Zijue faida za kuoa single mothers

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
11,261
Reaction score
17,202
Watu wengi wamekua na kasumba ya kuwaponda single mothers kwamba hawafai kuoa na kutoa sababu kedekede sasa leo nakupa faida za kuoa single mothers.
1. Kashapevuka kiakili.
2.Atalea mtoto / watoto vizuri kwani ana uzoefu.
3..Anajua thamani ya kupendwa,kwani ashatendwa
4.Hatatamani kukupoteza kwani alishampoteza aliyempenda huko nyuma.
5.Atajitahidi asikukosee,ashajifunza kutokana na makosa ya nyuma
6.Akikukosea atakuomba msamaha,anajua thamani ya kuomba msamaha.
7.Ni wavumilivu.
8.Anathamini ile heshima ya kuitwa mrs fulani
9.Tayari una uhakika wa uzazi..sio mgumba.

Hizo ni baadhi tu ya faida lukuki za kuoa single mother..hivyo msiogope, hata Mungu ukimuomba msamaha anatoa nafasi ya pili, faida ni nyingi sana kuliko hasara😂

Credrit: Msouthherbs.
 
1. Kuna tofauti ya kupevuka na kuvurugwa na maisha hadi ukalazimika kukubaliana na hali yoyote itayokukuta na ukatakiwa kujishusha. Anapevuka binti anayevunja ungo, single mother anavurugwa na aliyezaa nae anakukubalia wewe na kuendana na masharti yako magumu kwasababu hana namna.

2. Single mother wengi sio walezi wazuri wa watoto. Labda kama umefanya reference ya akina mama wa miaka ya nyuma( kuanzia 1980 kurudi nyuma) ambao hii character ya single mothers haiwahusu sana maana haikuwa desturi yao. Ila hawa wa sasa ni breed ya tofauti inayoendeshwa na mtandaoni na life style ya uharibifu. Sasa ingia ujue haujui.

3. Thamani ya kupendwa huwa anae ifahamu ni yule mwenye history nzuri ya malezi tokea kwa wazazi. Masingle mother wengi wa sasa wanatokea familia za mama bila baba, au mama na baba wa hovyo yaani broken homes ambazo hazinaga misingi ya upendo. Hawajui thamani wala maana ya upendo. Akija kwa mwanaume anajinyenyekesha ili kupata hifadhi ila sio kwa mapenzi sababu wengi wanakuwa na trauma aidha za malezi waliyokulia au za mahusiano yaliyoharibika. Ni swala la muda akipata alichofuata umeisha. Kama unakataa jaribu ujionee.

4. Of course kama unampa anachotaka hatotaka kukupoteza but mind you, watoto wake wakishakomaa na kuanza maisha na yeye akajiwekea msingi then hapo hata ukiondoka hasituki. Kwakifupi wapo kimkakati na hili kwa waliowahi kukutana na visanga vya single mothers watakushuhudia wazi wazi kabisa kuwa ni kweli.

5. Kuhusu kujifunza nitakukatalia kwa asilimia 90. Mara nyingi huwa hawajifunzi. Wengi wanapoa kwa muda na kinachotokea ni yale matabia yake utashangaa yamehamia kwa watoto. Wengi huwa wanakuwa tayari ni damaged goods kutokea huko walipotoka. Ukiona mfupa fisi kaucha jua mbwa hatauweza. Ukiona aliyeanza nae amemshindwa wewe unayekwenda kupokea mpira utawezea wapi?

6. Kuomba msamaha haimaanishi mtu atabadilika. Sometimes ni tekiniki ya kukupunguza makali na kukuandaa kwa pigo au shambulizi jipya. Usijidanganye na machozi ya mamba na drama za kukuigizia mapenzi, hawa wadudu ni ma best actress wa mahusiano.

7. Neno kuvumilia linamaanisha ni kitendo cha kukaa sehemu pasipofaa. Mwanamke ambaye anavumilia sehemu ambapo anajua au kaona sio stahiki yake then jua ana lake jambo mwisho wa siku.

8. Angekuwa ana thamini ile heshima ya kuwa mrs fulan then angejitunza na kuwa makini sana kipindi cha usichana akiwa na 16 hadi 26 years. But kwa bahati mbaya wengi umri huo wanakuwa wanaruka sarakasi za usichana kisha wanakuja kushtukia hawana pa kushika hatimae kutelekezwa sababu ni wazi walitumika vibaya nani anataka kuoa demu aliyeliwa na masela.

9. Kama kigezo ni uzazi why uende kuanza na mwanamke aliyezaa hawa ambao hawajazaa hata mtoto m'moja na pengine ni bikra nao wafuate huo uzembe?

Kwa kifupi hakuna ulichoweza kuongea chenye tija kwa wanaume hapo cha zaidi umeongea mambo ambayo sidhani hata wewe binafsi umeshawahi shuhudia binafsi au kuona watu wakiyapata. Acha kuwa kilaza. Kama unapenda vya kunyonga vya kuchinja utaviweza wewe kweli? [emoji848]
 
Mkuu hizi kunguni ulizowasagia hapa sio za nchi hii..🙌
 
Never narudia tena never yaani usijaribu kuwaendea na theories hizi walahi utajuta speaking kutokana na experience single mom ambae at least utakaa bila mashaka sana ni yule ambae kafiwa tu na baba mtoto wake yaani (single-widow mom 😜) ila kama baba wa mtoto yupo hai usijichanganye kabisa ni bahati mno kutokuku kuta jambo wana visirani na gumbu na visasi juu..
 
Hapo namba 3 jidanganye tu,aliyempenda utamjua baada ya kuanza kuishi naye,huwa hawawezi kujizuia kuficha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…