Zifahamu wilaya 5 kwa uwekezaji na biashara kanda ya kaskazini....Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara.
1. KARATU. Hii ipo namba 1 sababu kuu ni kiungo cha utalii kwa nchi ya Tanzania na pia ni mapito ya barabara kutoka Arusha to Mara na barabara ya Arusha To Maswa.
2. BABATI. Ni mji unaokua kwa haraka sababu kuu ni Makao makuu ya mkoa wa Manyara pia huzungukwa na wilaya Za Kondoa, Hanang na mbulu zinazoitegemea kiuchumi, pia inachagizwa na uwepo wa karibu wa majiji ya Dodoma na Arusha ukiachilia mbali barabara ya Moshi kuelelea Singida, Tabora na Kanda ya Ziwa.
3. SAME. Mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na idadi kubwa ya watu ndani ya wilaya hii kupelekea kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi na pia kutokana na umbali wa Miji mikubwa kutokuwa karibu yaani Tanga jiji na Manispaa ya moshi, hivyo Same hubeba mahitaji ya maeneo jirani mfano Lushoto, Mwanga na Simanjiro.
4. HIMO. Huu ni mji ndani ya Wilaya ya Moshi vijijini, Himo imeibeba njia panda ambapo kuna mizani kubwa zinazohudumia barabara inayoelekea Arusha To Dar, Tanga na Kuelekea Kenya katika bandari ya Mombasa. Eneo hili linakua zaidi kibiashara sabubu kuu ikiwa n uwingi wa watu katika wilaya hii kubwa katika mkoa wa kilimanjaro hivyo mahitaji muhimu huanzia na kupatikana hapa, pia soko kubwa la mahindi na nafaka nyingine lipo Himo.
5.MKINGA .. Wilaya mpya mkoani Tanga inayohitaji uwekezaji mkubwa hivyo kuibua fursa nyingi kwa wanaohitaji kuanza biashara mpya.
Wilaya nyingine nyingi kwa kaskazini mwendo wake sio mkubwa kimaendeleo kama hizo tajwa hapo. Ni maoni binafsi sio ya serikali.