Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Hayo Magari ya # 12 hapo huwa yanapita njia gani Mkuu kwani binafsi japo niko ' down town ' kwa ' miongo ' mitatu sasa ya Uhai wangu lakini sijawahi kubahatisha kuyaona japo nina hamu sana niyaone.
Mitaa ya makumbusho barack obama na sarrender mkuu
 
Nimejifunza kitu.mungu akubariki muandaaji wa hii thread
 
Namba za magari ni mpangilio wa kuweza kutambua magari kwa sababu za usalama barabarani na kwenye matukio tofauti.Serikali na idara husika huweza kubadilisha mfumo wa namba za magari.
Kwa mfano wale tulio "wahenga"magari ya serikali yalikuwa na plate number inayoanzia na GT ikimaanisha Government of Tz,kila mji mkuu wa mkoa uliwa na namba zake kwa magari binafsi. Kwa mfano Mbeya - MB, Moshi -MS Tanga TA DSM - DS Arusha- AR Tabora -TB n.k. siku za karibuni tumebadilisha mfumo wa namba za magari kulingana na ule wa SADC mfano T 666 CCC
Siku za nyuma magari yanayotumia DFP yalikuwa yanatumia TX
 
1.T 000 xxx namba za magari ya watu binafsi na makampuni binafsi(ikiwa plate namba ni nyeupe basi ni gari ya biashara)
2.ST (kuanzia A mpaka sasa L yaani mfano STH,STK na STL) magari ya serikali kuuu
3.SU ni gari za mashirika ya umma
4.SM ni gari za serikali za mtaa( halmashauri)
5.DFP now DFPA gari ambayo yametolewa misaada yapo kwenye miradi fulani(donors fund projects)
6.T 000 CD 000 gari zinazomilikiwa na mashirika ya umoja wa mataifa pia kijan hutembelewa na wafanyakaz wa balozi mbali mbali
7.PT 000 police Tanzania
8.JW ni jwtz
9.UT uhamiaji Tanzania
10.FT fire Tanzania
11.MT magereza Tanzania
12.E,1or E2 kuendelea ni usalama wa taifa
13.kuna wenye majina yao binafsi
14.j ni namba za majaji
15.CAG mkakuzi mkuu wa serikali
16 kuna namba pia maalum kwenye gari ya rais makamu waziri mkuu spika na mawaziri

10: FT (fire Tanzania) sio sahihi. Inabidi iwe
ZT (zimamoto Tanzania)

12:E 1, E 2, inamaanisha hizo ni gari Za escort. Escort 1 (E 1) escort 2, (E 2)
 
4. Jaji Mkuu wa Tanzania
Gari la Jaji Mkuu wa Tanzania huwa na herufi JM kwenye kibao chake


Kuna jingine limeandikwa JK, tukaambiwa ni Jaji Kiongozi, je tofauti yao ni nini?
 
8. Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO). Kibao chenye namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na herufi CD kisha namba tena.

umoja-mataifa-jpg.836488
9. Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
Magari ya Ubalozi nchini Tanzania huanziwa na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD kisha namba. Pia namba hizi hutumiwa na wafanyakazi wa ubalozi husika hata kama ni watanzania. Mfano wa Ubalozi ni Marekani

balozi-jpg.836489


Mkuu, hapa ungeongezea kuwa number plates zao zinatofautiana kwa rangi,
UN - Blue
Balozi - Green
 
14. Magereza Tanzania
Magari ya Magereza ya Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi MT kisha hufuatiwa na namba kadhaa mbele yake kwenye kibao cha magari hayo

magereza-jpg.836496


Kuna moja nilikuta lina namba za mpangilio huu lakini kibao chake ni chekundu likiwa na bendera, mengine yana kibao chenye rangi hiyo na maandishi rangi hiyo, ila ni RAC, hayo ni magari ya watu gani?
 
Inakuwaje pale unakuta gari jipya kabisa lakini namba za zamani, kwa mfano kuna V8 moja mpya kabisa ina namba T804AVB
 
Escort 1 for president and so on


Kuna mmoja alikuwa analiosha gari la namna hiyo Benz pale Kijitonyama, akawakodishia jamaa kwenda walikokuwa wanakwenda sikujua kama lilikuwa ni gari la huko!!!!
 
Umesahau kuna magari huwa nayaona mitaa ya keko pale msd,mitaa ya Victoria (bagamoyo rd) kule wazo kama unaenda madale ya usajili wa UT afu plate number zake zimeandikwa kama za polisi...kwani hizo nazo niza serikali?
 
Back
Top Bottom