Zijue faida za kuoa single mothers

Zijue faida za kuoa single mothers

6.Akikukosea atakuomba msamaha,anajua thamani ya kuomba msamaha.
Mke wangu mimi ni kamanda in chief kwenye hili suala. Yan ni mwamba!!.
Mpaka ukasikie neno "nisamehe" toka kinywan mwake, bas huwa naanza kupata mashaka sana na kujiuliza vitu vitu vingiiii.
Yule mama sijui hata kuokoka aliokokaje, maana kuomba msamaha niiii mbiiiiiiinde sio kitoto.
😂😂
 
Neno sahihi ni sio tasa badala ya neno Mgumba. Ugumba anaweza kuwa nao kwa sababu kama vile baada ya uzazi akapata pid sugu yaweza mletea ugumba.
 
Watu wengi wamekua na kasumba ya kuwaponda single mothers kwamba hawafai kuoa na kutoa sababu kedekede sasa leo nakupa faida za kuoa single mothers.
1. Kashapevuka kiakili.
2.Atalea mtoto / watoto vizuri kwani ana uzoefu.
3..Anajua thamani ya kupendwa,kwani ashatendwa
4.Hatatamani kukupoteza kwani alishampoteza aliyempenda huko nyuma.
5.Atajitahidi asikukosee,ashajifunza kutokana na makosa ya nyuma
6.Akikukosea atakuomba msamaha,anajua thamani ya kuomba msamaha.
7.Ni wavumilivu.
8.Anathamini ile heshima ya kuitwa mrs fulani
9.Tayari una uhakika wa uzazi..sio mgumba.

Hizo ni baadhi tu ya faida lukuki za kuoa single mother..hivyo msiogope, hata Mungu ukimuomba msamaha anatoa nafasi ya pili, faida ni nyingi sana kuliko hasara[emoji23]

Credrit: Msouthherbs.
Labda sio huyu niliyekuwa nimemuoa mimi.... Yaani mpaka najuta, sio wote wako hivyo, wengine ukianza kuishi nao unakuja kupata jibu la kwanini waliachika.... Wanazingua sana baadhi yao aisee
 
1. Kuna tofauti ya kupevuka na kuvurugwa na maisha hadi ukalazimika kukubaliana na hali yoyote itayokukuta na ukatakiwa kujishusha. Anapevuka binti anayevunja ungo, single mother anavurugwa na aliyezaa nae anakukubalia wewe na kuendana na masharti yako magumu kwasababu hana namna.

2. Single mother wengi sio walezi wazuri wa watoto. Labda kama umefanya reference ya akina mama wa miaka ya nyuma( kuanzia 1980 kurudi nyuma) ambao hii character ya single mothers haiwahusu sana maana haikuwa desturi yao. Ila hawa wa sasa ni breed ya tofauti inayoendeshwa na mtandaoni na life style ya uharibifu. Sasa ingia ujue haujui.

3. Thamani ya kupendwa huwa anae ifahamu ni yule mwenye history nzuri ya malezi tokea kwa wazazi. Masingle mother wengi wa sasa wanatokea familia za mama bila baba, au mama na baba wa hovyo yaani broken homes ambazo hazinaga misingi ya upendo. Hawajui thamani wala maana ya upendo. Akija kwa mwanaume anajinyenyekesha ili kupata hifadhi ila sio kwa mapenzi sababu wengi wanakuwa na trauma aidha za malezi waliyokulia au za mahusiano yaliyoharibika. Ni swala la muda akipata alichofuata umeisha. Kama unakataa jaribu ujionee.

4. Of course kama unampa anachotaka hatotaka kukupoteza but mind you, watoto wake wakishakomaa na kuanza maisha na yeye akajiwekea msingi then hapo hata ukiondoka hasituki. Kwakifupi wapo kimkakati na hili kwa waliowahi kukutana na visanga vya single mothers watakushuhudia wazi wazi kabisa kuwa ni kweli.

5. Kuhusu kujifunza nitakukatalia kwa asilimia 90. Mara nyingi huwa hawajifunzi. Wengi wanapoa kwa muda na kinachotokea ni yale matabia yake utashangaa yamehamia kwa watoto. Wengi huwa wanakuwa tayari ni damaged goods kutokea huko walipotoka. Ukiona mfupa fisi kaucha jua mbwa hatauweza. Ukiona aliyeanza nae amemshindwa wewe unayekwenda kupokea mpira utawezea wapi?

6. Kuomba msamaha haimaanishi mtu atabadilika. Sometimes ni tekiniki ya kukupunguza makali na kukuandaa kwa pigo au shambulizi jipya. Usijidanganye na machozi ya mamba na drama za kukuigizia mapenzi, hawa wadudu ni ma best actress wa mahusiano.

