Zijue Alama za barabarani pamoja na matumizi yake

Zijue Alama za barabarani pamoja na matumizi yake

Mabasi ya mizigo? Halafu picha ya Lorry
Yaani kama Google translate vile
 
Ule mstari wa katikati upi Huwa unakataza kuovertake ulio solid au ule wa dot dot

Kawaida mistari ile ukiikuta mara nyingi ipo hivi kwenye kona au mlima au kwenye hatari yoyote ile kama kwenye makutano ya njia ya reli n.k,sasa kwa sheria za barabarani kama mistari ipo 2 ule wenye dot dot kama unavyouita wewe ndiyo wa kwanza kwa upande wako unaruhusiwa kuovertake,maana yake ni wewe ushaipita hatari kwa hiyo upo huru kuuvuka kama ni kona ushaipita mbele unaona kila kitu.Na kama ule ambao continuous strip ni wa kwanza kwa upande wako wewe halafu pembeni upo pembeni discontinuous strip.Wewe huruhusiwi kuuvuka kwa sababu mbele yako bado hujaivuka hatari.kama kuna kona maana yake wewe mbele haupo huru kuovert.kiasi chake utakuwa umeelewa [emoji120][emoji120].Na kama barabara ina yote miwili double continuous strip.huruhusiwi kuivuka kamwe.ila na upo mmoja continuous strip hurusiwi pia kuovertake yaani mpaka uuvuke mstari wenyewe,ila kuovertake gari unaruhusiwa barabara kama ni pana au kama kuna chombo cha usafiri ambacho kama pikipiki unaruhusiwa.muhimu usiuvuke tu mstai.
 
Ule mstari wa katikati upi Huwa unakataza kuovertake ulio solid au ule wa dot dot

IMG_2285.jpg
IMG_2286.jpg

Ni hii unayoizungumzia
 
Mstai huo mweupe ndio unaokataza ku overtake mara nyingi unawekwa ktk kona kali ktk miteremko na ktk vilima sehemu ambazo dereva haoni mbele anakoelekea na yule anaetoka upande wa pili pia
 
Unapouona huo mstari mweupe mreefu bila dot dot nyeupe maana yake hutakiwi kuovertake hiyo sehemu ukiwa ktk mteremko ukaona huo mstari mweupe mreefu kushoto kwake kuna dotdot maana yake unaruhusiwa kuovetake hilo eneo . Ila yule anaetoka upande mwingine huo mstari mweupe mrefu unamkataza .ukiona mahali dot dot kila upande mstari mweupe haupo maana yake hilo eneo siyo hatarishi unaruhusiwa kuovetake na yule anaetoka upande wa pili pia anaruhusiwa kuovertake
 
Nimeona alama ya kichwa cha binadamu afu katikati kimechorwa mstari mwekundu! Alama hii nimeiona maeneo ya Mombo - Korogwe! Ni nini hicho?
 
Kuna ambazo nimeona kwenye barabara ya Dar Moshi sijawahi ona popote hata hapa. Mara limechorwa sikio kubwa then ukakatiza mstari kama kulikata, nyingine kimechorwa kichwa kikubwa ukakatiza mstari kukikata, halafu kuna nyingine nimeona Dar kuna S hapa sijaziona, labda ni za tanzania tu.
 
Dah
Kuna ambazo nimeona kwenye barabara ya Dar Moshi sijawahi ona popote hata hapa. Mara limechorwa sikio kubwa then ukakatiza mstari kama kulikata, nyingine kimechorwa kichwa kikubwa ukakatiza mstari kukikata, halafu kuna nyingine nimeona Dar kuna S hapa sijaziona, labda ni za tanzania tu.
Dah.... sikio lililokatwa maana yake Kuna kivuko Cha wasiosikia (viziwi ) barabara....kwenye S hautakiwi kusimamisha gari...[emoji2960]
 
Kuna kaudanganyifu kwenye kijani
Nahisi hicho kibao cha;
83 Km Morogoro
350 Km Iringa
Patakuwa Chalinze ambapo ni 83 Km kwenda Morogoro, nilitegemea kibao kiandikwe 383 Km
Screenshot_2019-09-25-17-09-37-1.png
mpaka Iringa kwakuwa kutoka Morogoro hadi Iringa ni 300 Km
 
Kaudanganyifu ka pili kamefanywa na TANROADS, kutoka lilipo bango la kuonyesha 300m mpaka kuifikia round about urefu ni meta 300 lakini bango lilipo pale limeandikwa meta 100, halafu lile la meta 300 lililotakiwa kuwa hapo limewekwa umbali wa meta 100 kutoka round about kuelekea Dodoma, yaeleka msimamizi wa TANROADS
Screenshot_2019-09-25-17-17-11-1.png
hakuwepo wakati wa jwekaji wa mabango hayo
 
kwenye hizo alama za kudhibiti mbona huwa naziona kwenye njia ya makutano hiyo ya Ruhusu na simama..

swali lingine, natakiwa kuacha umbali gan kat ya gari langu na gari jingine tukiwa barabara kuu

Naomba na ufafanuzi wa ile mistari ya njano na meupe barabarani ile mirefu na ile iliyokatikakatika vipande
Ni nusu ya Speed yako
  • 60 km/h = 30 m
  • 70 km/h = 35 m
  • 80 km/h = 40 m
  • 90 km/h = 45 m
  • 100 km/h = 50 m
  • 110 km/h = 55 m
  • 120 km/h = 60 m
  • 130 km/h = 65 m
 
Nimeona alama ya kichwa cha binadamu afu katikati kimechorwa mstari mwekundu! Alama hii nimeiona maeneo ya Mombo - Korogwe! Ni nini hicho?
Humaanisha walemavu wa akili, (Vichaa) madishi yao yameyumba
 
Back
Top Bottom