Nicole 2021
New Member
- Aug 27, 2022
- 1
- 0
Hautojutia rafiki Kwa kuzijua Siri hizi Kwa afya Bora. Kwanini tuangamie Kwa kukosa maarifa?
Ngoja nikushirikishe tone la upendo rafiki yangu unayesoma Uzi huu.
Afya ni uhai, Kuna afya ya Mwili, ya Akili na afya ya Roho. Wengi wetu tunaijua Sana afya ya mwili ambayo tunaipata Kwa kula chakula Bora, maji na kufanya mazoezi. Sasa napenda kukushirikisha kuhisu afya ya akili na afya ya Roho ambazo tukizikosa uhai wetu unakuwa matatani, Tena heri kukosa afya ya mwili kuliko ya akili na roho.
Afya ya akili na roho inashibishwa Kwa Imani, upendo furaha na maadili mema. Kwa namna gani hizi Siri zinafanya kazi kulinda afya zetu?
Ni dhahiri kuwa Kama hatuna amani Rohoni, hatupendani, hatuna furaha, hamna maadili mema miongoni mwetu basi migogoro na mifarakano ya mara Kwa mara haitokoma, vivyo hivyo Afya zetu zitadhoofika.
Afya ya akili na roho zinahitaji kushibishwa, na na chakula chake ni Iman, matumaini, upendo na furaha. Hizi ndizo siri zilizojificha kwaajili ya afya Bora.
Afya Bora sio kula chakula Bora , maji na mazoezi tu bali pia kuwa na Imani, upendo,tumaini, utulivu na furaha afya itashamiri mara dufu.
Ambatana nami kuona ni Kwa namna gani Siri hizi zinavyofanya kazi kwaajili ya afya zetu.
Tuanze na Imani. Kuna msemo katika biblia unasema "Imani yako inakuponya ". Kumbe Imani ni afya, tukiwa na Imani hatuumwi ovyo. Imani inatufanya tu(relax). Kukosa Imani kunasababisha hofu na huzuni ambazo ni chanzo Cha maradhi kama vile (pressure), vidonda vya tumbo, kuchanganyikiwa nk. Imani ni kuwa na hakika ya Mambo yatarajiwayo, binadamu tumetofautiana Kuna wengine hawana subira kabisa, hawatulii mathalani wanapotafuta kufanikiwa, ndo maana wengine wanakuwa wezi, na wengine wanafanya Mambo yasiyofaa. Imani ni chakula Cha Roho na akili kwahiyo Imani ni afya.
Je, ulishawahi kumuuliza rafiki yako au mtu unayemfahamu kwamba umekuwa na afya nzuri maybe akakujibu nimeridhika tu, Sili hata chakula Cha kueleweka yani (balance diet) mlo kamili. Mtu huyo ametawaliwa na furaha, amani, uhuru, na upendo. Kila mmoja ajaribu Siri hizi ninazokumegea na utafurahi kusoma Uzi huu milele hatojutia.
Upendo nao unachukua hatamu katika afya zetu, bila upendo sisi ni watu bure. Tukipendana bila kujali makabila, dini na itikadi za kisiasa tutaishi Kwa afya ya mwili akili na roho. Upendo ni chakula Cha roho. Endapo roho ikikosa chakula chake afya mbovu itatuandama. Tukiishi Kwa upendo, utulivu na amani maradhi tunayosababisha
kwakukosa afya ya roho yatakuwa historia. Tupendane kuanzia kwenye familia zetu, na wote wanaowazunguka. Ubinafsi ni adui kiafya. Mimi nawapenda wote mnaosoma uzi huu na wale ambao hawataweza kusoma. Kwa upendo tuwashirikishe wengine kuhisu upendo Kama nyenzo ya afya Bora.
Furaha, Kila mmoja ana namna ya kujifurahisha. Furahi kadiri uwezavyo kwani furaha ni chanzo Cha afya bora. Usiruhusu moyo wako kuwa na huzuni hata mara moja kwasababu huzuni ni adui wa afya, huzuni hudhoofisha afya, huzuni huleta magonjwa.
Kwa kuhitimisha, napenda kutoa rai yangu Kwa jamii, asasi za kiserikali zikiwemo shule pamoja na asasi binafsi hasa zinazoshughulika na masuala ya elimu ya afya. Kama ambavyo tumekuwa tukielimishwa kuhusu afya ya Mwili ambayo imejikita kwenye kuhamasisha mlo kamili, kunywa maji na mazoezi iwe vivyohivyo kuhusu afya ya akili na roho ambayo imekuwa ikisahaulika na elimu yake kuwepo Kwa uchache. Na Kwa wasomaji wangu endapo ukiona inafaa Sana basi mshirikishe na mwenzio apate kunufaika kiafya.