Kilemakyaaro
JF-Expert Member
- Jul 19, 2016
- 5,051
- 5,104
Ahsante kwa elimu nisaidie kutofautisha kati ya STK, STL
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizo zenye E mkuu zinamaanisha Escort na hutumika kwenye misafara ya wakubwakuna zile gari za usalama za ikulu huwa zimeandikwa "E" sijui inamaanisha nini na pia kuna gari za ikulu zimeandikwa "J" , kwa anae faham atujuze
Mkuu mimi magari ya balozi ambayo nayajua ni Marekani wanaotumia 116 na Uingereza wanaotumia 115 balozi nyingine huwa ni changamoto kwelikweliUFAFANUZI:
1. gari za ikulu zikiandikwa E zinamaanisha Escort. ni xile za kusindikiza misafara ya viongozi
2. tutambue kinachozungumzwa hapa sio vifupi vyovyote vya viongozi bali vifupi kwenye namba za gari. kumbe aliyesema DC(mkuu wa wilaya) nadhani hii haipo kwenye namba za gari.
3. RC-mkuu wa mkoa. hii kweli ipo. ila RPC kwenye magari cjaiona kwangu itakuwa ni elimu mpya. asante kwa uliyetujuza.
4. kweli gari za TISS kwa maadili na mazingira yao hazipaswi kuwa na namba maalumu iki zisiharibu kazi.
5.Polisi pia ktk idara ya upelelezi wanaweza wasitumie PT ili kufanikisha kazi za kiintelijensia
6. gari za kibalozi ukiacha ile CD, kuna namba maalum wamepewa kila ubalozi kiac kwamba gari yoyote ya ubalozi ikipita wapo wanaojua ni ubalozi gani. naomba anayejua atujuze.
Mkuu hapo kwenye Uingereza kaangalie tena nafikiri wao ni 115Plate namba za ubaloz zinajulikana kwa namba ya kuanzia ili ijulikane kuwa ni ubaloz gani kwa mfani
T116CD....... Ni marekani
T68CD.........Ni korea
T254CD.......Uingereza
Wengine wanaweza endelea hapo..
Nitumie namba yako nikupongezeNiliwahi kujichomeka nikapanda magar ya msafara wa wazir mkuu wakati wa pinda hakuna aliyenishtukia, maana nilikuwa smart sana
UT usalama wa taifa
Uhamiaji Tanzania- magari yanayomilikiwa na idara ya uhamiaji Tanzania
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]PT=Popoma Tanzania
Uhamiaji TanzaniaUT usalama wa taifa
Mbona sikuizi sizioni zile STGTUJIFUNZE KIDOGO MAANA YA PLATE NAMBA NA RANGI ZAKE(NAJUA WENGI WETU MAGARI HATUNA LKN TUJIFUNZE IVYOIVYO)
1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara.
2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi.
3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo:
(a) SU - shirika la umma , mfano vyuo vikuu vya serikali
(b) SM - Serikali za Mitaa , mfano ni halmashauri
(c) STK,STL,STJ - serikali, mfano ni wizara
4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limetolewa kwa ajili ya matumizi ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili kutoka nje ya nchi.
5. Kibao chenye rangi ya bluu na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO).
6. Kibao chenye rangi ya kijani na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na ofisi za ubalozi wa nchi fulani. Mfano ubalozi wa Ufaransa.
7. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Polisi. Namba hizi huwa na herufi PT
8. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya nyeupe
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Wananchi (JW). Namba hizi huwa na herufi JW.
9. Kibao chenye rangi ya kijani na namba zenye herufi MT
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Magereza...
Hamnamagari mnajadili haya wenyemagariyao watajadili nn