Zijue MISSION 09 za KBG (FSB sasa) ambazo kama baadhi zingefanikiwa Dunia ingekuwa tofauti na leo

Zijue MISSION 09 za KBG (FSB sasa) ambazo kama baadhi zingefanikiwa Dunia ingekuwa tofauti na leo

kweli haya mambo mazito,ule ukorofi wa USA umepungua kwa sasa baada ya URUSI kujiimarisha zaidi kiulinzi ndani na nje ukichukulia mfano sakata la UKRAINE wamarekani na washirika wao kuufyata,pia lile sakata la kuharibu mfumo wa umeme kwenye manowari yao kwenye bahari nyeusi,kiukweli putin amenisisimua katika utawala wake
 
kweli haya mambo mazito,ule ukorofi wa USA umepungua kwa sasa baada ya URUSI kujiimarisha zaidi kiulinzi ndani na nje ukichukulia mfano sakata la UKRAINE wamarekani na washirika wao kuufyata,pia lile sakata la kuharibu mfumo wa umeme kwenye manowari yao kwenye bahari nyeusi,kiukweli putin amenisisimua katika utawala wake
Utawala wa Russia ni zaidi ya Puttin, Boris alochagua watu 4 ambao watatawala kwa muda mrefu, Puttin na Medvedev ni wawili kati yao, hao wengine wanafahamika na KGB/FSB, Puttin na Medvedev.
Watakuwa wana exchange mpaka......
 
Utawala wa Russia ni zaidi ya Puttin, Boris alochagua watu 4 ambao watatawala kwa muda mrefu, Puttin na Medvedev ni wawili kati yao, hao wengine wanafahamika na KGB/FSB, Puttin na Medvedev.
Watakuwa wana exchange mpaka......

Kuna documentary ya jinsi Vladimir Putin alivyoingia katika power inaitwa How Vladimir Putin came into Power, hii inaeleza mipango yote ilivyofanyika mpaka huyu jamaa anachukua nchi!
Kutoka kuwa Mkurugenzi Mkuu wa KGB/FSB mpaka kuwa Kiongozi wa Russia ni mipango ilifanywa.
 
Bora hao wanajitangaza bar Mbona hao FBI wanavaa kabisa vizibao vyao wala haihitaji mtu kwenda kusikiliza,japo kuna wasiovaa pia kama wale wa TISS nao wasio jitangaza.
FBI sio kitengo cha siri, tofauti na askari wengine ni kuwa wao hawavai sare za kiaskari, ila wanapokuwa katika operation mara nyingi wanakuwa na utambulisho fulani dhahiri kama fulana au jaketi zenye jina FBI, au vitambulisho vinavyo onekana, lakini wale wa vitengo vya siri hutawajua asilani
 
Kama ilivyo CIA, KGB (imekuwa FSB kuanzia 1995)shirika la kijasusi la USSR sasa URUSI limewahi kuhusika katika operation hatari sana maeneo mbalimbali Duniani. Kilele cha operation hizo ilikuwa kipindi cha vita baridi. Taarifa nyingi zilijulika pale jasusi la KGB Vasili Mitrokhin lilipotorokea uingereza na Mafaili yenye siri nyingi maana alikuwa ni mtunza kumbukumbu wa shirika hizo.

1:MASHAMBULIO KWA MIUNDOMBINU YA MAREKANI
Hungry-Horse-Dam.png

kUANZIA 1957 Hadi 72 KGB walianza kupiga picha miundombinu ya marekani kwa siri. Mitambo ya umeme,Mafuta chochote kile ambacho kingeleta athari za kudumu kwa mmarekani kilipigwa picha.Mipango yote ilikuwa ni kuahakikisha ikitokea vita, wanapiga shambulio moja amerika hasa new york inakoswa umeme, na kuanza kushambuliwa na russia mtaa kwa mtaa.

2: MIKAKATI HATARI YA KUOKOA MATEKA RAIA WA URUSI.

Hostage-Retribution.jpg

Mwaka 74 walinda kikosi maalumu kiitwacho ALPHA GROUP. KBG waliunda kikosi hiki kutekeleza mission za siri sana na Za kikatili kupita kiasi ili kuwaokoa mateka wao. Mfano ni huu wa LEBANON.
Magaidi waliwateka wanadiplomasia wanne wa kirusi siria. Lengo ni kuizuia russia isiiunge mkono siria.Baada ya maridhiano kufeli na magaidi kuonyesha wamemuua mmoja wa mateka, ndipo kikosi hiki kikaingilia kati, waliperereza na kujua kundi hilo ni hesbula. Wakamteka ndugu wa karibu na kiongozi mkuu wa hesbula. wakawa wanamkata vipande vidogo vidogo vya mwili wakivituma kwa kiongozi huyo vikiambatana na ujumbe.Baadae walimuua na wakamtumia kiongozi huyo ujumbe kuwa wanajua pote walipo ndugu na familia yake na kinachofuata ni kuwafanya wote kama huyo ndugu yao akiwemo na yeye aliyedhani hajulikani. Haraka sana magaidi waliwaachia hao mateka bila masharti yoyote.

