Uchaguzi 2020 Zijue sababu kuchelewa vikao Kamati Kuu ya CCM kupitisha Wagombea wa Ubunge

Uchaguzi 2020 Zijue sababu kuchelewa vikao Kamati Kuu ya CCM kupitisha Wagombea wa Ubunge

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Ratiba za kichama hapa Makao Makuu Dodoma zinaonesha kuwa vikao vya Kamati Kuu wa CCM almaarufu kama CC vilipaswa kufanyika tarehe 7 na 8 ya mwezi huu. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kikao cha Kamati Kuu kilichoketi hapa Dodoma au hata Dar es Salaam. Ajenda kuu ya kikao hicho ni kupitisha majina ya Wagombea wa Ubunge wa Majimbo wa CCM Tanzania Bara na Visiwani.

Zipo sababu mbili zilizochelewesha vikao vya Kamati Kuu. Kwanza, kuna tuhuma lukuki za rushwa kwenye mchakato wa kura za maoni majimboni. Taarifa zimemiminwa CCM kutoka TAKUKURU, waliogombea, makada hadi wananchi wa kawaida kuhusu vitendo vya rushwa kwenye kura za maoni chamani. Kamati ya Maadili ya chama imeelemewa na makabrasha ya tuhuma kutoka karibu kila mkoa wa Tanzania.

Katika hilo la rushwa, kuna wakubwa chamani wanataka itumike FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE katika kupata suluhu la jambo hilo. Yaani, rushwa isionekane kwenye macho ya wanaKamati Kuu na hivyo wagombea waangaliwe kwa vigezo vinginevyo kama kukubalika na si rushwa. Inapendeezwa kuonwa kuwa wagombea walizidiana dau wenyewe kwenye majimbo yao. Kuna mvutano mkubwa kwenye Kamati ya Maadili na hata baina ya viongozi waandamizi wa chama.

Sababu ya pili ni sauti za makada na wananchi kuhusu nani arudishwe wapi kugombea. Kuna waliokataliwa majimboni lakini wanatakiwa uongozini; kuna waliopita majimboni lakini hawatakiwi chamani na uongozini; kuna waliokataliwa lakini wanatakiwa huko huko majimboni. Kamati Kuu imetumia muda wa kutosha kutega masikio yake huko site ili kujiridhisha kabla ya kufanya uamuzi wake. Je, waliokatwa wataandikwa tena?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwa sasa jijini Dodoma)
 
Wawakate tu waliotoa rushwa wote na wafanye uamuzi based na advantage ya mtu utendaji wake. Ila CCM kwa rushwa kiboko hadi viti maalumu rushwa, hichi chama kwa kweli kijifikirie mtu anayetoa rushwa hafai maana ni adui wa haki.
 
Wawakate tu waliotoa rushwa wote na wafanye uamuzi based na advantage ya mtu utendaji wake. Ila ccm kwa rushwa kiboko Hadi viti maalumu rushwa, hichi chama kwa kweli kijifikirie mtu anayetoa rushwa hafai maana Ni adui wa haki.
Wakiwakata kwa rushwa mchakato unaweza kuanza upya[emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom