Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

kuna zile gari za usalama za ikulu huwa zimeandikwa "E" sijui inamaanisha nini na pia kuna gari za ikulu zimeandikwa "J" , kwa anae faham atujuze
Hizo zenye E mkuu zinamaanisha Escort na hutumika kwenye misafara ya wakubwa
 
UFAFANUZI:
1. gari za ikulu zikiandikwa E zinamaanisha Escort. ni xile za kusindikiza misafara ya viongozi
2. tutambue kinachozungumzwa hapa sio vifupi vyovyote vya viongozi bali vifupi kwenye namba za gari. kumbe aliyesema DC(mkuu wa wilaya) nadhani hii haipo kwenye namba za gari.
3. RC-mkuu wa mkoa. hii kweli ipo. ila RPC kwenye magari cjaiona kwangu itakuwa ni elimu mpya. asante kwa uliyetujuza.
4. kweli gari za TISS kwa maadili na mazingira yao hazipaswi kuwa na namba maalumu iki zisiharibu kazi.
5.Polisi pia ktk idara ya upelelezi wanaweza wasitumie PT ili kufanikisha kazi za kiintelijensia
6. gari za kibalozi ukiacha ile CD, kuna namba maalum wamepewa kila ubalozi kiac kwamba gari yoyote ya ubalozi ikipita wapo wanaojua ni ubalozi gani. naomba anayejua atujuze.
Mkuu mimi magari ya balozi ambayo nayajua ni Marekani wanaotumia 116 na Uingereza wanaotumia 115 balozi nyingine huwa ni changamoto kwelikweli
 
Kuna namba pia huwa za kijani na huandikwa EAC hizi ni za wabunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki lkn nafikiri hata watumishi wake huwa na namba hizo
 
Plate namba za ubaloz zinajulikana kwa namba ya kuanzia ili ijulikane kuwa ni ubaloz gani kwa mfani
T116CD....... Ni marekani
T68CD.........Ni korea
T254CD.......Uingereza

Wengine wanaweza endelea hapo..
Mkuu hapo kwenye Uingereza kaangalie tena nafikiri wao ni 115
 
Kuna gari ina CNA hii inasimama badala ya nini
 
TUJIFUNZE KIDOGO MAANA YA PLATE NAMBA NA RANGI ZAKE(NAJUA WENGI WETU MAGARI HATUNA LKN TUJIFUNZE IVYOIVYO)

1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara.

2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi.

3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo:

(a) SU - shirika la umma , mfano vyuo vikuu vya serikali

(b) SM - Serikali za Mitaa , mfano ni halmashauri

(c) STK,STL,STJ - serikali, mfano ni wizara

4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limetolewa kwa ajili ya matumizi ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili kutoka nje ya nchi.

5. Kibao chenye rangi ya bluu na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO).

6. Kibao chenye rangi ya kijani na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na ofisi za ubalozi wa nchi fulani. Mfano ubalozi wa Ufaransa.

7. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Polisi. Namba hizi huwa na herufi PT

8. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya nyeupe

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Wananchi (JW). Namba hizi huwa na herufi JW.

9. Kibao chenye rangi ya kijani na namba zenye herufi MT

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Magereza...
 
Vipi kuhusu zile plate namba zenye majina ya watu binafsi
Kama

Mzee mkavu
Chief
Diamond
Dr mwaka ?
 
Hamnamagari mnajadili haya wenyemagariyao watajadili nn
 
Mbona sikuizi sizioni zile STG
 
Mkuu mbona umewajumuisha wakati aliyeleta uzi ni mmoja tu, tena hajafanya majadiliano ameleta tu taarifa na kusepa Ingawa ipo tu humu muda mrefu. Tukiachana na hayo hii style yako ya uandishi ni unpingikable
Hamnamagari mnajadili haya wenyemagariyao watajadili nn
 
Eli24 OP mbona umewaonjesha tu kuhusu hii elimu ya plate number.Plate number zote zina vifupi tu ya herufi, Hujaeleza T, STK, MT, SM, PT, JW nk zinasimama badala ya maneno gani kwa kirefu.Hujaeleza pia plate number zenye RC, J, JM, WE au WA, zingine zina ngao ya taifa zina maanisha nini? Pia hujasema kwa mfano gari inaanzia na herfu T 420 halafu tena BOL chini yake.Hii 420 ni kitu gani na BOL chini yake ni herufi zinazosimama badala ya nini.Halafu je kama gari inatafutwa imefanya uhalifu na zikajulikana namba za juu tu kama T 420 bila ya herufi za chini inatosha kuibaini gari husika na namba hizo tu?
 
Back
Top Bottom