7. Neno kuvumilia linamaanisha ni kitendo cha kukaa sehemu pasipofaa. Mwanamke ambaye anavumilia sehemu ambapo anajua au kaona sio stahiki yake then jua ana lake jambo mwisho wa siku.

8. Angekuwa ana thamini ile heshima ya kuwa mrs fulan then angejitunza na kuwa makini sana kipindi cha usichana akiwa na 16 hadi 26 years. But kwa bahati mbaya wengi umri huo wanakuwa wanaruka sarakasi za usichana kisha wanakuja kushtukia hawana pa kushika hatimae kutelekezwa sababu ni wazi walitumika vibaya nani anataka kuoa demu aliyeliwa na masela.

9. Kama kigezo ni uzazi why uende kuanza na mwanamke aliyezaa hawa ambao hawajazaa hata mtoto m'moja na pengine ni bikra nao wafuate huo uzembe?

Kwa kifupi hakuna ulichoweza kuongea chenye tija kwa wanaume hapo cha zaidi umeongea mambo ambayo sidhani hata wewe binafsi umeshawahi shuhudia binafsi au kuona watu wakiyapata. Acha kuwa kilaza. Kama unapenda vya kunyonga vya kuchinja utaviweza wewe kweli? [emoji848]


Mkuu ulifanya utafiti KUHUSU hawa viumbe Mbona kama umewabana Sana 😁
 
Kuna mwanetu kitaa ishu ya ma single maza kaipeleka next level. Jamaa in his early 20s kaoa single maza ana watoto watano na kati ya hao watoto wawili wanashea baba mmoja, wawili baba zao hawajulikani na mmoja ni wa baba wa hivi karibuni ambae ndo kamtema akajaa kwa mwanetu. Mwanetu nae kamzalisha mtoto mmoja. Life ni riziki mguuni asipotoka hali. Nikimuangalia jamaa naona kabisa japo kutoboa sometimes ni mipango ya muumba ila nikimuangalia jamaa naona amepotea.

Jamani wahuni tulee damu zetu tuache kuzitelekeza haijalishi umekwazwa namna gani na mzazi mwenzio, mnawabebesha mizigo wanenu kitaa.
 
Watu wengi wamekua na kasumba ya kuwaponda single mothers kwamba hawafai kuoa na kutoa sababu kedekede sasa leo nakupa faida za kuoa single mothers.
1. Kashapevuka kiakili.
2.Atalea mtoto / watoto vizuri kwani ana uzoefu.
3..Anajua thamani ya kupendwa,kwani ashatendwa
4.Hatatamani kukupoteza kwani alishampoteza aliyempenda huko nyuma.
5.Atajitahidi asikukosee,ashajifunza kutokana na makosa ya nyuma
6.Akikukosea atakuomba msamaha,anajua thamani ya kuomba msamaha.
7.Ni wavumilivu.
8.Anathamini ile heshima ya kuitwa mrs fulani
9.Tayari una uhakika wa uzazi..sio mgumba.

Hizo ni baadhi tu ya faida lukuki za kuoa single mother..hivyo msiogope, hata Mungu ukimuomba msamaha anatoa nafasi ya pili, faida ni nyingi sana kuliko hasara😂

Credrit: Msouthherbs.
Hasara za kuoa single mothers
1: Uwezo mdogo katika kukusaidia kimaisha.
2: Kuna uwezekano aliyezaa nae ndiye aliyempenda na wewe amekukubali kwa sababu zake kama vile fedha, upole au upoyoyo ulio nao.
3: Mwenye thamani kwenye mahusiano yake wakati wote ni mtoto au watoto uliomkuta nae, hata hisia zake kwako zitategemea unavyowajali au kumjali mtoto wake.
4: Wengi kutoka nje ya mahusiano ni kama kumsukuma mlevi, wameshakufa ganzi kwenye eneo hilo.
5: Anaweza akalipiza maumivu yake ya mahusiano yake ya nyuma kwako ukatamani ardhi ifunguke uingie.
6: Ukikuta single mother ana mtoto wa kike, muogope kama ukoma.Ukimzingua tu anakupelekea kesi ya ngono kwa katoto kake, utakimbia na shati begani ukimwachia kila kitu kuogopa msala kwani kuthibitika kuwa anachosema ni uongo, utakuwa umekuwa kama chuma chakavu.
NB
Wanawake wana uwezo mkubwa wa kusoma hisia za wanaume hivyo ukichanganya na uzoefu alionao katika mahusiano, atakunyoa nywele kama Samsoni.
 
Back
Top Bottom