Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Mkuu mbona umewajumuisha wakati aliyeleta uzi ni mmoja tu, tena hajafanya majadiliano ameleta tu taarifa na kusepa Ingawa ipo tu humu muda mrefu. Tukiachana na hayo hii style yako ya uandishi ni unpingikable
Pdidy, mbona unaandika kama cherehani? Ndugu yangu kuandika bado hujajua tu ni bora kuacha hiyo kazi au kasome tu.
 
Additionally Gari ya Rais ina Ngao, Ya mkuu wa majeshi plate number yake ni nyota nne, Chief of secretary ikulu ni CS, Wakuu wa mikoa ni RC ikifatiwa na province lake, J ni jaji, S ni speaker ila pia mawaziri na manaibu waziri they have special plate number pia
 
STK serikali ya Tanzania hio K ni mwendelezo tu wa herufi kuna STK, STG
PT ni polisi Tanzania
MT magereza Tanzania
DFPA Donor fund project Africa
SM serikali za mitaa
 
STK serikali ya Tanzania hio K ni mwendelezo tu wa herufi kuna STK, STG
PT ni polisi Tanzania
MT magereza Tanzania
DFPA Donor fund project Africa
SM serikali za mitaa
Kassina,naomba niendelee kufafanua kuwa hizi namba za Serikali pamoja na.taasisi zake ikiwa pamoja na majeshi zinatokana au zimeanzishwa kuwa kufuata mpango maalumu wa kuhifadhi kumbukumbu ya mali za Serikali unaofahamika kitaalamu kama (code au.coding).Hivyo,ST ni Serikali ya Tanzania,na ilianza STA,STB,STC,STD,STE,STF,STG,STH,STG....H,J,K na.sasa ni.L.Sambamba na magari ya jeshi utaona 709JW18,maana yake ni kwa hiko ni gari la 709linalomilikiwa na.Jeshi la.Wananchi kwa mwaka huo wa.2018.Kwenye hii RAC 345 ni kwamba mamlaka ya miliki reli nchini ina sajili mali zake.pamoja na magari na RA ni Railways Administration nao walianza RAA,RAB,RAC.Utaratibu kwa kusajili magari pia hutumika kutambua mali za serikali na kuweka kumbukumbu kwenye.sii tuu magari,bali pia kwenye mali(assets) kama majengo,samahi pamoja na vifaa mbali mbali.Asante
 
Habari wakuu natumai mko poa na wiki ndo kwaanza iko kati...ninyooshe kwenye mada,nimekua nikipishana na magari ya serikali yenye plate namba mfano STK,SU n.k lakini sifahamu kirefu chake ni nini..Tafadhari kama unafahamu tujuzane.


NB:samahani nilikosea jukwaa na sijui jinsi ya kuediti kwenda jukwaa husika.
 
Habari wakuu natumai mko poa na wiki ndo kwaanza iko kati...ninyooshe kwenye mada,nimekua nikipishana na magari ya serikali yenye plate namba mfano STK,SU n.k lakini sifahamu kirefu chake ni nini..Tafadhari kama unafahamu tujuzane.


NB:samahani nilikosea jukwaa na sijui jinsi ya kuediti kwenda jukwaa husika.
MT = Magereza Tanzania
PT = police Tanzania
SU = Shirika la Umma
SM = serikali za Mitaa
UT= uhamiaji Tanzania
RC = Regional commisioner
DFP= Doner Fund project
JW = Jeshi la wananchi
CD = magari ya ubalozi
J= magari ya majaji
SMZ = serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
W= mawaziri
NW = Naibu waziri
CS = katibu mkuu kiongozi
CAG= mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

Na mengine mengi tuu.
 
MT = Magereza Tanzania
PT = police Tanzania
SU = Shirika la Umma
SM = serikali za Mitaa
UT= uhamiaji Tanzania
RC = Regional commisioner
DFP= Doner Fund project
JW = Jeshi la wananchi
CD = magari ya ubalozi
J= magari ya majaji
SMZ = serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
W= mawaziri
NW = Naibu waziri
CS = katibu mkuu kiongozi
CAG= mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

Na mengine mengi tuu.
Gari ya waziri mkuu, makamu wa rais na rais zinakuwaje?
 
MT = Magereza Tanzania
PT = police Tanzania
SU = Shirika la Umma
SM = serikali za Mitaa
UT= uhamiaji Tanzania
RC = Regional commisioner
DFP= Doner Fund project
JW = Jeshi la wananchi
CD = magari ya ubalozi
J= magari ya majaji
SMZ = serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
W= mawaziri
NW = Naibu waziri
CS = katibu mkuu kiongozi
CAG= mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

Na mengine mengi tuu.
IGP=Inspector General of Police (Mkuu wa polisi)
 
Habari wakuu natumai mko poa na wiki ndo kwaanza iko kati...ninyooshe kwenye mada,nimekua nikipishana na magari ya serikali yenye plate namba mfano STK,SU n.k lakini sifahamu kirefu chake ni nini..Tafadhari kama unafahamu tujuzane.


NB:samahani nilikosea jukwaa na sijui jinsi ya kuediti kwenda jukwaa husika.

Ingia huu uzi.

ZIJUE NAMBA ZA MAGARI YA TANZANIA PAMOJA NA NAMBA MAALUM ZA MAGARI YA VIONGOZI WA SERIKALI NA TAASISI ZA UMMA.



Ukiona mtaani gari zimeandikwa ktk plate number kama ifuatavyo usiumize kichwa jua ni hivi:

1. Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
Namba za magari yanayitumika kumbeba Rais au Makamu wa Rais na Waziri Mkuu haziandikwi namba wale herufi katika kibao chake, bali huwa na nembo ya taifa ya Bwana na Bibi. Kwa Kiingereza magari haya hufahamika kama State Cars,


2. Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
Spika wa Bunge pia gari lake huwa halina namba kwenye kibao chake bali huwa na herufi S pekee. Gari la Naibu Spika nalo huwa na herufi NS pekee. Maana ya herufi S ni Spika na NS ni Naibu Spika


3. Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatumia gari ambalo lina kibandiko chenye herufi CS pekee. Ikiwa maana ya CS ni Chief secretary


4. Jaji Mkuu wa Tanzania

Gari la Jaji Mkuu wa Tanzania huwa na herufi JM kwenye kibao chake


5. Mkuu wa Majeshi (CDF)
Gari la Mkuu wa Majeshi wa Tanzania katika kibao chake huwa hakuna namba wala herufi zozote bali kunakuwepo na Nyota nne kwenye kibao cha gari lake


6. Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
Magari ya Waziri na Manaibu wao huwa na herufi zinazoonyesha cheo (kama ni waziri au Naibu waziri) halafu hufuatia ana vifupisho vya majina ya Wizara zao. Gari la Waziri huwa na herufi W ikifuatia na kifupisho cha jina la Wizara yake. Gari la Naibu waziri huwa na herufi NW ikifuatiwa na kifupisho cha jina la Wizara yake


7. Gari za Serikali za Mitaa
Magari ya Serikali za Mitaa, yanayotumiwa kwenye Serikali hizo. Magari hayo kuwa na kibao chenye Herufi SM zikifuatiwa na namba tofauti tofauti.


8. Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO). Kibao chenye namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na herufi CD kisha namba tena.


9. Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania

Magari ya Ubalozi nchini Tanzania huanziwa na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD kisha namba. Pia namba hizi hutumiwa na wafanyakazi wa ubalozi husika hata kama ni watanzania. Mfano wa Ubalozi ni Marekani


10. Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
Magari yanayotumiwa na mashirika ya Umma huwa na kibao (Plate Number) ambazo huanziwa na herufi SU na kufuatiwa na namba tofauti tofauti kwenye vibao hivyo


11. Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu to nje ya nchi
Magari yanayotumika kwenye miradi inayofadhiliwa kutoka nje ya nchi kuwa na kibao chenye herufi DFP (Donor's Fund Project) ikifuatiwa na namba tofauti tofauti. Pia tofauti na DFP utakuta mengine yana DFPA


12. Magari ya Police wa Tanzania

Magari ya Polisi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi PT (Polisi of Tanzania) halafu hufuatiwa na namba tofauti tofauti mbele yake


13. Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania
Magari ya Jeshi la Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na namba kadhaa kisha hufuatiwa na herufi JW kisha hufuatiwa na namba tena.


