Zijue Alama za barabarani pamoja na matumizi yake

Uliza tu.
kwenye hizo alama za kudhibiti mbona huwa naziona kwenye njia ya makutano hiyo ya Ruhusu na simama..

swali lingine, natakiwa kuacha umbali gan kat ya gari langu na gari jingine tukiwa barabara kuu

Naomba na ufafanuzi wa ile mistari ya njano na meupe barabarani ile mirefu na ile iliyokatikakatika vipande
 
Swali la kwanza mara nyingi utumika pale panapokuwa na matengenezo kwenye barabara.kuna mtu uwa anashika bango la GOupande mmoja na STOP upande wa pili.
Swali la pili sijajua ni mita ngapi nimesahau ila unatakuwa uache umbali wa kutosha.
Swali la tatu MISTARI YA NJANO.pembeni ya barabara inaonyesha mwisho wa mapana ya barabara.
MSTARI MWEUPE WA KATI ULIONYOOKA.unamkataza dereva kulipita gari la mbele yake.
MSTARI MWEUPE WA KATI ULIOACHANA ACHANA humruhusu dereva kulipita gari la mbele yake.
Ni hivyo.kama haujaelewa au kuna mapungufu WATAKUJA WENGINE KUSAHIHISHA.
 
Bila shaka atakua amepata alichokitaka...
 
Thread yenye kujenga sana hii, aksante Mkuu, ila uwe tayari kutoa maelezo ya ziada pia.
 
Maelezo yaliyotolewa kwenye baadhi ya alama hayatoi ufafanuzi mzuri, hasa kwa madereva wanafunzi. Mfano alama ya R3, Maelezo yake yanatakiwa kuwa, Alama ya amri ya kukataza, Barabara imefungwa kwa magari yanayo ingia, huenda ikawa wazi kwa Magari yanayo toka.

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…