Zijue Sababu za Kwanini ni Wasira?, He is The Right Man at The Right Time & The Right Place. It Is A Project!, Ikikamilika, Atang'atuka, Kama Kinana!

Point ni ndogo tu baada ya miaka mitano ijayo kuisha watakuja na mitano tena umri sio inshu kama wasira😂😂😂
 
Kama tangu akiwa miaka 28 anaingia serikalini kama kiongozi hadi leo ana miaka 80 na bado taabu ni ile ile yaani nchi haijapiga hatua maridhawa katika Uchumi, Elimu, Huduma za jamii, Afya na Demokrasia, basi huyo mzee ni garasa kama wengine wa kaliba yake.

Endeleeni kusifiana lakini nchi inahitaji ukombozi na siyo maajuza waliotufikisha hapa
 
Uchawa mtupu ....
 
Kwa hiyo ule utabiri /maono Yako ya YEYE yamekufa?
 
Embu fatanua nyie mlioshuhudia mtanange huo ilikuaje? wkt wasira tyson anamtwanga mtu makonde walikua ni piga nikupige au ndg mwandishi alikua ana guard tu?
 
Wasira ameletwa Chamani kukiimarisha Chama kanda ya Ziwa. Full stop hakuna bla balaa.CCM ilipywaya sana huko,hii ni kumuongezea Doto Biteko nguvu.

Ila nasikitika kusema wamechelewa sana
Huyu huyu Wassira alipigwa KO na mwanamke kule Bunda?Hamna kitu hapo,Nimemuelewa Mchangiaji mmoja hapo juu amesema Tyson amewekwa hapo kama zunga lakini mtendaji yupo tena nachelea kusema hatokei kwenye chama bali TissCcm
 
Huyu mzee anajua.sana.kupangua hoja ndio maana ameteuliwa. Yuko vizuri kichwani.
Pia CCM imetengenza mfumo mwingine baada ya ule wa Kleptokrasia kwamba wakati wa dharura wana uwezo wa kufanya teuzi ambazo hazifuati taratibu.

Ni stratejia ilowekwa baada ya kuondoka kwa viongozi makini na twaweza kuiita hybrid rotation system yaani wateua hata mzee kama Wassira kwasababu licha ya umri alo nao lakini bado aonyesha ana uwezo mkubwa kiakili.
 
Paskali naheshimu maoni yako lakini sikubaliani na MTAZAMO wako.

Ni SIFA gani ambazo Wasira anazo baadhi ya vijana wenye 40 to 55 hawana ? Au ni SIFA gani ambazo Wasira anazo lakini over 60 years CCM imeshindwa kuandaa kijana mwenye sifa za Wasira ?

Vijana hawajioni kwenye nafas kubwa . Mwenyekiti wao ni mzee, inakuaje na makamu awe mzee, je tunawaandaaje vijana? Hii ndio sababu tukitafuta vijana makini kwenye high post hatupati……matokeo yake vijana wanapoteza confidence na kuchagua uchawi na mindless behaviorism
Wasira alipaswa kuwa mshauri wa chama na sio makamu

Hata ivyo najiuliza ni lini ile nafasi imeshikwa na KIJANA?
Mangulu alikuwa old man
Kinana alikuwa old man
Wasira old man

Au Mwenyekiti wanaogopa vijana wasije kupindua meza maana vijana wengi ni impatient

All in all , Katiba mpyq ndio mpango
 

Chawa wenyewe ndio kama mtoa mada. Kila kitu kwao ni kupongeza, kusifu, kupamba, kuhalalisha hata ambapo wanaona kuna makosa ila hawana ujasiri kusema ukweli.
 
😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…