14. Magereza Tanzania
Magari ya Magereza ya Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi MT kisha hufuatiwa na namba kadhaa mbele yake kwenye kibao cha magari hayo


15. Serikali ya Tanzania
Serikali ya Tanzania ina gari zake tofauti tofauti ambzo hutumika kwa mfano Wilayani au hata kwenye halmashauri. Magari haya huwa na kibandiko chenye Herufi za mwanzo STK au STJ au STL na baada ya hapo hufuatiwa na namba kadhaa mbele

16. Magari ya Wakuu wa Mikoa
Wakuu wa mikoa wote nchi huwa na magari ambayo huwana plate number ka tofauti. Gari la mkuu wa mkoa huwa na kibandiko ambacho kuanza na herufi RC na kisha hufuatiwa na herufi ambazo ni kifupi cha mkoa wake. Herufi RC humaanisha Regional Commisioner. Mfano; RC NJB- Mkuu wa Mkoa Njombe

3581ab2af279f4e88b6e5835db373d21.jpg

17. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Serikali ya mapinduzi Zanzibar hutumia magari yenye kibao chenye kuanziwa na herufi SMZ kisha kufuatwa na tarakimu kadhaa. Magari haya hutumika kwenye shuguli za kiserikali hivyo hupewa viongozi wa serikali katika ngazi fulani


18. JR- Jaji wa Mahakama ya Rufaa

19. JK- Jaji Kiongozi

20. J- Jaji wa Mahakama Kuu

21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)

22. CAG - Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

23. Magari ya watu binafsi
Magari ya watu binafsi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanza na herufi T kisha tarakimu tatu hufuata na baada ya hapo herufi tatu hufuata. Magari haya ya binafsi yanaweza kuwa ya biashara au la.

Pia kwenye magari ya binafsi ambayo sio ya biashara kunauwezekano kuwa na kibandiko ambacho kina jina mtu binafsi.

7832710ceee8ae678ff885687f150ebb.jpg
56948b739030cda3dfeaca98c548adc1.jpg
382a1430b3f1c04d345a7f8fd38b7832.jpg

NYONGEZA:
Magari yote haya huwa pia na tofauti katika rangi za plate number hizo, rangi hizo zinaingiliana sehemu na sehemu;

1. Magari yenye plate number za Rangi ya Njano
  • Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
  • Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Jaji Mkuu wa Tanzania
  • Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
  • Gari za Serikali za Mitaa
  • Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
  • Serikali ya Tanzania
  • Magari ya Wakuu wa Mikoa
2. Magari yenye plate number za rangi ya Kijani
  • Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
  • Magereza Tanzania
3. Magari yenye plate number za rangi nyeusi
  • Magari ya Police wa Tanzania (Maandishi ya rangi ya njano)
  • Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (Maandishi ya rangi nyeupe)
4. Magari yenye plate number za rangi nyekundu
  • Mkuu wa Majeshi (CDF) (Nyota zilizopo huwa na rangi ya dhahabu)
  • Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu toka nje ya nchi
5. Magari yenye plate number za rangi nyeupe
  • Magari kwa ajili ya biashara (Commercial Use)
  • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
6. Magari yenye plate number za rangi ya bluu
  • Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa
 
MT = Magereza Tanzania
PT = police Tanzania
SU = Shirika la Umma
SM = serikali za Mitaa
UT= uhamiaji Tanzania
RC = Regional commisioner
DFP= Doner Fund project
JW = Jeshi la wananchi
CD = magari ya ubalozi
J= magari ya majaji
SMZ = serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
W= mawaziri
NW = Naibu waziri
CS = katibu mkuu kiongozi
CAG= mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

Na mengine mengi tuu.
ZT= zima moto
 
STK serikari kuu ya tanzania
STK = ST + K
= Serikali ya Tanzania + Alphabet (a, b, c ..... z) .
Kila baada ya Gari 999 herufi ya mwisho inabadilika. Kwa hiyo kabla ya STK ilikuwepo STJ ; STL , STM zitafuata STK.
 
Back
Top Bottom