Wadau, kuna aina kuu tatu za mchepuko.
1. MCHEPUKO LAMI
Huu mchepuko hauna shida yoyote(hategemei kitu chochote kutoka kwako) sana sana yeye ndo atakuwa anakusaidia. Utaupenda mchepuko huu!
2. MCHEPUKO KOKOTO.
Mchepuko huu unasumbua sn na maswali km "upo wapi?", "Unafanya nn?", "Utakuja saa ngapi?", "Leo zamu yangu lazima uje na km huji nakufuata mbele ya mke" n.k.
3. MCHEPUKO VUMBI
Dah! Mchepuko huu ni noma
Mchepuko unakutegemea kwa 90% kwa kila kitu.
Mchepuko unakuchafua kweli kweli, unakuchuna kweli kweli. Mchepuko huu mpaka wife atajua coz huduma lazima zipungue.
Ongezea sifa za michepuko hapo juu au ongeza aina za michepuko unayoijua
Tafakari upo katika mchepuko gani?
Acha michepuko weweee!