Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Je plate namba Kama ya hii ni ya nani
RC
DSM?
 
1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara.


2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi.


3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo:

(a) SU - shirika la umma , mfano vyuo vikuu vya serikali

(b) SM - Serikali za Mitaa , mfano ni halmashauri

(c) STK,STL,STJ - serikali, mfano ni wizara


4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limetolewa kwa ajili ya matumizi ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili kutoka nje ya nchi.


5. Kibao chenye rangi ya bluu na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO).


6. Kibao chenye rangi ya kijani na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na ofisi za ubalozi wa nchi fulani. Mfano ubalozi wa Ufaransa.


7. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Polisi. Namba hizi huwa na herufi PT


8. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Wananchi (JW). Namba hizi huwa na herufi JW.


9. Kibao chenye rangi ya kijani na namba zenye herufi MT

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Magereza.

bb2d322a442f7f5681399ad0145f3e00.jpg

Shukrani sana mkuu kwa ufafanuzi kuna gari moja nimeliona juzi kati mitaa ya Africana lina kibao chenye rangi nyeupe na maandishi mekundu kama gari za miradi hiyo ina maanisha nini?
 
J (then namba)=judge (majaji wamewekwa kwa rank)
JR (then namba)=Jaji ya mahakama ya rufaa

Kuna taasis nyeti zinatumia namba binafsi wakati mwingne na vioo vya rangi nyeusi

Mfano: Takukuru, usalama wa taifa n.k
 
Busara ni kitu cha bure kiongoz, sijamtusi mtu hapa kama ulikerwa na nlichopost ungekaa kimya may b wengine watapata ufahamu..

Tuwe wabunifu kwenye mambo ya msingi na si kuonyesha ubunifu na umahiri kwenye kutukana,

PONGERA
 
CGI-Commissioner General Immigration

IGP-inspector General Police

CDF- Chief of Defence Forces

CGF- Commissioner General Fire

CGP- Commissioner General Prisons

CS- Chief Secretary

CAG- Comptroller and Auditor General

AG-Arttoney General

S-Speaker

N S-Naibu Speaker

KUB-Kiongoz wa Upinzani Bungeni

Mchango wangu ni huo mwenye swali la ufahamu anaweza uliza
J-Judge
RC-Regional Commissioner
 
Na kibao cha kushtukiza ukirudi nyumbani jioni inamaana umesaliti
 
Kibao Cha platinumz ujue ni gari ya Simba mnyama wa tandale
 
Back
Top Bottom