3:KUTUMIA WANAWAKE WAREMBO KUREKODI VIDEO ZA NGONO ZA VIONGOZI
Blackmail-Stewardess.jpg

KGB ilijumuisha wanawake warembo waliowaita "SWALLOWS", USSR walikuwa na mpango wa kutawala dunia, Mshirika wao Indonesia alipopata nguvu walipata hofu atawaasi na kujikita na uislamu. Raisi wa nchi hiyo SURKANO ndio alikuwa kikwazo. Baada ya kumfuatilia waligundua anaudhaifu mkubwa katika NGONO. Walipanga SwALLOWS wa kutosha hotelini alipofikia na kwenye ndege kama wahudumu. Bila kujua wakamrekodi akiwa anafanya mapenzi na wadada hao kwa mpigo. Walipomtishia na kumtumia hizo clip ili awe mpole aendelee kuwaunga mkono, majibu yakawa tofauti maana hakushtushwa na aliomba wamtumie nyingine zaidi maana zile zilikuwa ni chache. Jaribio likafeli.

4:KBG HACKERS (WADUKUZI WA KIMTANDAO) WALITEMBELEA ZAIDI YA COMPUTER 400 ZA WANAJESHI WA MAREKANI
Old-Computer.jpg

mwAKA 80 Walikuwa wanatafuta jinsi ya kuPATA siri za jeshi la marekani. Walimuajiri jamaa anayeitwa Markus Hess mtaalamu aliyebobea katika anga hizo. Shughuli nzima ilifanyikia UJERUMANi ambapo aliweza kuACCESS computer zaidi ya mianne za jeshi la US. Akifanikiwa kubashiri PASSWORD za computer muhimu kabisa PENTAGON na kupata taarifa za siri za wanajeshi lukuki.
Hadi pale mtaalamu wa US Cliford stoll siku moja katika pitapita zake akaona vitu asivyovielewa kwenye system yao. ilimchukua miezi 10 kujua nini kilikuwa kinaendelea na huyo jamaa aligundua ana SUPPERACCESS ya Deffensive system ikiwemo mitambo ya nyuklia marekani. Hadi alipowekewa mtego wa kimtandao na kunaswa huko hannover ujerumani. alikuwa anawauzia KBG hizo siri.

5:OPERATION RYAN
Spying-on-the-US.jpg

Miaka ya 80, ulizuka uvumi kuwa US wanajiandaa kuilipua russia muda wowote na makombora ya NYUKLIA. Ndio KGB na urusi wakaja na hii operation ambayo ni kubwa kuwahi kutokea.
Walipanga kuweka satelite zitakazopiga picha vituo vya kijeshi marekani nzima kila sekunde kuona kama kuna kombola linakuja,Pia kumonitor matumizi ya RADA amerika yote ili kuangalia uwezekano wa shambulio. Pia kuwachunguza raia na wanajeshi wa marekani wote wanapoondoka US, PIa kuiweka NATO chini ya uachunguzi wa hali ya juu. Walijaribu kuingilia mawasiliano ya simu yote nchini marekani na ulaya yote. Waliweka mtandao wa MAKACHERO duniani ambao wako tayari muda wote kushambulia wakiona urusi inavamiwa na marekani. Operation hii ya mabilioni ilihairishwa miaka mitatu baadae.

6:KUNUNUA BENKI ZA WAMAREKANI
6-us-bancorp.jpg

KBG hawakupanga kutumia mashushu wao kujua siri za selikali ya malekani, Badala yake walitumia BENKI.Wlipanga kununua BENKI TATU huko Northern California. Hawakukurupuka walijua benk hizi zilitumika na makampuni yaliyokuwa yanatengeneza TECHNOLOGY za jeshi la US, Wakaona kumiliki hizo benki watapata taarifa za siri za nini wanafanya jeshini kwa maana ya teknolojia.CIA walishtukia huu mchakato baada ya kugundua Mnunuzi kutoka Singapole aliingiziwa pesa kutoka RUSSIA.

7:OPERATION PANDORA
Watts-Riots.png

Waliendelea kuiandama marekani maana ndio alikuwa adui yao namba moja. Safari hii KBG wanapanga machafuko ndani ya US. Unakumbuka miaka ya 60 kulikuwa na vuguvugu la watu kupinga ubaguzi, kwa KGB hii ilikuwa ni fursa. Waliandaa vipeperushi NEW YORK na majarida feki yaliyoonyesha watu weusi wanawavamia wenye asili ya WAYAHUDI na kuwaibia vitu. Majarida haya yalionyesha kuwa walalamikaji ni kundi la waisrael JEWISH DEFENCE LEAGUE ambao kwa FBI walihesabiwa kama magaidi. Kisha wakayasmbaza kwa watu weusi waliokuwa wanamiliki silaa na mapolisi/wanajeshi weusi uchochezi huu wajiandae na mashambulizi ya wayahudi. Kuzidi kuchochea KGB walipanga kukilipua chuo kilichojaa wanafunzi weusi tu. Baada ya kulipuka chuo watume ujumbe kwa vyama vyote vya watu weusi kuwa ni WAYAHUDI ndio wanahusika.

