Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Zifuatazo ni hasara za matusi anazopata mtukanaji mwenyewe, na pia hasara anazowasababishia wale anaowatukana:
Hasara za Matusi Kiafya:
1. Kutukana kunaongeza viwango vya mfadhaiko wa akili, kiasi cha kusababisha magonjwa ya moyo na kushusha kinga ya mwili.
2. Matusi huamsha hasira na wasiwasi, na kupelekea ongezeko la shinikizo la damu.
3. Matukano yanaweza kusababisha huzuni na unyogovu kwa mtukanaji na anayetukanwa.
4. Wanaotukanwa wanaweza kushindwa kupata usingizi kwa sababu ya mawazo mazito na hivyo kusababisha magonjwa yatokanayo na kushindwa kulala.
5. Matusi huweza kuathiri mfumo wa neva. Mfadhaiko wa mara kwa mara unaotokana na matusi unaweza kudhoofisha utendaji kazi wa mfumo wa neva.
6. Matusi huweza kuongeza hatari ya magonjwa sugu. Mfadhaiko unaosababishwa na matusi unaweza kuchangia magonjwa kama kisukari na vidonda vya tumbo.
7. Matusi huchochea hasira. Matusi yanaweza kusababisha hisia za ghadhabu zinazodhuru afya ya mwili.
8. Watu wanaotukana mara nyingi wanakosa msaada wa kijamii, jambo linaloathiri ustawi wa hisia zao.
9. Watu wanaoathiriwa na matusi kuna wakati hujikuta wakijiumiza au kuwaza kujiua kwa sababu ya huzuni kubwa.
10. Matusi yanaweza kuchochea msongo wa mawazo unaoathiri mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Hasara za Matusi Kijamii
11. Matusi yanasababisha mahusiano mabovu katika jamii.
12. Watu wanaotukana hujipotezea heshima katika jamii.
13. Matusi yanaweza kusababisha mtu akanyanyapaliwa au kutengwa na jamii.
14. Katika familia, matusi husababisha ugomvi na uvunjifu wa umoja na mshikamano.
15. Matusi mara nyingi husababisha watukanaji kupoteza marafiki wa karibu.
16. Matusi huchochea watu kulipa kisasi na hivyo kusababisha migogoro mikubwa zaidi.
17. Mtu anayejulikana kuwa ana tabia ya kutukana anaweza kukosa msaada anapokuwa na uhitaji.
18. Matukano yanaweza kuchochea matendo ya ukatili, uuaji na vurugu.
19. Matusi mara nyingi husababisha kuvunjika kwa ndoa na kuchangia wana ndoa kupeana talaka.
20. Watu wanaotukana hujisababishia kutopendwa na jamii na hivyo wanajikuta wakiwa wapweke.
Hasara za Matusi Kiuchumi
21. Watukanaji huweza kupoteza kazi. Tabia ya kutukana mahali pa kazi inaweza kusababisha mtu kufukuzwa kazini.
22. Matusi kwa mfanyabiashara huweza kumfanya apoteze wateja. Biashara inaweza kupoteza wateja kutokana na lugha chafu za matusi kutoka kwa mmiliki wa biashara au wahudumu wake.
23. Matusi yanaweza kusababisha kazi kuzorota au kushusha ari ya uzalishaji.
24. Matusi huweza kusababisha watukanaji kushtakiwa kisheria kwa maneno yao ya chuki au dharau au kwa kuwavunjia wengine heshima.
25. Madhara ya kisaikolojia yanayohusiana na matusi yanaweza kumfanya mtukanaji au aliyetukanwa alipe gharama kubwa za kupata ushauri nasaha.
26. Wawekezaji wanaweza kukwepa kushirikiana na mtu au mfanyabiashara mwenye tabia ya matusi.
27. Matusi huleta migogoro ya kibiashara au uhasama kwa wadau wa biashara.
28. Matusi hupoteza bure muda wa kazi. Muda unaotumiwa na watukanaji ungeweza kutumika kuzalisha mali au kwa shughuli za kiuchumi.
29. Matusi huathiri sifa ya kampuni au shirika: Biashara au taasisi inayoendeshwa na watu wenye tabia ya matusi hupoteza sifa kwa wateja na washirika.
Hasara ya kiroho
30. Hii ni hasara kubwa kuliko zote. Mtukanaji asipotubu, hawezi kuingia mbinguni kwenye uzima wa milele. Katika kitabu cha 1 Wakorintho 6:9-10 imeandikwa hivi:
"Au hamjui ya kwamba wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wasenge, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."
Mpaka hapo tumeona wazi jinsi matusi yanavyoleta hasara kiafya, kijamii kiuchumi na kiroho. Jitenge na matusi. Tubu dhambi hiyo mapema na uombe Mungu akusamehe na umruhusu Yesu atawale maisha yako. Yesu atakupa neema ya kuishinda dhambi ya matusi na dhambi zote nyingine. Barikiwa!