha hayana formula lakini yana siri kibao! Kamata hizi 11, zikikufaa zichukue na unibariki kimyakimya, hazikufai futa bila kunitukana kimyakimya![emoji286][emoji286]

Siri ya kwanza;

[emoji1428]Tengeneza connection na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha kula maana "kikulacho kinguoni kwako!" Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake![emoji2047][emoji2047]

Siri ya Pili
[emoji1428]Usimwamini sana rafiki yako ,kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye Wewe si rafiki yako! Kama hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako then boss wako ukurushie. Utatamani kufa[emoji3][emoji3]

Siri ya tatu;
[emoji1428]Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni 1.bahati, 2.kipaji na 3.bidii yenye akili! Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana[emoji276][emoji276]!

Siri ya nne:
[emoji1428]Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni masikini kumpata rafiki bilionea maana wahenga walisema ndege wanaofanana huruka pamoja. Kama huamini kamuulize Mo na Haji Manara[emoji87][emoji87]

Siri ya tano;

[emoji1428]Ukiona kila mtu anakurushia mawe usijifariji kwamba mti wenye matundo ndo unaopigwa mawe, kuna miti mingine inapigwa mawe kwa sababu ina nyoka! Kikubwa jitathimini pengine wewe ni Mfalme mwenye mkia, ila hujauona[emoji276][emoji276]

Siri ya Sita
[emoji1428]Kuwa makini sana na watu wanaosema tuko nyuma yako maana ukigeuka unaweza usiwakute Kama kivuli chako mwenyewe ikifika usiku kinakukimbia vipi huyo mtu asiyekula kwako?[emoji2378][emoji2378]

Siri ya Saba
[emoji1428]Ili ufurahie maisha jifunze kujinyenyekeza na siyo kujikomba! Unyenyekevu ni kiwango cha juu kabisa cha matumizi ya akili, kujikomba ni kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya akili! Moja ya madhara ya kujikomba ni kuishi maisha yako yote umepiga magoti![emoji851]

Siri ya Nane

[emoji1428]Kabla hujafanya maamuzi jitahidi kupata ukweli wa jambo kutoka pande zote. Leo hii watoto wengi hawana mahusiano na baba zao kwa sababu ya kusikiliza ufundi wa mama zao katika kusimulia mabaya ya baba zao! Huyajui ya mama yako kwa sababu baba yako alichagua kuyaficha! Kama unamchukia baba yako hebu muombe msamaha kwanza halafu mwambie akusimulie ya mama yako ufe[emoji3]

Siri ya Tisa
[emoji1428]Mlango mmoja ukifungwa usihangaike kuufungua, unaweza ubomoa bure.
Pita hata dirishani maana kisicho riziki hakiliki! Asiyekupenda muache aende zake, tena mpe na nauli kabisa[emoji2957]

Siri ya Kumi
[emoji1428]Hata kama umeishafika mbali kiasi gani, ukijua umepotea njia rudi kuliko kupotea jumla! Kuanza upya si ujinga.Bora uanze upya ufike salama kuliko kuendelea usifike [emoji2321]

Siri ya Kumi na moja
[emoji1428]Haijalishi umri umekwenda kiasi gani kama una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri ni namba tu na uzee hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto watayabusu tu[emoji2089][emoji2089]!

[emoji1374]muwe na Siku Njema[emoji1374]
 
Mi hizi ishu za marafiki huwa nazichukulia kama watu wa kupiga nao story, kwenda viwanjani, n.k na hapo kigezo kikuu ni kuwa level moja hasa katika uchumi, maana huwezi ukawa boss wa taasisi kubwa eti unamwona steve nyerere ni rafiki 😂😂😂 jamaa anakuona ngazi tu, kwa hio ni muhimu sana uwe na marafiki hamjapishana sana, lasivyo moja atakuwa chawa, ataanza kuhisi unamnyayasa hata ukimpa msaada, ataogopa kukukosoa ili kulinda tumbo lake, n.k
 
Duh ukitimiza ndoto watayabusu tu[emoji120][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Haijalishi umri umekwenda kiasi gani kama una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri ni namba tu na uzee hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto watayabusu tu[emoji2089][emoji2089]![emoji23]
 
Back
Top Bottom