Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Mada nzuri ila waliotoa maana ya RAC 3847 kwamba ni Railway Asset Corporation ni kudanganya wengine hizi ni plate number za Rwanda
 
CGI-Commissioner General Immigration

IGP-inspector General Police

CDF- Chief of Defence Forces

CGF- Commissioner General Fire

CGP- Commissioner General Prisons

CS- Chief Secretary

CAG- Comptroller and Auditor General

AG-Arttoney General

S-Speaker

N S-Naibu Speaker

KUB-Kiongoz wa Upinzani Bungeni

Mchango wangu ni huo mwenye swali la ufahamu anaweza uliza
Acha uongo lini umeona gari la mkuu wa majeshi limeandikwa CDF??
 
Mada nzuri ila waliotoa maana ya RAC 3847 kwamba ni Railway Asset Corporation ni kudanganya wengine hizi ni plate number za Rwanda
Zinaweza kuwa zinafanana na rwanda lakini hawajakosea hizo namba za railway toka zamani sana. Ukichunhuza utaona pia zina bendera ya Tanzania za Rwanda zitakuwa na bendera ya Twanda
 
Ukiona mtaani gari zimeandikwa ktk plate number kama ifuatavyo usiumize kichwa jua ni hivi:

1. Ngao-Rais, makamu wa rais na waziri mkuu

2. S-Spika wa bunge

3. JM- Jaji mkuu

4. JR- Jaji wa mahakama ya rufaa

5. JK- Jaji Kiongozi

6. J- Jaji wa mahakama kuu

7. XXXX-Mkuu wa majeshi(CDF)

8. CAG-Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

9. CS- Katibu mkuu kiongozi

10. W mwanzoni inaashiria waziri kisha kifupi cha wizara yake hufuata

11. NW-Naibu waziri

12. DFP-Donor's Fund project

13. ST-Serikali ya Tanzania kisha herufi nyingine hufuata

14. SMZ-Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

15. PT-Police of Tanzania

16. SM-Serikali za mitaa

17. CD- Magari ya ubalozini

18. SU-Shirika la umma.

19. gari za jeshi pia zina namba zake ambazo zina vifupi vya JW

20. MT-Magereza Tanzania

21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)

22. Gari nyingine za umma zina namba zaidi ya moja kwa kazi maalum

NYONGEZA:
Gari za biashara zina plate number nyeupe na zile za matumizi binafsi plate number ya njano.

*mwenye nyongeza au masahihisho au vyote, aingie ulingoni tutoane ushamba, tuelimishane tusije tukatumia muda mrefu kuyashangaa magari yenye namba hizo mpaka tupate ajali. ....

Karibuni
Hapo namba 7 sio xxxx ni nyota ****
 
Ukiona mtaani gari zimeandikwa ktk plate number kama ifuatavyo usiumize kichwa jua ni hivi:

1. Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
Namba za magari yanayitumika kumbeba Rais au Makamu wa Rais na Waziri Mkuu haziandikwi namba wale herufi katika kibao chake, bali huwa na nembo ya taifa ya Bwana na Bibi. Kwa Kiingereza magari haya hufahamika kama State Cars,

2. Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
Spika wa Bunge pia gari lake huwa halina namba kwenye kibao chake bali huwa na herufi S pekee. Gari la Naibu Spika nalo huwa na herufi NS pekee

3. Jaji Mkuu wa Tanzania
Gari la Jaji Mkuu wa Tanzania huwa na herufi JM kwenye kibao chake

4. JR- Jaji wa Mahakama ya Rufaa

5. JK- Jaji Kiongozi

6. J- Jaji wa Mahakama Kuu

7. Mkuu wa Majeshi (CDF)
Gari la Mkuu wa Majeshi wa Tanzania katika kibao chake huwa hakuna namba wala herufi zozote bali kunakuwepo na Nyota nne kwenye kibao cha gari lake

8. CAG - Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

9. CS- Katibu mkuu kiongozi

10. Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
Magari ya Waziri na Manaibu wao huwa na herufi zinazoonyesha cheo (kama ni waziri au Naibu waziri) halafu hufuatia ana vifupisho vya majina ya Wizara zao. Gari la Waziri huwa na herufi W ikifuatia na kifupisho cha jina la Wizara yake. Gari la Naibu waziri huwa na herufi NW ikifuatiwa na kifupisho cha jina la Wizara yake

View attachment 668115 View attachment 668114

12. DFP-Donor's Fund project

13. ST-Serikali ya Tanzania kisha herufi nyingine hufuata

14. SMZ-Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

15. PT-Police of Tanzania

16. SM-Serikali za mitaa

17. CD- Magari ya ubalozini

18. SU-Shirika la umma.

19. gari za jeshi pia zina namba zake ambazo zina vifupi vya JW

20. MT-Magereza Tanzania

21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)

22. Gari nyingine za umma zina namba zaidi ya moja kwa kazi maalum

NYONGEZA:
Gari za biashara zina plate number nyeupe na zile za matumizi binafsi plate number ya njano.

*mwenye nyongeza au masahihisho au vyote, aingie ulingoni tutoane ushamba, tuelimishane tusije tukatumia muda mrefu kuyashangaa magari yenye namba hizo mpaka tupate ajali. ....

Karibuni
FB_IMG_1462613552012.jpg
 
Umesahau ukiona gari limeandikwa "gwanko"nalo pia la ujue ni la mwanachama wa jamiiforum
 
Namba za Mawaziri zinachanganya sana. Tafadhali mtoa hoja ingekuwa vema ukatuwekea vile vifupisho vya Namaba za Magari ya Mawaziri na Manaibu wao. Vile vifupisho vyake ni taabu sana kuving'amua kwa harakaharaka.
Kwa kipindi hiki imekua taab maana Wizara nyingi zimeunganishwa na kuwa moja mkuu
 
Back
Top Bottom