8:SAKAFU YA KUSIKILIZIA
Hotel-Viru.png

KBG walikuwa wako vizuri sana ktk kuweka vinasa sauti kusikiliza mazungumzo katika maofisi na majengo mengi. Yaani waliwahi kuweka vinasa sauti katika hoteli maarufu kwa zaidi ya miaka 20 bia kujulikana. Mfano nchini ESTONIA jengo lenye ghorofa 22 lililokuwa linafikiwa na wafanya biashara wakubwa duniani, kulikuwa na floor ya 23 ya siri iliyokaliwa na KGB kwa muda wa miaka 20 hadi USSR ilipoanguka mwaka 1991. Mtoto mdogo aliyempa barozi wa Marekani Russia zawadi ambayo ilipachikwa kinasa sauti chenye uwezo wa hali ya juu. Kwa miaka saba KGB walikuwa wanasikiliza mawasiliano yote hadi kilipo gunduliwa ka bahati mbaya na mfanyakazi wa radio wa UK alipokosea mawimbi na kusikia mazungumzo asiyoyaelewa.

9:KUFADHILI UGAIDI
Terrorists.jpg

Jasusi la KGB Aleksandr Sakharovsky anajinasibu kuwa "Utekaji wa ndege ni UVUMBUZI WAKE".
Waliungana na YASSER Alafat na kumsaidia kuchukua madalaka ya PARESTINA. Walitengeneza magaidi wa kutosha na wapigania uhuru ili kuwadhoofisha maaduia wao. Mfano mwaka 69 tu ndege zaidi ya 82 zilitekwa sehemu mbalimbali duniani na hawa jamaa. Walichochea vita huko IRELAND kwa kuwasambazia Bunduki,bastola, mabomu wanajeshi kitu kilicholeta machafuko makubwa. Lengo lao lilikuwa ni kutengeneza mataifa mengi yenye kuunga mkono ukomunisti.


DUNIA INA MAMBO MENGI,
HII NI TAASISI MOJA TU LAKINI UKISOMA KUHUSU CIA(US), MOSSAD(UZAYUNI), MI6(UK), ISI (PAKISTANI),BND(ujerumani), RAW(INDIA), DGSE (UFARANSA),ASIS(AUSTRALIA) NA MSS(CHINA) UTAJUA GHARAMA YA KUILINDA NA KUITANGAZA NCHI KATIKATI YA MAADUI BILA VITA.
Nimesoma story yooote lakini ulipofika mwisho ndo umeharibu...hasa hapo kwenye magaidi na kuihusisha PALESTINE...
Rekebisha mwisho wa story yako
 
Nimesoma story yooote lakini ulipofika mwisho ndo umeharibu...hasa hapo kwenye magaidi na kuihusisha PALESTINE...
Rekebisha mwisho wa story yako
hujaeleweka, toa fact utaeleweka.
 
umetofautiana na habari bila kutoa maelezo ya kutosha kwa nini hukubali,
Mimi sikubali Waarabu kuitwa magaidi..na nitapinga mpaka keaho kutwa. Kwasababu gaidi halisi amevaa suti na kuuaminisha ulimwengu kwamba yeye ni mtu safi
 
Mimi sikubali Waarabu kuitwa magaidi..na nitapinga mpaka keaho kutwa. Kwasababu gaidi halisi amevaa suti na kuuaminisha ulimwengu kwamba yeye ni mtu safi
ookay, hiyo ni wewe, kila mtu huwa yuko sawa ila sio lazima iwe sahihi. ila gaidi hana uhusiano wowote na rangi au kabila.
ila humu ameongelewa gaidi wa parestina. inawezekana akawepo gaidi mweusi mzungu mchina hata muhindi pia mkuu.
 
Utawala wa Russia ni zaidi ya Puttin, Boris alochagua watu 4 ambao watatawala kwa muda mrefu, Puttin na Medvedev ni wawili kati yao, hao wengine wanafahamika na KGB/FSB, Puttin na Medvedev.
Watakuwa wana exchange mpaka......
 
basi utawala wa putin imekua nyundo kwa USA ule ukorofi/uchanganishi(rejea vita afganstan na libya)kwa syria wamebanwa na mrusi pia ndege aina ya @SU-24 ni pigo baya kwa marekani nadhan wataufyata
 
Ujasusi wa kijinga sana huu. Ndio maana USSR ilianguka. Tia maji tia maji kama hizi haziwezi wafanya superpower wa dunia! Katika ujasusi oparesheni ikifeli inaonyesha ubomu wa oparesheni hiyi. Hamjui tuu gharama ya damu kwa jasusi au majasusu wanaopewa misheni na ikafeli. Sheria za uendeshaji wa misheni za kijasusi zinapofeli ni kuwa tunawapoteza wote na vyote vilivyohusika.
 
Back
Top Bottom